Watanzania tusiwe wajinga huyo Singasinga hana makosa, ataondoka Seth Singh atarudi mwengine kwa jina lengine, Serikali wenyewe inapotafuta mwekezaji inatafuta aliye mjanja wa kuweza kula nae,haiwezi hata siku moja kampuni safi inayofuata haki kupata kazi au kushinda Tenda.Tuna treni tunaambiwa inataka kujengwa Kwenda na kurudi Airpot inafaida saana na sisi, hivi hiyo reli itatusaidia nini sisi kama sio ulaji kwanini badala yake mwekezaji atafutwe wa kuwekekeza reli ya kwenda mikoani itasaidia kuleta abiria na kuboresha hali ya wananchi wanaofanya kila aina ya biashara.
Huyo singa kalazimishwa kuchukua hiyo pesa na kapewa hela yake halali,walokula hela ya umma ni hao waliogawana mapesa kwa viroba, ni wazi wamemwambia chukua halali yako sisi tuachie hizi kodi na malipo ya serikali tutashughulika nazo wewe usijali.
Tujiulize tunataka tuchukue kiwanda tumpe nani Tanesco, shirika ambalo linajiendesha kwa hasara kutokana na wizi wa wabilioni, hasara ambayo inabebwa na wananchi, hamuoni afadhali huyo singa kiwanda kinatupa umeme ila kisimamiwe vizuri na serikali, tukiwakabidhi Tanesco hata mwaka hakichukui kitakufa. Tujiulize tulikua na viwanda vingapi hapa nchini na sasa vipo wapi? Tumeshindwa kuviendesha na vikauzwa kiujanja ujanja kwa wawekezaji feki mpaka sasa hakuna kinachofanya kazi na mashine zimengolewa kupelekwa nje ya nchi wamebakisha majengo.
Bora tumuache huyo Singa yeye sio taizo, tatizo ni hawa waliochukua pesa na na wakawana na kula ndiyo wamechukua za Umma kodi zetu na malipo mengine, huyo singa kachukua kilicho chake.
Tusifanye mambo kwa jazba tatizo tunalo sisi siyo singa, ndiyo maana majanga kama haya yanajirudia. Ukiona mkeo anatembea nje,muue mkeo sio mwanaume kwasababu ukiua mwanaume,mke ataleta mwanaume mwengine utaua wangapi????