ze-dudu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 17,640
- 22,748
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani hukuona video mzee!Pesa ni nyara za serikali, hakuna ujinga kama huo utafanyika.... hivi yule Ivan wa Zari si ilikuwa stori hizi hizi!
RipMarafiki wa milionea raia wa Zimbwabwe, Genius Kadungure aliyejulikana kama Ginimbi kwa muktadha wa kijamii, wamesema atazikwa na gunia lilojaa Dola, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Mfanyabiashara huyo aliyeishi maisha ya kifahari aliacha maagizo hayo kwa wanachama wa "all-white funeral", kama ilivyoandikwa na gazeti la Herald.
Ginimbi alifariki kutokana na ajali ya gari Jumapili, jijini Harare pamoja na mlimbwende Mitchelle Amuli aliyejulikana kama Moana.
Familia ya Moana imetaka fedha za mazishi kutoka kwa wanaowafariji.
Familia imeahirisha mazishi kwa wiki mbili ikisubiria majibu ya DNA na kukusanya michango ya kifedha kwa ajili ya kumuaga kwa heshima, imeripotiwa na Zim Morning post.
Matajiri wa Zimbabwe wamekuwa wakiahidi fedha kwa ajili ya mazishi ya Ginimbi.
Naibu Waziri Tino Machakaire ameahidi kununua jeneza kubwa kwa ajili ya Ginimbi, Mbunge Temba Mliswa amechangia wanyama wengi kwa ajili ya kuchinjwa kwenye mazishi hayo.
Wakati mwanasiasa Acie Lumumba ameahidi lita 1000 za mafuta ya dizeli, kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya ndani.
Ginimbi na Maona kwa pamoja walikuwa wanatoka kwenye sherere ya "all-white" ambapo gari yao iligongana na gari nyingine iliyokuwa inakuja mbele yao, ilichepuka nje ya barabara na kugonga mti kisha kulipuka moto.
Kwanini Waafrika tunajiita majina ya ajabu na kujishushia Heshima wenyew kisa Mtu flan kaamua azikwe na hela..
Why unasema MIAFRIKA haina akili?
Kwani Hao wazungu hawafanyi haya? Mbn tumezidi kujichukia?