billiary obstraction inasababishwa na nini?

billiary obstraction inasababishwa na nini?

hugo jr

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
498
Reaction score
1,645
habari wapendwa
nina tatizo la ugonjwa wa manjano, kwenye ngozi na macho. last time niliambiwa nile sana miwa nitapona lakini wapi
kwa sababu nilikua sina maumiv nilichelewa kwenda hospital
j3 nilienda hospital nikafanyiwa ultra sound j4 wakafanya ct scan
majibu dokta kasema ni billiary obstraction na kanipa barua niwahi muhimbili haraka sana
nikamuuliza ndo ugonjwa gani yeye akajibu wahi muhimbili, kwa anae jua jaman ni kitu gani hii maana nimepagawa mno
nipo najiandaa niende huko kesho
 
Kuna mfumo unaitwa biliary system unaowezesha nyongo (bile) inayotengenezwa mwilini kwenda kuondolewa kwa njia ya choo na mkojo, sasa inapotokea mirija ya huu mfumo umeziba ndio hiyo wanaita biliary obstruction sasa hiyo husababisha nyongo kuchanganyikana na damu na kukuletea manjano.

Visababishi vinaweza kuwa vivimbe kwenye mfumo(tumors) ,mawe (gall stones) kuziba njia na nyingine ni sababu za kuzaliwa nazo

Ndo hivo kwa ufupi
 
asante sana mkuu
nimepata picha kidogo
 
Back
Top Bottom