kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Uchumi, mila, dini, desturi na huduma zetu za afya haviruhusu kutoa Bima ya afya kwa wote. Matibabu ni hitaji la nne la binadamu nyuma ya hewa, maji na chakula (Maslow's). Jiulize je, jamii yote inapata hewa, maji na chakula? Kama jibu ni bado basi bima ya afya kwa wote ni kitendawili.
Uchumi wetu: Wananchi hawana pesa ya kulipia ugonjwa ambao haujatokea wakati Kuna shida Leo inayoshindikana kutatuliwa kwa ukosefu wa pesa.
Dini na Mila: mtu mmoja ana wake na watoto wengi sana kuliko idadi inayotakiwa na bima. Mke yupi atibiwe na nani aachwe? Watoto wepi wasitibiwe?
Huduma za afya: Watu wakiwa na bima wanahamasika wengi kwenda kutibiwa hata kwa ugonjwa kidogo sana ili hela yake isipotee bure. Je, tunao watumishi wa afya wa kutosha kuhudumia ongezeko hilo? Vifaa je? Wodi je? Dawa je?
Tabia za maskini: maskini wanaugua sana kutokana na uwezo mdogo wa kufuata kanuni za afya. Kila siku watakwenda hospital.
Hata mataifa makubwa yameshindwa kutoa Bima ya afya kwa wote sembuse sisi?
Huduma zitakuwa hovyohovyo kabisa.