Bilioni 100 kusambaza umeme mitaa inayofanana na vijiji

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
815
Reaction score
733
1591105612528.png

Serikali kupitia Wizara ya Nishati, imetenga Sh 103.8 kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye mitaa inayofanana na vijiji mkoani Lindi. Hayo yameelezwa na waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani juzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa miundobinu ya gesi asilia majumbani mkoani Lindi uliofanyika katika Kata ya Mnazi Mmoja Manispaa ya Lindi.

Kalemani amekiri kuna maeneo ya mjini ambayo mengi yaliitwa kama mitaa na si vijiji wakati kuna mitaa ambayo haina tofauti na vijiji.

“Tumeshatoa maelekezo kuwa mitaa yote inayofanana na vijiji iwe kwenye miji, Manispaa ama majiji yote ipelekewe umeme kwa Sh 27,000,” amesema.

Aidha, amesema fedha hizo zimetengwa katika bajeti ya mwaka 2019/2020 huku akimsisitiza Meneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Kanda ya kusini, Feisian Makota kuzingatia na kuanza kutekeleza maagizo hayo kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Awali akimkaribisha Waziri wa Nishati kuzungumza na wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alimuomba waziri huyo kuangalia namna ya kuwaunganisha wananchi wanaoishi katika maeneo hayo sawa na wale wa vijijini ambako miradi ya REA inatekelezwa.
 
Mmeanza wizi eti maana mmeshaanza kutoa tenda kununua majenereta Wakati ,mlitaifisha ya aggreco,symbion power wizi uleule wa mambo ya umeme umerudi upya.
 
Niwaombee tu mkamilishe katika matendo.Sio maneno.
 
lindi ndio mnaombwa kura hivyo sasa kisha tukutane 2024.
 
Serikali kupitia Wizara ya Nishati, imetenga Sh 103.8 kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye mitaa inayofanana na vijiji mkoani Lindi. Hayo yameelezwa na waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani juzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa miundobinu ya gesi asilia majumbani mkoani Lindi uliofanyika katika Kata ya Mnazi Mmoja Manispaa ya Lindi.

Kalemani amekiri kuna maeneo ya mjini ambayo mengi yaliitwa kama mitaa na si vijiji wakati kuna mitaa ambayo haina tofauti na vijiji.

“Tumeshatoa maelekezo kuwa mitaa yote inayofanana na vijiji iwe kwenye miji, Manispaa ama majiji yote ipelekewe umeme kwa Sh 27,000,” amesema.

Aidha, amesema fedha hizo zimetengwa katika bajeti ya mwaka 2019/2020 huku akimsisitiza Meneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Kanda ya kusini, Feisian Makota kuzingatia na kuanza kutekeleza maagizo hayo kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Awali akimkaribisha Waziri wa Nishati kuzungumza na wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alimuomba waziri huyo kuangalia namna ya kuwaunganisha wananchi wanaoishi katika maeneo hayo sawa na wale wa vijijini ambako miradi ya REA inatekelezwa.
Haya ndio maendeleo makubwa tunayo yazungumzia.
P
 
Kwamba Serikali iliyoko madarakani imejikita katika naendeleo ya vitu ni msingi sahihi wa maendeleo ya watu kijamii, kisiasa na kiuchumi. Siyo rahisi kuendeleza watu bila kuwa na nyezo za kufanya hivyo. Maendeleo ya vitu huchochea maendeleo ya watu. Mifano:
• Umeme wa uhakika utachochea kuanzishwa viwanda;
• Uwepo wa viwanda utahitaji miundo mbinu imara na bora ya usafirishaji (barabara, maji, reli na anga) wa malighafi na bidhaa zitakazolishwa viwandani;
• Miundo mbinu itaongeza uzalishaji wa malighafi za viwandani (mazao ya kilimo, uvuvi, mifugo, madini, nk);
• Kuongezeka kwa mahitaji ya malighafi za viwandani kutachochea uzalishaji wake na hivyo kukuza kipato cha wazalishaji, ambao ndio watu wenyewe.
• Isitoshe, kuongezeka kwa viwanda kutapanua wigo wa mahitaji ya ajira na kuinua pato la Taifa; na
• Pato la Taifa likiongezeka, Serikali inakuwa na uwezo wa kupanua na kuboresha huduma za jamii (elimu, afya na maji) zinazogusa maisha ya mtu kwa kila siku.

Tuipongeze Serikali kwa uamuzi wake wa kusambaza umeme kila kona ya nchi kwa bei inayoakisi kipato cha wananchi wengi.
 
Back
Top Bottom