DidYouKnow
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,229
- 1,950
Watanzania wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu madhumuni ya mifuko ya Bima ya Afya na jinsi inavyotenda kazi. Kukosa elimu hii huongeza malalamiko kuhusu uchangiaji na kujiunga na mifuko husika.
Mimi kama mtanzania niliyebahatika kupata elimu ndogo nimewiwa kutengeneza thread hii kwa nia ya kutoa elimu isiyo ya kitaalamu kuhusu mifuko ya bima ya afya, hasa tukitumia mfano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (Ningependa kuuita MFUKOTIBA nikimaanisha MFUKO wa Taifa wa Bima Afya). Nikiri kuwa mimi si mtumishi wa mfuko wowote wa Bima ya Afya, ila ninatambua mafanikio makubwa yaliyoletwa na mifuko hii.
Hebu tuanze na mfano mdogo.
Miongoni mwetu kuna watanzania wengi ambao ni tegemeo kubwa kwa familia na hata koo zao. Mtu huyu tegemeo, labda tumfananishe na Mtemi. Mtemi ni kiongozi au mtawala anayesimamia jamii fulani katika uzalishaji na usambazaji wa rasilimali na pia ana majukumu ya kutatua shida na migogoro mbalimbali katika himaya yake.
Mtemi anategemewa kuunganisha watu katika eneo la mashauri, uchumi na mambo mengine ya kijamii. Mtu huyu kila kuwapo na shida familia humfuata ili ahusike kulitatua.
Hebu fikiria. Yamkini kila baada ya siku kadhaa Mtemi anapewa taarifa ya mmoja wa wanafamilia wake kukumbwa na magonjwa mbalimbali, hivyo anapaswa apelekwe hospitali. Inawezekana hata yeye binafsi ameshatumia gharama zake nyingi kutibu wanafamilia wagonjwa huko nyuma na au alishaomba michango mingi toka kwa baadhi ya wanafamilia wenye uwezo kiasi ili kusaidia matibabu ya watu wake, lakini sasa hawawezi kutoa msaada zaidi.
Kwa hekima, mtemi anaamua kulipa gharama au kuchangisha pesa za matibabu kwa mara ya mwisho, lakini anaazimia kuitisha mkutano wa watawala wake au wananchi wote anaowaongoza ili kukabili tatizo hili la matibabu. Mtemi anawaambia wanajumuiya kwa sababu kumekuwa na changamoto ya gharama za matibabu, basi watengeneze mfuko wa matibabu katika utawala wao.
Fedha za mfuko huu zitatumika kulipia gharama za matibabu kwa mchangiaji yeyote pamoja na wategemezi wake. Kama mtu hatokuwa mchangiaji basi hatonufaika na michango ya mfuko husika. Mfuko huo utaanzishwa kwa michango ya wanafamilia na utaendeshwa kwa fedha hizohizo. Hakuna pesa yeyote ya nje itaingizwa kama mtaji.
Wanahimaya wanakubaliana na wazo na wanaazimia kuanzisha mfuko. Wanakubaliana namna ya kuchangia. Wale walioajiriwa, watakatwa asilimia 3 ya mshahara wao.
Kitu kimoja kikubwa katika mfuko huu ni kuufanya uwe endelevu. Mfuko utakuwa endelevu ikiwa matumizi ya wanachama katika matibabu hayatazidi michango yao. Mwanachama akiugua gharama zote za matibabu zitalipiwa na mfuko.
Mara nyingi wanachama wagonjwa hutumia gharama kubwa za matibabu zaidi ya fedha walizowahi changia katika mfuko. Hii inamaanisha kwamba kama mwanachama ana magonjwa sugu kama ya Kisukari au shinikizo la damu n.k. atakuwa akitumia pesa zaidi ya anayochangia na hivyo pesa zilizochangiwa na watu wengine ambao si wagonjwa ndio zitasaidia kwenye matibabu yake.
