Bilionea Mengi atoa darasa kwa Muhongo

Bilionea Mengi atoa darasa kwa Muhongo

Gefu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
6,930
Reaction score
2,565
Akiongea kwa kujiamini,bilionea Mengi leo wakati akikabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la ujasiliamali,ametoa darala na kujibu hoja ya waziri Muhongo kwamba wafanyabiashara wa tanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye mafuta.

Akijibu hoja hiyo kwa kujiamini na kicheko cha kuonyesha kuwa waziri hakuwa na tafsiri sahihi ya neno mtaji alisema, "mtaji si pesa pekee,bali pesa ni sehemu ya mtaji. Kikubwa ni wazo na fursa ya rasilimali tulizonazo ambazo tunaweza kuzitumia kama mtaji wa kuingia ubia na wawekezaji wakubwa"

Wakichangia washindi wa ujasiliamali walisema mafanikio yao hayajatokana na fedha,bali wazo ndo lilileta fedha. Mtazamo huu wa Mengi unawiana na ule wa rais mstaafu wa awamu ya tatu ambapo alihanikiza kauli mbiu ya "mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe" na kudiriki kumzawadia mtaji mlemavu aliye beba ujumbe huu. Nawasilisha...
 
Unajua hapa ni kutoelewana kwa hawa waheshimiwa.
Kila mmoja na tafsiri yake.

Jana nilmfuatilia Mzee Mengi na nimekubali mawazo yake.

Unajua Waziri alionyesha dharau kwamba watanzania hakuna mwenyekuweza ku afford gharama zake.

Je Mabilionea wa Tanzania anajua pesa walipata wapi?na muda gani wameanza kufanikiwa kwenye biashara zao?na anajua kipato chake?
Hivi ni Benki gani haiwezi kumkopehsa mzee mengi,na je wahisani wenzake kwenye biashara Nje ya nchi Serikari Inawajua?
Na je serikali kweli imethamini mchango wake kwa kuajiri watu wengi kwenye miradi yake?achilia mbali hisani za kibinaadam anazofanya.

Huu mradi mie naona kuna watu wameishalengwa,na wakuu wanalijua hilo.
Kwani nani haju kama CRDB imekopesha marangapi pesa Serikali hii,na hiyo pesa inashindwaje kukopesha Matajiri wa nchi hii.
Na yeye hajui kama Hao matajiri wanaweza kujiunga na kufanya mapinduzi ya miradi mikubwa kama hiyo?

Mie mwenyewe naona ni Dharau sana kuwaambie kwamba watanzania hawana mitaji mikubwa ya kuwekeza kwenye Mafuta,Miradi ya gesi yenyewe zengwe tupu.
We jitokeze tu Mtanzania uone Terms utakazopewa.

Tubadilike.Nchi hii kuna watu wanapesa na wanaweza kufanya lolote kama hao wa nje wanavyoeweza kufanya hapa nchini.

Serrikali hapa inachojaribu kufanya ni kuwabana kina mzee mengi na wenzie,na utaratibu unaotumika ni kwamba lazima waonyeshe mitaji yao wenyewe bila ya kuwa na mshirika.Na wanajua hapo watashindwa/
Cha kushangaza ni kwamba hao wa nje wenyewe wakija lazima wajiunge ndio waweze kufanya miradi hiyo.
 
tatizo uongozi siyo kufahamu kilakitu. kiongozi kaa na wadau wakujuze siyo ifikie ionekane watanzania hatuwezi kilakitu.no dhambi
 
Weka Mezani 100 Billion unapewa Kitalu cha Gesi, hakuna kutumia Kigezo cha Ngozi au Uraia kuanza bishara za kimachinga machinga za 'Upungufu unaonge mara wee kwan una shing ngapi?
 
Ni katika kudandia Mada .... Hivi ni Mamlaka gani hapa Nchini inayotunukia watu U-Bilionea na U-Milionea? Hivi ili mtu uitwe Milionea au Bilionea ni lazima utimize vigezo gani?
 
kama ana hela si ashindane na wenzie, ye kwanini anataka kupendelewa? vitalu mali yetu watanzania sote na tunawakilishwa na TPDC nukta!
 
...mkuu nimekuelewa sana, serikali ya marekani inatoa ruzuku kwa wafanyabiashara waweze kuzalisha na kushindana katika soko, tanzania ni nchi pekee ambayo wafanyabiashara wakubwa wanadharaulika,tena hadharani. serikali inashindwa nini kumsapoti mzee mengi hata akapewa mkopo na ADB..? hivi mengi hawezi kupata kibali na akajiregista kwenye masoko ya hisa ya kimataifa akapata wabia. no wonder ruzuku zinaenda kwenye vyama vya siasa badala ya wafanyabiashara waaminifu kama mzee Mengi...
 
kama ana hela si ashindane na wenzie, ye kwanini anataka kupendelewa? vitalu mali yetu watanzania sote na tunawakilishwa na TPDC nukta!

...hataki kupendelewa ila kauli ya waziri ndo inawabagua wawekezaji wazawa kwamba hawana uwezo, na serikali inataka mtu aje na mabilioni aweke mezani ndo apewe tenda. biashara haiendi hivyo,hata kama wewe si mfanyabiashara lakini utakuwa umesikia neno 'malikauli' manayake biashara ni zaidi ya cash in hand, namuunga mkono Mengi...
 
