Bilionea wa Nigeria amzawadia Tayo $350,000 baada ya kushindwa kuzinyakua $300,000 za BBA Hotshot

dexterous

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
2,037
Reaction score
3,134
Imeripotiwa kuwa baada ya mshiriki wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Afrika, Tayo kuzikosa dola laki tatu za Biggie zilizomwendea Idris wa Tanzania Jumapili iliyopita, mshiriki huyo wa Naija amezawadiwa $350,000 sawa na zaidi ya milioni 600 kutoka kwa shabiki wake bilionea.

Bilionea huyo aitwaye Ayiri Emami ameamua kuongeza dola 50,000 juu zaidi ya ile ambayo ilitolewa na Biggie ambayo ni $300,000 kutokana na kuwa shabiki mkubwa wa Tayo.

Staa wa Nigeria Davido ameshare picha ya story hiyo Instagram na kuandika "we do this easy, bar dey".

Inasemekana hii si mara ya kwanza kwa bilionea huyo kumwaga mkwanja mrefu kwa wasanii anaowapenda, aliwahi kufanya hivyo kwenye harusi ya 2Face 2010 ambapo inasemekana alitoa zaidi ya Naira milioni 20 (sawa na zaidi ya Tsh 189,000,000) na kumzawadia Range Rover mpya, na pia alimzawadia msanii mwingine aitwaye Durella gari aina ya Toyota Prado Jeep.

=======================

Chanzo: MillardAyo.com

========

UPDATE: Mshindi wa Pili wa BBA Hotshots 2014: Akanusha kupewa pesa na tajiri wa Nigeria


 
mmmh hii kali....yani hawataki kushindwa.....aya nigeria hongera zenu......
 
Either way...ushindi bado utabaki kwa Idriss tu hata kama angepewa billion 321
 
Ni juzi tu tulishuhudia ushindi wa kijana wetu idris ndani ya jumba la BBA akijinyakulia kitita cha dola 300000 na kuwaacha wenzake patupu hasa mshindi wa pili kutoka Nigeria mr R

Jamaa kahuzunika sana na akawa myonge ile mbaya sasa kilichonifanya nivute huu uzi hapa ni leo hii tajiri mmoja au bilionear wa kineigeria kaamua kumpa mshikaji ali aondokane na unyonge wa kutoka patupu kitita cha dola 350000 ni.zaidi ya kile cha kwenye mjengo hii sijui kama ingekua tz ingekuaje
 
ni kama kushow off,wanasahau ile ni tuzo inaweka historia na heshima tena africa lote.

True...inaonekana imewauma sana kukosa tena mwaka huu, tatizo wanajiona wapo superior sana siku hizi, ila ukweli unabaki palepale na historia tayari ishawekwa
 
Ebwana inaonekana wanaigeria wamekasirika sana huo ushindi wa Idris.
 
Hii ishu inanikumbusha Munya wa Zimbabwe
 
Kaamua kumpa mnajeria mwenzake mkwanja easy like that. .cjui hawataki kushindwa mnayosema nyie..kwani ni mara moja ishu kama izo kutokea...
 
Angempa hata trillion lakini kaweka history tayari kuwa ni mshindi wa Bba hotshosts kimewauma sana watajibeba
 
Wanaigeria kwa sifa wakati kuna mafukara wa kutupwa
 
Asilimia kubwa ya Wanaigeria hawana sehemu ya kulala, wanalala mabarabarani na chini ya madaraja, ni masikini wa kutupwa,
 
Rugemalila mbona amumpi pongezi alitoa million 400 mchango wa harusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…