Bilionea Dangote anataka kuinunua Arsenal

Bilionea Dangote anataka kuinunua Arsenal

Najua ni mfanyabiashara anayehitaji faida, lakini naona kama angenunua tu klabu moja katika nchi yoyote AFRIKA na aipaishe, mbona TP Mazembe wameweza kupitia yule tajiri Katumba(kama sijakosea jina), Waafrika tujaribu kuvipaisha vya kwetu kwanza.

Ni Moïse Katumbi mkuu
 
Dunia ya leo ni pesa inaongea. Wazungu pamoja na ubaguzi wao wamenyiosha mikono kwa fujo za waarabu. Mnigeria aweke pesa ndefu tu mbona timu atapata?
 
Mohamed El Fayeed anamiliki Fulham, na ni mtu kutoka Libya...

Anatoka Misri, El Fayeed alishaiuza hiyo timu miaka kama 2 iliyopita. Anayemiliki timu hivi sasa ni Mmarekani wa kipakstani Shahid Khan ambaye pia anamiliki timu ya NFL Jacksonville Jaguars.
 
Mbona mzee aKILI MALI a.k.a Abramovic ukimunulia sofa zenye rangi nyekundu tu tayari ume mmaliza kwani yeye aliiisha sema kuwa furaha yake ni kumkalia mbaya wako, na ndo maana hata nyumbani kwake kaweka kapeti na sofa zenye rangi nyekundu kwa nia kukomoa .na hivyo nafsi yake hutulia.
Pg.24%5B1%5D.JPG
maji.jpg
yahaya+akilimali.jpg

Hivi vizee dizaini hii ndivyo vinadumaza soka la Bongo. Si Yanga Si Simba. Mziray alisema Yanga na Simba zikifa kesho kuna watu wengi watakufa kwa njaa. Watu kama hawa hawana new ideas wala nini ni siasa na kelele tupu ndani ya vilabu. Hii sio katika soka tu hata katika Siasa za nchi watu wanaendekeza nchi au vyama viongozwe na wazee wasioleta new ideas, new challenges bali wanakazania watakula nini joni na kesho badala ya kuweka mikakati ya maendeleo ya mbeleni. Tanzania kwa ujumla hatutafika mbali si kimaisha tu bali hata kisoka kama wazee kama hawa wasio na new ideas za karne hii wataendelea kuendesha vilabu na nchi yetu.
 
Dunia ya leo ni pesa inaongea. Wazungu pamoja na ubaguzi wao wamenyiosha mikono kwa fujo za waarabu. Mnigeria aweke pesa ndefu tu mbona timu atapata?

Inategemea mkuu. Pesa ndio zina matter lakini kuna club nyingine hata uje na pesa huwezi kuzinunua mf timu za Spain. Vile vile wafanyabiashara wanazingatia vitu vingi wakati wa kununua timu (kibiashara zaidi). Lazima wajue biashara ya soka inavyoendeshwa kabla ya kununua timu.
 
Wazungu hawatakuwa tayari kumuuzia Muafrica timu.. It'll be shame to them..

Hawa watu sio binadamu wenzetu kabisa, wana roho za ajabu sana..

you are wrong brother, watauza kwa bei sahihi watakapohitaji kuuza, kwa mtu yeyote mwenye vigezo.
 
Back
Top Bottom