Bilal Waikela ni nani?

Mkuu Kokola, asante kwa hoja murua kuzungumzia harakati za uhuru bila mrengo wa udini.

Paskali
 
Mkuu hii ya wasabato kuwa na shule nyingi kuliko makanisa mengine wakati wa Uhuru nao ni historia mpya kwangu, unaweza kuileza kwa mifano kwa kuangalia zilizokuwa shule za kisabato, kiislamu ,kiroman catholic ,ki Luther walau tuone picha halisi?
 
Shukran Mzee wangu Mohamed Said, na kuhusu kitabu ninacho na nimetoa tongotongo nyingi sana kunako historia ya nchi yangu
Binafsi nilielekeza swali hili kwa peterwapeter ili anishibishe kunako hoja yake aloijenga kwa kudhani juu ya mada yetu
Boywise,
Ahsante sana.
 
Tena dini zenyewe bora hata zingekuwa zetu kweli.

Zote za kuletewa na meli.

Zote zina mambo tofauti sana na tamaduni zetu.

Na tumezibugia kama mtu mwenye njaa kwenye dhifa.
Wewe utamaduni wako ni upi?
 
Maalim Muhammed Said, hoja ya Kokola iko very valid kwa hoja tuwazungumzie wapigania uhuru kama wapigania uhuru bila kuwanasibisha na udini kwa kutaja dini zao.

Hata kama waasisi wa African Association ndiyo hao walioasisi Al Jamiatul
Islamiyya Fi Tanganyika, na wote walikuwa Waislamu, hakuna sababu yoyote ya msingi kuinasibisha TAA na uislamu wa waasisi wake as if kutaka kuahadaa kuwa TAA ni zao la Uislamu wa waasisi wake kana kwamba kama sio Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika TAA isingezaliwa!. No! .

Hata kama Iddi Faiz ndie alikuwa mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika na kuja kuwa mweka hazina wa TANU, huo uweka hazina wake has nothing to do with Uislamu wake. Unaweza kabisa kuwaenzi babu zako na baba zako kwa michango yao kwenye kupigania uhuru bila kuwanasibisha na dini zao.

Sina kumbukumbu kama kuna Wakristu wamewashikia bango wapigania Uhuru wa Kikristu kwa kuwanasibisha na Ukristu wao. Idadi ya Waislamu kuwa ni wengi zaidi ya Wakristu sio kigezo cha kuzinasibisha na Uislamu as if nchi hii imekombolewa na watu wa dini fulani tuu, ili hali watu wa dini zote walishiriki na wengine kibao hawakuwa na dini nao pia walishiriki kikamilifu.

Tuwatambue na kuwaenzi mashujaa wa uhuru kwa michango yao na majina yao na sio kwa dini zao.

Paskali
 
Mkuu Alwatan
Asante kwa hoja maridhawa. Hatutaki ufia dini kwenye mijadala ya kisiasa.

Paskali
 
Paskali,
Mimi babu yangu Salum Abdallah aliwekwa kizuizini na hakuwa mtu mjinga.
Alikuwa mtu barabara sana.

1947 aliongoza ''general strike,'' dhidi ya wakoloni na akafanya hivyo 1949.

1953 alikuwa akihudhuria mikutano ya siri wakipanga kuundwa kwa TANU na
katika kundi lao wakamleta Germano Pacha Dar es Salaam kuhudhuria mkutano
wa TAA 1954 ulioasisi TANU.

1955 babu yangu akaasisi Tanganyika Railway African Union (TRAU) akiwa rais
muasisi.

1960 akiwa rais wa TRAU aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82.
Hii ilikkuwa haijapatapo kutokea.

Mgomo mrefu Afrika Mashariki ulikuwa ule wa Kenya ulioongozwa na Makhan
Singh.

Babu aliingoza TRAU ikishirikiana na TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hakuwa mtu, ''mjinga mjinga,'' au wa ''mchezo mchezo.''

