Bilioni 63.2 za Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), zasainiwa ili kuwezesha Taasisi za Fedha Tanzania

Bilioni 63.2 za Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), zasainiwa ili kuwezesha Taasisi za Fedha Tanzania

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
EADB YATOA BILIONI 63.2 KUZIWEZESHA TAASISI ZA FEDHA TANZANIA

Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) imesaini hati ya makubaliano ya utoaji wa mtaji wa jumla ya shilingi bilioni 63.2 kwa ajili ya kuziwezesha taasisi tatu za kifedha nchini Tanzania katika shughuli za utoaji mikopo kwa sekta za kimkakati zinazochochea maendeleo ya haraka ya kiuchumi.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi Mtendaji wa EADB, Bernard Mono, amesema fedha hizo zitaelekezwa katika sekta za nishati, uzalishaji viwandani, miundombinu na madini, ambazo zina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

CUE IN: Bernard Mono...

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa fedha, Kamishna wa Uendelezaji Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya EADB, Charles Mwamaja, amesema lengo kuu la uwezeshaji huo ni kuleta mabadiliko ya haraka ya kiuchumi, kuongeza ujumuishaji wa kifedha na kuweka mazingira wezeshi kwa Watanzania wengi kunufaika na huduma za kifedha.
CUE IN: Charles Mwamaja...

Taasisi zilizonufaika na mpango huo ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya TIB ambayo imewezeshwa kwa mtaji wa shilingi bilioni 30, Azania Bank iliyopewa shilingi bilioni 13.3, na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba (TMRC) ambayo imepata shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kutoa mikopo ya nyumba.

Baadhi ya wanufaika wa makubaliano hayo wamesema hatua hiyo ni chachu ya kuongeza kasi ya upatikanaji wa mitaji, kupanua huduma za kifedha na kuendeleza ajira kwa Watanzania, hususan vijana, kupitia shughuli za kiuchumi zinazofadhiliwa na mikopo hiyo.
VOXY: Wanufaika wakieleza maoni yao...

Uwekezaji huu wa EADB unatajwa kuwa sehemu ya mkakati mpana wa benki hiyo kusaidia ukuaji wa uchumi wa kikanda kwa kuimarisha mifumo ya kifedha ya ndani, pamoja na kuchochea maendeleo endelevu katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
IMG-20250623-WA0028.jpg
IMG-20250623-WA0057.jpg
IMG-20250623-WA0041.jpg
IMG-20250623-WA0051.jpg
IMG-20250623-WA0048.jpg
IMG-20250623-WA0032.jpg
IMG-20250623-WA0044.jpg
IMG-20250623-WA0055.jpg
IMG-20250623-WA0063.jpg
IMG-20250623-WA0043.jpg
IMG-20250623-WA0045.jpg
IMG-20250623-WA0047.jpg
IMG-20250623-WA0056.jpg
IMG-20250623-WA0060.jpg
IMG-20250623-WA0029.jpg
IMG-20250623-WA0061.jpg
IMG-20250623-WA0030.jpg
IMG-20250623-WA0034.jpg
IMG-20250623-WA0036(1).jpg
IMG-20250623-WA0039.jpg
IMG-20250623-WA0036.jpg
 
Back
Top Bottom