Bima ya afya NHIF fomu za kujiunga zilirahisishwa mpaka kwenye zahanati

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
3,118
Reaction score
4,238
Nimeleta nyuzi zaidi ya moja humu kuhusu hawa watu wa bima na sidhani kama nitawazungumza vizuri bila ya wao kujirekebisha. Namuomba mola awajaalie baya lolote tu kama zawadi yao kwa huu uhuni na usumbufu wanaonifanyia

Tunawasemaga polisi bure tu mazee, sekta sumbufu ni afya! Nataja kwa ufupi mlolongo wa matukio yanayosababisha nawalaani NHIF

Kwanza watumishi tulijaza fomu zao tukajiunga kisha baadae ndipo yakaja maswala ya nida. Ikawa ukitaka kuongeza mtu utachagua kiambata kati ya nida, voters id, nk. Watu wakawa wanapata usumbufu lakini ikawa simu ikipigwa ukajieleza vizuri jambo linaisha kadi inatengenezwa. Nida ilipochanganyia usumbufu ukaja rasmi, kwanza vitu vyote vikatupwa huko ikawa bila nida mtu hatengenezewi kadi. Hii tukauma meno tuendane nayo.

Sasa mambo yakazidi kuwa magumu
Baada ya kuoa mke nimesumbuliwa sana kutengenezewa kadi yake mwishowe wakatengeneza. Mtiti ukavaa sura nyingine kabisa ilipofika kwa wakwe. Nimepeleka ombi la kumuongeza mzee (mkwe) wakakataa eti anayeonekana kwenye NIDA siyo yule wa kwenye cheti cha kuzaliwa mke. Nilikaa muda nikatuma tena ombi nikapigiwa tena simu kwa mara nyingine na ombi likacanceliwa vilevile

Iliniuma sana hiyo maana mzee yule alikuwa na kliniki ngumu kweli kweli ikawapunyua watu hela mpaka basi. Hoja yenyewe iliyomnyima mzee wa watu haki yake sasa... ngoja nikuwekee hapa ujionee. Mtu mfano anaitwa MUSSA JAMES ISSA NDEGE; mtoto wake kwenye cheti cha kuzaliwa sehemu ya jina la baba akaandika MUSSA JAMES ISSA na mzee mwenyewe kwenye NIDA akaandika MUSSA JAMES NDEGE tayari mtoto anaambiwa huyu mwenye nida siyo baba yako!

Moja ya dependants akapoteza kadi naenda hospitalini wanipe fomu nijaze apate kadi naambiwa hakuna huduma hiyo kwa sasa kila kitu kwenye mfumo niingie huko nimalize haja zote. Naingia huko napo nakutana na ujinga, kwanza namba ya simu uliyojisajilia NHIF hata kama ni 10 yrs ago unatakiwa uingize hiyohiyo na ndipo upate OTP.

Hapo ndo akili kumkichwa namba unayo au huna. Wanasema wanatuma kwenye email na simu lakini kwenye email hutakaa uione OTP na hata kwenye simu kwenyewe sms inachelewa na usitoke kwenye mfumo!

Ukishapokea otp ukaingia kwenye mfumo kuna mfumo kujiridhisha kama ni wewe. Ni jambo jema sana hili lakini isivyo bahati ni kwamba hii ni sehemu ambayo wenzangu wote wamekwamia hapo. Kuna maswali ya NIDA unaulizwa ebana hutakiwi kukosea hata nukta. Unaulizwa taja jina la baba mfano kule iliyopo ni Mohamedi ukaandika Mohamed tayari umekosa na utaendelea kuletewa swali lingine.

Mbaya zaidi ni wale wenye baadhi ya vitu vinapishana (vinatofautiana) Notification inakuja kabisa inasema taarifa za NIDA ni tofauti na taarifa zilizowasilishwa na mwajiri kwenye ofisi ya NHIF kisha yale maswali yao unawekewa pata vizuri lakini inakuwa huendelei mbele bali utaishia kujibu maswali yanayojirudia rudia mpaka utakapo amua mwenyewe kuacha

Mimi nilifanikiwa kuvuka hapo lakini humo ndani hakuna sehemu ya kutuma maombi ya kadi nikipiga simu huduma kwa wateja mkoani hakuna msaada. Mara ngoja nitakupigia mara unapewa maelezo yasiyo na mgongo wala tumbo. Aliyekuja kunichosha ni huduma kwa wateja ya 199 kuniambia nibebe loss report ya polisi niende mkoani nikajazishwe fomu ya kutengenezea kadi nyingine! Angejua tu...

Abarikiwe yule daktari alimwambia mke ataje namba ya NIDA akamhudumia kwa namba ya NIDA mbadala wa kadi ya NHIF. Imagine umkute dokta kisirani aliyekariri kadi kadi kadi! Au uende kwenye kizahanati ambapo wanatumia kuandika tu hakuna mfumo (kompyuta)

Jamiiforums wafikishieni ujumbe huu serikali watu tunapata tabu mno. Mwanzo fomu za kujiunga zilirahisishwa mpaka kwenye zahanati zikawekwa kwajili ya kujiunga sasa wameshapata wateja wanakata hela zetu hawatujali tena. Ukiwa na shida ya huduma fulani unaambiwa ufike ofisini mkoani. Mbona mwanzo kujaza fomu hamkusema niende mkoani
 
...Mimi Kitambulisho cha wife kilichakaa, nikawapelekea NHIF kule Town, nikaambiwa lete Nida yake, nilivyopeleka nikaambiwa kile kitambulisho cha NHIF kimefika atatumia cha NIDA, juzi akaumwa anaenda Hosp akaambiwa Hakionekani kwa System hivyo alipie, akalipia...badae nikamchek mtu wa NHIF akiangalie kwa System akanambia kipo mbona....
 
Pole ndugu.
 
Mods siyo lazima kuhariri baadhi ya heading,
Ona sasa mmepoteza mwelekeo wa uzi mimi nimetaja mauozo na mausumbufu kibao ninayopitishwa na wahusika wa NHIF nyinyi mmekwenda kuweka heading inagusa kitu kimoja tu

Hatahivyo siyo kesi, kikubwa ujumbe ufike na narudia tena kusema na kumuomba mola;

WALAANIWE WATU WOTE WA NHIF WALIOHUSIKA KUNISUMBUA. AIDHA WAHUSIKA WAKUU WA NHIF NAO KAMA HAWATAKI KUREKEBISHA HIZI CHANGAMOTO NINAZOLALAMIKIA HUMU KILA MUDA BASI NAO BAYA LOLOTE LIWAKUTE, POTELEA MBALI
 
Ikoje hiyo? Maana mimi nilikataaga kwanza kabisa nisijiunge na mfuko wa bima kipindi ndio nimeajiriwa lakini ushawishi tena si unajua
Ni bima ya afya mkuu Ina vifurushi aina 5 Kuna
jubilee afya
Pamoja afya
J-care premium
J-care senior
J-care junior

Wacheki pia
 
Back
Top Bottom