Alikuwa na dereva wake Msukuma tulimpa jina, ''Msloopagas.''
Hadi leo sijajua jina lake halisi lilikuwa lipi.

Babu yangu aliwekwa kizuizini kwa sababu alitofautiana na Nyerere alipotaka
viongozi wa vyama vya wafanyakazi wavunje vyama vyao pawepo na chama
kimoja nchi nzima chini ya TANU.

Katika watu waliompinga katika mkutano wa viongozi wa vyama vya wafanyakazi
uliofanyika Moshi alikuwa babu yangu Salum Abdallah.

Hii ndiyo sababu ya yeye kuwekwa kizuizini mwaka wa 1964 akisingiziwa kuwa
alikuwa mmoja wa watu waliokula njama ya kupindua serikali wakati jeshi lilipoasi
Januari 20, 1964.

Babu yangu hakuwa mjinga wala mtu wa mchezo.
 
Mimi utamaduni wangu ni kutafuta ukweli, dini yangu ni mapenzi.
Utamaduni wenu unaosema ni tofauti na huo wa hao unaona wameubeba kutoka ng'ambo ni upi?:usikwepe swali
 
Maalim Muhammed Said, pole kwa yaliyomkuta Baba yako, hata Baba yangu yako yaliyomkuta. Mimi nimemzungumzia Muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni mtu very serious, alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo na hakutaka kabisa ujinga ujinga. Aliinyoosha nchi hii barabara kabisa kwa kuvunjilia mbali udini udini na ukabila ukabila ukabila kwa kuvunja uchifu.

Paskali
 
Al Watan nimeandika kitabu kizima ambacho kinaitwa, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes the Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika." Umuhimu wake ni kuwa walijitolea kupambana na ukoloni.
Sheikh! Neno linalowauma sana ni kusikia Waislam na Uislam katika harakati za ukombozi wa Tanganyika! Wakiwasoma kina Bwana Heri na Abushiri mitima inataka kuwapasuka!! Achilia mbali Mkwawa na Kinjekitile Mashujaa wa Taifa wanaojulikana lakini utambulisho wao ukizuiwa kujulikana kwa uwazi!
Huwa najiuliza kwanini "hawa jamaa zetu" wanaumia kwa chuki na hasama pindi uislam unapotajwa je ni zile chuki wanazopandikizana ama kuna jambo jingine limejificha maana tunahimizana utaifa huku wengine wakitajwa kuwa hawana sifa!!!
 
Paskali,
Mimi hapa nahadithia historia ya Mzee Waikela wewe naona umevutiwa
zaidi na mambo ya udini.

Ningefurahi kama unaijua historia ya Nyerere wakati wa kudai uhuru ukatueleza.

Wazee wangu walikuwa, ''very serious,'' katika suala la ukombozi na ndiyo maana
waliweza kuasisi TANU 1954 na kumpeleka Nyerere UNO 1955.

Mkusanyaji wa fedha za safari ya UNO alikuwa Idd Faiz Mafungo ambae alikuwa
mweka hazina wa TANU na mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya.

Idd Faiz kadi yake ya TANU ni namba 25.

Huyu na ndugu yake Idd Tosiri ndiyo waliompeleka Nyerere kumjulisha kwa
Sheikh Mohamed Ramia Bagamoyo.

Wazee wangu walikuwa watu, ''serious,'' walitembea na Nyerere nchi nzima
kudai uhuru wa Tanganyika.
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, hakuna mpenda haki hata mmoja anayekerwa na ukweli. Hivyo hakuna mtu yoyote anayekerwa au kuumizwa na ulichoandika, ila kuwa sisi baadhi yetu ambao ni waumini wa nothing but the truth, hatukerwi na over amplification ya the role of Islam kwenye harakati za uhuru, bali tunakerwa na "the I'll motive behind" haswa pale historia hiyo inapokuwa na over emphasis zenye urongo ndani yake just to make believe Uhuru wa Tanganyika ni kazi ya watu wa dini fulani pekee na baada ya uhuru, watu wa dini hiyo were marginalised kitu ambacho sii kweli.

