Bilioni 4.14 Zakamilisha Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Morogoro

Bilioni 4.14 Zakamilisha Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Morogoro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

BILIONI 4.14 ZAKAMILISHA MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MOROGORO

Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ilipokea fedha jumla ya Shilingi Bilioni 4.14 (Tsh. 4,140,000,000) kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Hospitali ya Wilaya katika Makao Makuu ya Halmashauri yaliyopo Kata ya Mvuha.

Hadi sasa majengo 16 yameshakamilika kwa asilimia 99% ikiwemo jengo la maabara, jengo la mionzi, jengo la mama na mtoto, jengo la dawa, jengo la wagonjwa wa nje, jengo la utawala, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la dharura, jengo la mionzi, jengo la kufulia, wodi ya upasuaji kina baba na kina mama, wodi za wanawake, wanaume na watoto.

Vilevile, Hospitali imeshapokea vifaa tiba mbalimbali vyenye jumla ya TZS 887,768,111.24 na Watumishi wanaendelea kutoa huduma mbalimbali zikiwemo huduma ya wagonjwa wa ndani na nje, vipimo vya maabara, huduma za mionzi, huduma za kinywa na meno Pamoja na upasuaji.

Kwa ujumla Uongozi wa Halmashauri pamoja na Wananchi tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita kupitia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwa kuwaboreshea huduma za afya.
 

Attachments

  • Screenshot 2024-08-13 at 18-29-27 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    Screenshot 2024-08-13 at 18-29-27 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    888.6 KB · Views: 11
  • Screenshot 2024-08-13 at 18-29-34 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    Screenshot 2024-08-13 at 18-29-34 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    841.3 KB · Views: 11
  • Screenshot 2024-08-13 at 18-29-39 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    Screenshot 2024-08-13 at 18-29-39 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    885.1 KB · Views: 11
  • Screenshot 2024-08-13 at 18-29-44 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    Screenshot 2024-08-13 at 18-29-44 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    844.2 KB · Views: 10
  • Screenshot 2024-08-13 at 18-29-49 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    Screenshot 2024-08-13 at 18-29-49 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    699.5 KB · Views: 12
  • Screenshot 2024-08-13 at 18-29-53 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    Screenshot 2024-08-13 at 18-29-53 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    478.3 KB · Views: 9
  • Screenshot 2024-08-13 at 18-29-58 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    Screenshot 2024-08-13 at 18-29-58 Joanfaithkataraia (@joanfaithkataraia) • Instagram photos an...png
    419 KB · Views: 10
Back
Top Bottom