Hakuna Mungu huyu tuliyeletewa kwenye vitabu. Hayupo. Katungwa na watu tu.
Habari za Uislamu na Ukristo ni tamaduni za watu wa nje tumepandikiziwa tu sisi Waafrika na sasa zinataka kutumaliza.
Tamaduni za uongo wa kijinga sana unaokuambia Wayahudi ni taifa teule la Mungu. Hivyo wewe Mzaramo huna maana kwa Mungu kulinganisha na Myahudi.
Ujinga sana.
Tamaduni zinazokuambia ukisali angalia Maka. Kama vile Mungu anakaa Maka. Kama vile kwenu Africa si muhimu Maka ndiko muhimu.
Ni njia ya kuku control kisaikolojia ufikiri Muafrika hana maana. Mwenye maana Muarabu na Myahudi.
Ujinga mkubwa sana.
Ukitaka kujua hilo angalia Quran na Biblia vitabu vyote hivi vimejaa logical contradictions kiasi kwamba haiyumkiniki kwamba ni vitabu vya Mungu.
Ukielewa hili, haya mengine ni mambo ya siasa za watu tu zinazotaka kujipaza juu kwa kutumia madhabahu ya dini za uongo na Mungu ambaye hayupo.
Waafrika weusi wanajifanya wanaujua Uislamu na Ukristo kupita Waarabu na Wayahudi.
Lakini historia za Waafrika na tamaduni zao wengi hata kuzijua hawazijui.
Aibu kubwa.