Bill Cosby afungwa jela miaka 3 hadi miaka 10 kwa unyanyasaji wa kingono

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mahakama ya Pennsylvania nchini Marekani imemshushia mvua ya kifungo cha kati ya miaka mitatu hadi kumi, mchekeshaji Bill Cosby mwenye umri wa mika 81, baada ya kumkuta na hatia ya kufanya unyanyasaji wa kingono na ubakaji dhidi ya msichana, miaka 14 iliyopita.

Jaji wa mahakama hiyo amesema Cosby amekutwa na hatia katika makosa matatu aliyoyafanya mwaka 2004, akimnyanyasa kingono na kumbaka msichana aliyetajwa kwa jina la Andrea Constand.

Mahakama pia imeamuru Cosby kusajiliwa kwenye orodha ya wanyanyasaji wa kingono na kwamba anapaswa kuhudhuria programu maalum ya kisaikolojia kwa kipindi cha maisha yake yote.

Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa mahakamani hapo, Cosby alimualika msichana huyo nyumbani kwake, kisha akamuwekea vidonge vya dawa za kulevya kwenye kinywaji chake kabla ya kuanza kumuingilia kwanza kwa kutumia vidole vyake.

Msichana Andrea Constand, alieleza kuwa kitendo hicho kilimtoa usichana wake, kumsababishia maumivu makali pamoja na matatizo makubwa ya kisaikolojia.


 
Huyu mtu si alikua na uwezo wa kupata wanawake anaowataka kwa ushawishi wa fedha na kipaji chake sasa ikawaje tena?.
 
Mzee alitaka kutoa bikra ya bint bila shurba,mana wakati huo tiari age ilikuwa about 67yrs
Da kamdhalilisha binti wa watu,hata hivo kuna kipindi walijitokeza wanawake kadhaa hata hivo sijui hao kesi zao vp.
 

Bill Cosby Sentenced To 3-10 Years In State Prison
Bill Cosby was sentenced to 3-10 years today.
He was taken to jail to be processed.
Cosby's legal team filed an appeal in the case
 
Si ajabu akatoka huko akiwa "ameolewa"
 
Kuna watu wengi sana hubakwa kwa njia hiyo na mastaa hata hapa nchini yanafanyika ila huona aibu kuyasema.
Wengine huona ni bahati kuliwa na mastaa hata kama ni kwa kubakwa hivyo.
Mfano halisi ni wa ile kesi maarufu ya April 7
 
ule msemo wa ukiwa na ela wanajileta wenyewe, mbona hau apply?
 
Huyu mzee nilikuwa namkubali sana miaka ya 80 na The Cosby show
Lakini nikaja kusikia matendo yake mabaya sina hamu

Lakini wengi ambao walikuwa karibu na watoto kwa show zao walikumbwa na madhila haya ya kutamani dogo dogo

Na wengi wamekuja kufedheheka uzeeni
Poor sod
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…