Ikitokea wanachama wote wa mfuko wa Bima ya Afya wakawa wagonjwa, wataua mfuko; kwani kama tulivyosema hapo juu matibabu ya mtu mmoja huwa ni gharama zaidi ya kile anachochangia mwanachama mmoja mmoja. Inahitaji michango kadhaa ili kulipia gharama za matibabu ya mwanachama mmoja.
Ni bahati mbaya sana kwamba mifuko mingi inakuwa na hatihati ya kufa kwa sababu watu wanaojiunga na mifuko hii kwa hiari, wengi wana magonjwa mbalimbali na wamejiunga kwa nia moja tu ya kutaka kunufaika kwenye matibabu kwa kutumia pesa za mfuko zilizochangwa na watu wengine. Ili mifuko idumu, inapaswa wanachama wengi wawe na afya.
Mfuko wa Bima ya Afya unaweza ufananisha na mlinzi nyumbani au katika eneo la biashara. Kama umemwajiri mlinzi, furaha yako ni kuona mali zako ziko salama. Tutakushangaa ukifukuza mlinzi, kisa toka umwajiri mlinzi hujawahi ibiwa.
Mwingine anauliza, mimi kila siku ninakatwa pesa kwenye mshahara wangu na siugui; je kuna faida gani nitapata ili kutumia pesa zangu? Nadhani wengine wanataka wapate magonjwa mazito kama kansa ili waone thamani ya uanachama wao. Inanikumbusha mwanachama mmoja wa mfuko wa kufa na kuzikana (sijui kwanini tuna hii mifuko, bora ingebadirishwa kuwa MFUKOTIBA), baada yakutoa michango mwaka mzima kwa watu tofauti bila yeye kufiwa, akaamua kujitoa kwenye mfuko; ati kwanini wanachangiwa wengine tu? Mbona ndugu zake hawafi ili naye apate michango?
Mwingine anauliza, mimi kila siku ninakatwa pesa kwenye mshahara wangu na siugui; je kuna faida gani nitapata ili kutumia pesa zangu? Huwa nawauliza hawa watu wanataka wapate kansa ili waone thamani ya uanachama wao? Inanikumbusha mwanachama mmoja wa mfuko wa kufa na kuzikana (sijui kwanini tuna hii mifuko, bora ingebadirishwa kuwa MFUKOTIBA), baada michango mwaka mzima kwa watu tofauti bila yeye kufiwa, akaamua kujitoa kwenye mfuko; ati kwanini wanachangiwa wengine tu? Mbona ndugu zake hawafi ili naye apate michango?
Wanachama wachache wa mifuko ya Bima ya Afya ambao kila siku wanalalamika kutopata faida kupitia uanachama wao kwa sababu ya kutougua wanakuwa wamekosa elimu ya bima. Wengine wanauliza hadi gawio wasipoumwa. Hayo siyo malengo ya mifuko hii. Kwani ukikata bima ya gari usipopata shida ipasayo kulipwa fidia utaenda kuomba gawio la fedha yako
Tuwashangae pia wale wanaotaka kujiunga na mifuko ya bima ya Afya wakiwa wagonjwa kwani wanafanana na mtu ambaye baada ya kupata ajali ya gari lake, anataka akakate bima ili apate mafao ya ajali. Pia tumshangae mfanyabiashara ambaye baada ya kuibiwa, ndipo anamtafuta mlinzi ili kurudisha mali zake zilizoibiwa.
Unaweza fananisha bima na mlinzi, ingawa si mlinzi haswa, bali ukiwa na Bima ya Afya na kukatokea na magonjwa basi hofu yako isiwe gharama za matibabu, bali kupona kutoka katika magonjwa.
Tusisubiri tuugue, Bima ya Afya ni sasa.
Rafiki yangu huwa anatania kwamba magonjwa fulani huwa yanawaogopa matajiri, lakini mimi nadhani anakosea, magonjwa huwaogopa wenye bima ya Afya maana hupata tabu sana kuwaondoa.