Bima ya afya kwa wote iwe sawa na mshahara kima cha chini kwa watumishi na wasio watumishi

Bima ya afya kwa wote iwe sawa na mshahara kima cha chini kwa watumishi na wasio watumishi

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,783
Reaction score
2,396
Habarini,

Ni wazi watumishi ndiyo wananufaika kwa bima ya afya hasa ukizingatia wao huchangia kwa kukatwa kwa 3% na kuchangiwa 3% na mwajiri.

Sasa kwanini serikali isianzishe utaratibu wa wananchi wote wa kawaida wasiyo na uwezo kuchangia kwa 6% ya hicho kima cha chini pendekezwa na wenye uwezo kuwekewa utaratibu wa kuchangia hata 10% kulingana na kipato chao?

Hivyo 500,000x3%=50,000/=x12=600,000/= kwa mwaka ili wananchi wote wapate matibabu sawa?

Mtumishi mwenye mshahara kima cha chini 500,000/= akatwe 3% ambayo ni 15,000/= kwa kwezi na kwa mwaka 150,000/= halafu mtu wa kawaida achangie zaidi ya 1mln kwa mwaka kweli ni sawa?
 
Back
Top Bottom