Mimi ni miongoni mwa waumini wa Nyerere, whatever he did kwa kuzivunjilia mbali taasisi zenye mwelekeo wa kuleta fundamentalism Tanzania, he did it in good faith, and thanks to him tuko hapa tulipo kwa kazi yake nzuri iliyotukuka, otherwise saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine.

Mungu amlaze mahali pema peponi huyu Mzee, na sisi huku tuuharakishe mchakato wa kumtangaza Mwenye Heri ili soon atangazwe Mtakatifu Julius Kambarage Nyerere.
Paskali.
 
Mwanamageuko,
Hatuwezi kufuta historia hii itabidi wastahamili tu.

Kitabu nimekiandika cha historia hii na sasa tunakwenda
toleo la nne.
 
Mkuu Pasco, Je aliinyoosha nchi kwa kuwaweka watu waliomuonesha alipokuwa akikosea kizuizini ama?? Tuwatazame Kambona na bibi Titi walikuwa wadini au kuna jambo walilipinga halikumpendeza baba wa taifa na ndipo wakanyooshwa na matokeo ya makosa yale yanatugharimu mpaka leo. Mkuu Pasco Historia ya Tanzania toka awali hata kabla ya mjerumani hakukuwa na ubaguzi wa kikabila wala dini. Yako mema ya Mwalimu ni kuimarisha sio kuasisi ama kuvunja ukabila binafsi Babu yangu alioa mkewe wa kwanza Uvinza mwaka 1903 na hakubaguliwa kuwa si mwenyeji wa pale. Pia alioa mke wa pili Tabora 1918 hakubaguliwa, Najiuliza ingelikuwa kuna ubaguzi wale manamba waliopelekwa na mjerumani Tanga hali yao ingekuwaje ugenini? Yako mambo yanapotoshwa kwa makusudi na "wanaotunga" Historia na matokeo yake historia potofu inawatolesha watu povu!!! Mwalimu alitengwa hata na ndugu yake wakati wa kutafuta uhuru na akakimbilia Ikizu kwenye pango ambako alijificha akiandika katiba. Hili haliandikwi ndio maana hata Chief Makongoro Matutu wa Ikizu hajulikani!!! Ilikuwaje Mu Ikizu ampokee Mzanaki kama kungelikuwa na ubaguzi? Ilikuwaje wapwani wampokee mbara kwenye ubaguzi??Ilikuwaje waislamu wampokee mkristu na kumpa nafasi kwenye udini??? Wako walioujenga udini na wanaupalilia nani anawataja na kuwagusa??? πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Paskali,
Sina ugomvi na fikra zako wala sikuzuii kuamini na kuandika upendacho.
Mie naandika historia kama niijuavyo na wala simlazimishi mtu kuniamini.
 
Paskali,
Sina ugomvi na fikra zako wala sikuzuii kuamini na kuandika upendacho.
Mie naandika historia kama niijuavyo na wala simlazimishi mtu kuniamini.
Asante, tuendelee na mnakasha ila uwezo to read in between the lunea, "the ill motive behind" maandiko fulani, is very important tool kuzuia kuwa carried out na the intended "ill motives" zinazojificha ndani ya maandishi fulani yenye nia ovu ya kupanda mbegu fulani za udini udini in a pretext ya kuhifadhi historia za mababu zetu!.

Tunamshukuru sana Mwalimu Nyerere, naye alikuwa na uwezo huu na kiukweli alibaini mapema na aliinyoosha bila kujali wahusika ni wapigania uhuru wenzake na walichangia nini kwenye TAA au kwenye kuasisi TANU!, hakutaka ujinga ujinga na alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo na kiukweli aliwanyoosha!.

Paskali
 
Mkuu Pasco msome Madaraka Nyerere anavyorudia kuandika historia kisha nayeye umuweke kwenye fungu hilohilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…