BIMA (INSURANCE): Uliza chochote kuhusu biashara ya Bima

1. Si kweli mkuu, Bima haiko mjini pekee bali hata vijijini ipo. Isipokuwa huko vijijini huwa kuna mawakala wa bima (Insurance Agents), wengi huwa wanafungua uwakala maeneo ya centers. Au wengine huwa wanafanya mobile insurance. Mfano: Siku ya mnada wanaweza kwenda na kuwakatia bima watu ambao wanafika pale mnadani na vyombo vyao vya
moto.

2. Kigezo kikubwa unatakiwa kuwa na Cheti cha awali (Certificate of Proficiency in Insurance - COP) na uwe na walau elimu ya kidato cha nne. Iwapo wewe binafsi huna vigezi hivyo unaweza kumuajiri mtu akawa Principal wako,yaani mwenye vigezi hivyo. Vitu vingine ni kama pesa ya Usajili, Leseni ya biashara, TIN number n.k.

Karibu
 
asante [HASHTAG]#newinsurer[/HASHTAG] kwa majibu hapo juu, usichoke kwa maswali mengine, unafikiri aina za bima zilizopo zimecover risks zote za wanadamu, kama jibu ni hapana, risk gani unafikiri unaweza ifanyia insurance? Lakini pia inawezekana uwakala wa bima ukafa kama huyo principal amehama au kuacha kazi kama huna principal mwingine?
 
Samahani mkuu nifafanulie hapo kwenye cheti cha awali na pesa ya usajili shingapi ?
 
Sio risk zote zinakuwa covered na Insurance, mf. Insuance kwa ajili ya matetemeko, mafuriko n.k. Unaweza ku cover risk zote kulingana na uwezo wako.

Kampuni ikifirisika uwakala unaisha, hapo unaruhusiwa kuhamia kwenye kampuni nyingine.
 
Samahani mkuu nifafanulie hapo kwenye cheti cha awali na pesa ya usajili shingapi ?

Cheti cha awali ni Cheti ambacho mtu anapatiwa baada ya kupata mafunzo kuhusu Bima. Utatakiwa kusoma kwa muda wa miezi takribani miwili ili kupata hicho cheti cha awali...

Pesa ya usajili ni takribani milioni 2 hivi...
 
Asante kwa ufafanuzi wako Mkuu, ila kuna chuo maalum ambapo unakwenda kupata hayo mafunzo ?
 
Bima za kawaida zenye ulazima kwenye magari (hizi ni zile bima ndogo na ikiwa huna unakamatwa na traffic) je zinamsaidia nini mmliki wa gari au zinasimama linapotokea tatizo gani?
 
Bima za kawaida zenye ulazima kwenye magari (hizi ni zile bima ndogo na ikiwa huna unakamatwa na traffic) je zinamsaidia nini mmliki wa gari au zinasimama linapotokea tatizo gani?

Bima hizo huitwa Third Party Insurance cover, third party ni mtu wa tatu. Mtu wa kwanza ni Kampuni ya bima, mtu wa pili ni wewe mteja wa bima na mtu wa tatu ni yule utakayemfanyia uharibifu wa mali yake.

Hivyo basi tatizo au ajali ikitokea Kampuni ya bima itamlipa mtu wa tatu yaani Third Party kupitia ile bima ndogo.

Inaweza kuwa ni mali imefanyiwa uharibifu au mtu ndiye amejeruhiwa.
 
Cheti cha awali ni Cheti ambacho mtu anapatiwa baada ya kupata mafunzo kuhusu Bima. Utatakiwa kusoma kwa muda wa miezi takribani miwili ili kupata hicho cheti cha awali...

Pesa ya usajili ni takribani milioni 2 hivi...

Mkuu sorry tunaomba breakdown ya hiyo 2m kama hutojali!
 
Sio risk zote zinakuwa covered na Insurance, mf. Insuance kwa ajili ya matetemeko, mafuriko n.k. Unaweza ku cover risk zote kulingana na uwezo wako.

Kampuni ikifirisika uwakala unaisha, hapo unaruhusiwa kuhamia kwenye kampuni nyingine.
Kama nilikata bima kwenye kampuni yenu alafu ikafilisika madai yangu napataje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…