MIKAEL MTANZANIA
New Member
- May 28, 2024
- 3
- 2
Kuna magonjwa mengi sugu ambayo kwa kweli yamekuwa tishio lakini binafsi nimeona ni vyema kugusia kwanza upande wa figo, hasa upatikanaji wa matibabu yake na huduma zake. Iko wazi kuwa mpaka sasa hapa Tanzania, asilimia takribani 7% ya watanzania wanasumbuliwa na tatizo la figo na wengi wao wamefikia hatua ya mwisho, yaani figo hazifanyi kazi tena.
Hivyo, watu hawa wanahitaji huduma ya kusafishwa damu kupitia mashine(Dialysis), kitendo hiki kwa mgonjwa lazima kifanyike mara mbili mpaka mara tatu kwa wiki. Gharama zake za usafishaji damu ni kubwa sana(300,000/=Tsh) laki tatu mpaka laki (180,000/= ) laki moja na themanini ndani ya wiki moja. Huduma hii mtu anatakiwa aipate mara tatu. Ukiangalia kipato cha mtanzania mwenzangu wakati mwingine kuiapata hata hiyo laki moja kwa wiki bado ni ngumu mno. Na asipopata huduma hiyo kifo kinaanza kubisha hodi mlangoni kwake.
Ukitazama ugonjwa wa figo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na shinikizo la damu lakini pia life style ya mtu, na bahati mbaya zaidi asilimia kubwa tena ya watu wenye shida ya figo wanafika hospitali tatizo likiwa limekomaa, hivyo hakuna tiba mbadala zaidi ya kusafisha damu au kupandikizwa figo,
Sote mimi na wadau wengine tutakubaliana kuwa Figo haitibiki ikishafikia hatua ya mwisho hivyo kuna option mbili tu, kusafisha damu au kupandikizwa figo nyingine.
Gharama za upandikizaji wa figo bado zipo juu zaidi, upandikizaji wake unagharimu milioni thelathini 30 kwa mtu mmoja mpka milioni 25 za kitanzania. Kiukweli kwa maisha ya watanzania waliowengi bado ni ngumu sana kuzimudu hizo ghrama, na mpaka sasa ni kwa mujibu wa takwimu ni takribani watu 120 tu ndio wamepandikiza figo kwa hapa Tanzania.
Ni kweli kwamba hapa nyumbani tanzania tunazo hospital mbili ambazo zinapandikiza figo, hospitali ya taifa Muhimbili na hospital ya rufaa ya Benjamini Mkapa, hii imesaidia kidogo watu kupunguza gharama za kusafiri kwenda nje kupandikiza figo.
Hata hivyo, hospitali hizi si kitu kama gharama zake ni kubwa kiasi hicho na kwa namna nyingine zinawiana na hospital za nje ya Tanzania. Hospitali tunazo na kama tunaweza basi hata gharama ziwe rafiki kwa maisha ya mtanzania.
Mpaka sasa Tanzania tupo kwenye nafasi ya 54 kwa nchi zinazoongoza kuwa na vifo vingi vya wagonjwa wa figo, hiyo idadi inachangiwa kwa kiasi kikubwa na gharama za matibabu pamoja na usafishaji wa figo kuwa juu kwani ni wachache wenye uwezo wa kuzimudu hizo gharama.
Je nini kifanyike?
1. Lazima kwanza kama taifa lijue ikiwa asilimia 7% ya watanzania wanaishi na tatizo la figo na wanahitaji kunufaika na huduma, basi serikali haina budi kupunguza ghrama za matibabu na usafishaji wa damu(Dialysis) kwani kiwango cha hiyo fedha ni kikubwa sana na hii hupelekea watu wengine kushindwa kuzimudu gharama za usafishaji wa kila wiki na kuamua kukaa nyumbani kusubiri rehema za mwenyezi Mungu.
2.Na kama haitoshi, ni vyema kuwatafutia watanzania BIMA ya kudumu, ambayo itawasaidia kwenye matibabu, kwa sababu usafishaji wa damu yaani (dialysis) kwa wagonjwa wengi wa figo ni kitu endelevu kwenye maisha yao.