Waziri Muhongo - ninathubutu kusema ni wa hovyo sana! Mpuuzi na pengine -------- ila sio Mjinga! Nilimsikiliza jana akisema Watanzania ni wavivu kusoma! Wavivu kusoma! Eti kama kuna mtu ana mashaka na mikataba aende pale Wizarani akaisome! Kama mikataba hio inaweza kusomwa na anayetaka kwa nini isiwekwe mahali pa ujumla kama Maktaba kuu ya Taifa au kwenye website ya Wizara tukaisoma huko. Je ukweli kwamba watu wengi wanaingia kwenye media kama jf au fb haitoshi kumwonyesha watanzania sio wavivu wa kusoma kama yeye? Yeye baada ya kupata uprofesa, amesoma au kuandika nini? Huyu ndiye MVIVU wa Kufikiri na wa Kusoma! Watanzania tuko tofauti, na ndio maana hajui hata kuwa wapo Watz mabilionea! Mpuuzi sana huyu!
 
Ni katika kudandia Mada .... Hivi ni Mamlaka gani hapa Nchini inayotunukia watu U-Bilionea na U-Milionea? Hivi ili mtu uitwe Milionea au Bilionea ni lazima utimize vigezo gani?
..lazima uwe na mabilioni mfukoni, lakini sio za epa, kwa bongo sijawahi sikia taasisi yoyote inayo fanya utafiti juu ya uwezo wa wawekezaji. kwa kimataifa zipo institutions zinazo dili na mambo ya uchumi, huwa za nje zinaendesha huu utafiti kila mwaka na ni muhimu sana kwa wawekezaji na taifa...
 
Waziri Muhongo - ninathubutu kusema ni wa hovyo sana! Mpuuzi na pengine -------- ila sio Mjinga! Nilimsikiliza jana akisema Watanzania ni wavivu kusoma! Wavivu kusoma! Eti kama kuna mtu ana mashaka na mikataba aende pale Wizarani akaisome! Kama mikataba hio inaweza kusomwa na anayetaka kwa nini isiwekwe mahali pa ujumla kama Maktaba kuu ya Taifa au kwenye website ya Wizara tukaisoma huko. Je ukweli kwamba watu wengi wanaingia kwenye media kama jf au fb haitoshi kumwonyesha watanzania sio wavivu wa kusoma kama yeye? Yeye baada ya kupata uprofesa, amesoma au kuandika nini? Huyu ndiye MVIVU wa Kufikiri na wa Kusoma! Watanzania tuko tofauti, na ndio maana hajui hata kuwa wapo Watz mabilionea! Mpuuzi sana huyu!
... na kwanini wasiiweke kwenye website yao, yaani watu tuache kazi na shughuli zetu tukaweke foleni ya kusoma mikataba..? nadhani huyu mzee ni mvibu wa kufikiri kwa kina...
 
Weka Mezani 100 Billion unapewa Kitalu cha Gesi, hakuna kutumia Kigezo cha Ngozi au Uraia kuanza bishara za kimachinga machinga za 'Upungufu unaonge mara wee kwan una shing ngapi?

...lohh mkuu hii sheria mpya ya uwekezaji imepitishwa kwenye bunge la juzi..? nijuze mkuu maana sikufiatilia kwa karibu....
 
...hataki kupendelewa ila kauli ya waziri ndo inawabagua wawekezaji wazawa kwamba hawana uwezo, na serikali inataka mtu aje na mabilioni aweke mezani ndo apewe tenda. biashara haiendi hivyo,hata kama wewe si mfanyabiashara lakini utakuwa umesikia neno 'malikauli' manayake biashara ni zaidi ya cash in hand, namuunga mkono Mengi...

Kama sikosei serikali imesema TPDC na wawekezaji watamiliki kwa uwiano wa 75%-25%. Kwa hiyo wanachoshindania wawekezaji ni nafasi ya kuingia ubia na TPDC kwa 25%. Hapa serikali haijamzuia Mengi wala mtu mwingine yoyote kushindania nafasi hii. Sasa niambie sababu gani ya msingi ya kumpendelea mtu mmoja anayejiita mzawa katika kupata hiyo nafasi, wakati Taifa linataka faida.
 
-------- hata awe na kontena la mavyeti ya ilimu upumbavu haupungui
 
Weka Mezani 100 Billion unapewa Kitalu cha Gesi, hakuna kutumia Kigezo cha Ngozi au Uraia kuanza bishara za kimachinga machinga za 'Upungufu unaonge mara wee kwan una shing ngapi?

mengi ana utajiri zaidi ya Billion 900, hawezi shindwa...
 
Hao wawekezaji anaowataka muhongo wanakuja kukopa kwenye bank zetu za ndani...
 
Kama sikosei serikali imesema TPDC na wawekezaji watamiliki kwa uwiano wa 75%-25%. Kwa hiyo wanachoshindania wawekezaji ni nafasi ya kuingia ubia na TPDC kwa 25%. Hapa serikali haijamzuia Mengi wala mtu mwingine yoyote kushindania nafasi hii. Sasa niambie sababu gani ya msingi ya kumpendelea mtu mmoja anayejiita mzawa katika kupata hiyo nafasi, wakati Taifa linataka faida.

....kwanza hapo kwenye red, taifa litapata faida zaidi kama tenda hii italwenda kwa mzawa na si mgeni. hebu fikiri kama asilimia 97 wanazochukua wawekezaji wa kigeni kwenye dhahabu kama zingechukuliwa na mzawa ingekuwaje kwa taifa letu. pili mzee mengi hajataka kupendelewa, lakini anataka wasiwekwe kwenye kapu moja na wawekezaji wa kigeni ambao wao waki bid pamoja na akina mengi na wenzake lazima wao watashinda kwakuwa wanamitaji mikubwa. kwani mbona magufuli ameweza kuwapa kazi makandarasi wazalendo na wakaweza..?
 
Back
Top Bottom