Mimi ni mstaafu mwandamizi niliyepo wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera.
Nilipata tetesi za kuwapo kwa uhakiki wa wastaafu walio kwenye mfuko wa bima ya Afya tangu mwezi Machi mwaka huu. Kila aliyeniambia nilipomuuliza alikozipata taarifa, naye aliniambia ameambiwa na mwingine.
Hakukuwapo uthibitisho wa chanzo.
Nilihisi kuwa ni jumbe za kitapeli ambazo zinatumwa mara kwa mara. Jana, jamaa yangu akanitumia na kuniuliza iwapo nimepata ujumbe huu:
"NHIF 17.03.2023 SAA 03:11PM NDG. MWANACHAMA MSTAAFU,TAFADHALI FIKA NA MWENZAWAKO KTK. OFISI YA MFUKO ILIYO KARIBU KWA AJILI YA ZOEZI LA UHAKIKI KABLA YA 30.04.2023. AIDHA, FIKA NA NA. YAKO YA NIDA NA NA. MWENZA WAKO. KWA UFAFANUZI _ PIGANA. 199 BILA MALIPO. SENDER HENRY".
Naye alitumiwa na mstaafu mwenzetu. Sikuamini kuwa huo ni ujumbe halali. Mtindo/namna ya uandishi haikuniongoza kuamini kuwa umetumwa na taasisi hii kubwa. Kuna makosa mengi ya kiuandishi na hata ya kimantiki. Hilo tuliache.
Niliingia kwenye tovuti yao. Sikuona tangazo hilo. Niliwasiliana nao kupitia simu hiyo 199. Nilipata ushirikiano mkubwa kwa aliyenipokea. Niliambiwa yafuatayo:
1. Ni kweli uhakiki upo. Unahusisha wastaafu na walioko kazini. Wanataka mstaafu aende na mweza wake.
2. Kila mhusika alishaarifiwa kupitia simu yake na kila mmoja ana tarehe yake. Mimi na wastaafu sita niliowauliza hatuna ujumbe huu.
3. Uhakiki unafanyika makao makuu ya mkoa.
4. Mwisho wa uhakiki ni Mei 30.
Inaelekea bima ya afya hawafahamu kuwa Wastaafu (wateja wao):
i) Ni wazee
ii) Wengi ni wagonjwa
iii) Wengi wana pato duni mno ambalo huenda halitoshi hata gharama ya kwenda mkoani.
iv) Baadhi ni walemavu
v) Kuna ambao hawawezi kusoma jumbe hizo
Yaani wao kwenye simu zao wanafahamu kubonyeza kitufe kimoja tu. Cha kupokelea simu.
Hawa hawawezi kuweka vocha, kukata simu baada ya maongezi, kuongeza salio, kuunga kifurushi nk.
Sembuse kusoma au kuandika ujumbe!
Ushauri:
1. Uhakiki ufanywe jirani na wahusika. Ikiwezekana kwenye Kata. Kuwalazimisha kwenda mkoani kuachwe. Haya ni mateso. Mateso makubwa mno.
Mstaafu aliyepo kijiji cha Muganza wilayani Ngara, mkoa wa Kagera, uhakiki huu utamgharimu siku 5 (kwenda Bukoba na Kurudi). Baadhi ya wastaafu wanahitaji kusindikizwa/kupata wasaidizi. Mbali ya adha za safari, fikiria muda na gharama za safari. Mkifika kwenye kata zao ni vema zaidi.
2. Zoezi hili lifanyike kwa uwazi na kwa haki. Tangazeni kwenye vyombo vya habari. Wekeni kwenye tovuti yenu.
Wasilianeni vema na wateja/wadau wenu. Uduni wa taarifa hizi na hata uandishi wa sms ya wito tunautofautishaje na sms nyingine za kitapeli tunazotumiwa mara kwa mara.
3. Fungueni ofisi wilayani au muweke dawati lenu ama kwa Mkuu wa wilaya au Halmashauri. Mnataka wazee hawa wafe kwa ajali barabarani kwa safari? Mara uhakiki wa PSSSF mkoani na sasa uhakiki huu nao mkoani.
Magonjwa mengine yanatokana adha hizi.
Wazee mnaowasumbua na kuwatesa leo walitumikia nchi hii kwa bidii na uaminifu mkubwa. Msiwalipe mateso kwa kuwajaza majuto na kihoro.
KWA HALI HII, UZEE SI DHAHABU BALI NI ADHABU.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.