Ningefurahi kuona bima zetu zinaboreshwa na kuwa na uwezo wa mgonjwa wa shida yoyote kupata uwezo wa kuitumia bima yake hata anapohitajika kwenda nje ya nchi kufanya matibabu zaidi. Swali la kujiuliza ikiwa kila wiki inakulazimu utoe zaidi ya laki sita kwenda kusafisha damu wewe unaingiza shingapi na bila bima ya kudumu utaishi? (BIMA BABA / BIMA MAMA}
3. Ni vyema pia kuongeza vifaa tiba, kitendo cha kusafisha damu kinagharimu masaa takribani manne kwa mgonjwa mmoja, na ukiangalia ni wagonjwa wengi wanahitaji huduma hiyo. Mpaka hospatili kubwa kama Mhimbili imelazamika kufanya hiyo huduma mchana na usiku na idadi ya wagonjwa wa figo inazidi kuongezeka kila mapambazuko.
4. Serikali lazima ifanye mpango kufikisha mashine hizo za usafishaji na hata kwenye baadhi ya hopistali za wilaya sio za mikoa tu, hii itasaidia kwani wanaoumwa sio watu wa Dar es salaam wala watu wa Mwanza tu, kuna watu wapo ndani vijijini huko NYAMAGANZA na wenyewe wanahitaji kufikiwa.
5. Vilevile kunayo shida ya Madaktari bingwa wa figo, hivyo ni mapendekezo yangu kuona serikali ikiongeza nguvu ya kuwasomesha madaktari kwani kuna uwezekano wa asilimia kubwa mno huko mbele ya vijana wengi kuja kuwa wagonjwa wa figo kutokana na lifestyle yao. (ukweli mchungu lakini tujiandae kuwapokea)
6. Tasisi binafsi zinazodili na maswala ya afya zitazame pia upande wa ugonjwa huu, sio kila taasis inayoibuka inafocus na watu wa HIV (UKIMWI} tu, ni vyema pia taasisi zijue kuna watu wanahitaji msaada pia kwani inawalazimu kila wiki kusafisha damu.
Mapendekezo yangu;
Ikiwa haya magonjwa makubwa na gharama za vipimo vyake ni kubwa na kupelekea watu wengi kutokupima afya zao mara kwa mara mpaka tatizo liwe kubwa, ni vyema wizara ya afya ikaongeza kipengele cha punguzo la gharama za vipimo, sisi watanzania sio waoga kucheki afya zetu mara kwa mara ila pia hatuna kipato cha kupima mara kwa mara. (BIMA BABA / BIMA MAMA}
Hivyo basi, itakuwa ni vizuri kama kutakuwa na programu ambayo mtu akienda hospitali wakati wa kuonana na daktari apewe punguzo la upimaji wa mwili mzima halafu yeye ndio atachagua, lengo ni kufanya wepesi wa kugundua watu wenye shida kubwa (magonjwa makubwa) ambazo zinachukua muda mrefu mpaka kuonekana mwilini na kuanza matibabu mapema kabla ya ugonjwa kuota mizizi. Kama tatizo litagundulika mapema na matibabu yake yakafanyika mapema, hii inakuwa tofauti na pale tatizo linapogundulika likiwa tayali limekomaa.
Tunaweza kupunguza ongezeko la wagonjwa wa figo kama juhudi za mtu mmoja mmoja zitaonekana kwani ugonjwa huu sio wa wazee tu, huu unatafuna watu wa rika zote, wazee vijana na watoto.
Tunaweza kuudhibiti ugonjwa huu kwa kubadili mfumo wa maisha (lifestyle) lakini pia kucheki afya mara kwa mara, kuzingatia vinywaji na vyakula vyetu, kufanya mazoezi, kunywa maji ya kutosha n.k. Lengo ni kupunguza idadi ya wagonjwa wa figo kwani ugonjwa huu unatesa na unagharama kubwa mno kujiuguza.
Mtibeli wa kisukuma.

Upvote
2