Bima ya Afya nchini Kenya kugharamia matibabu ya mke au mume mmoja tu kwa walio kwenye ndoa zilizo na zaidi ya mpenzi mmoja

Bima ya Afya nchini Kenya kugharamia matibabu ya mke au mume mmoja tu kwa walio kwenye ndoa zilizo na zaidi ya mpenzi mmoja

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Bima ya Afya nchini, NHIF, sasa itakuwa inagharamia matibabu ya mke au mume mmoja tu kwa walio kwenye ndoa zilizo na zaidi ya mpenzi mmoja.

Vile vile, bima hiyo pia itakuwa sasa inagharamia watoto watano tu baada ya mageuzi ambayo yalianza Januari 1, 2020.

Bima ya afya humu nchini NHIF imefanya mageuzi na sasa itakuwa inasimamia mwanandoa mmoja pamoja na watoto watano pekee. Picha: BusinessDaily

"Kwa bima ya kawaida, nambari ya mwanandoa iwe mmoja na watoto watano pekee," barua iliyotumiwa mameneja wa matawi ya bima hiyo ilisema.

Aidha mageuzi mengine ni kuwa wanachama wanaojilipia kibinafsi sasa watakuwa wanasubiri siku 90 ili kufaidika na bima hiyo baada ya kujisajili.

Na ni lazima wanachama hao wahakikishe kuwa wamelipia bima ya mwaka mzima ndani ya siku hizo 90 wanazosubiri ili kuanza kufaidika.

Watakaochelewa kulipa ada ya kila mwezi watapigwa faini ya asilimia 50.

Aidha, watakaochelewa kulipa ada ya kila mwezi watapigwa faini ya asilimia 50 na walazimike kulipia mwaka mzima sawa na kusubiri siku 30 ili kufaidika na malipo ya bima hiyo.

Iwapo yeyote atachelewa kulipia ada kwa zaidi ya mwaka mmoja, basi atalazimika kujisajili upya kwenye bima hiyo kama adhabu.

Aidha ni lazima mama awe amemaliza miezi sita tangu kujisajili kwenye bima hiyo ili aweze kulipiwa bili ya kujifungua.

Kina mama watalazimika kuwa wamemaliza miezi sita tangu kujisajili na NHIF ili kulipiwa bili ya kujifungua.

Wote watakaojumuishwa kufaidika na bima hiyo baada ya usajili wa kadi watalazimika kusubiri hadi miezi sita ili kulipiwa bili.

Hata hivyo, watoto waliozaliwa watakubaliwa mradi tu wajumuishwe ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya kuzaliwa.


Source: Tuko
 
KWA HIYO MILA ZA KIAFRIKA ZINAULIWA NA WAAFRIKA WENYEWE!!! AMA KWELI AKILI NI MALI. MABABU NA MABABU BARANI HAPA WAMEISHI NA MILA ZA ZAID YA MKE MMOJA . LEO ZINATUNGWA SHERIA KUFUATA MILA ZA KIZUNGU!
 
Back
Top Bottom