Pre GE2025 BIMA ya Afya,Toto Afya Kete Murua kwa Rais Samia 2025

Pre GE2025 BIMA ya Afya,Toto Afya Kete Murua kwa Rais Samia 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
697
Reaction score
1,358
Afya ni Mtaji kwa Binadamu yoyote madhali Tu huyo Binadamu anapumua

Kwa Nchi zinazoendelea Tanzania ikiwepo BIMA ya Afya kipaumbele kwa Wananchi wote

Kwa Tanzania Wananchi wengi wanaishi kwenye kipato cha chini hiyo pindi Afya inapokuwa mgogoro huna Bima ya Afya inakuwa shida kubwa

Siku za hivi karibuni tumeona baadhi ya watendaji hasa Wizara ya Afya kuwa sio wazalendo na zaidi kutaka kumchonganisha Rais na Wananchi wake

BIMA ya Afya imekuwa gharama na magonjwa au dawa nyingi zimetolewa

Toto Afya vigezo ni vigumu na watoto wengi wemekosa matibabu

Rai yangu kwa MH Rais Samia,Wizara ya Afya ikae na wadau wote kujadili ili Wananchi wote weweze kupata matibabu pasi na kuchelewa

MH Rais Wananchi wakiwa na uhakika na afya zao hasa kupata huduma za matibabu unakuwa umemuondelea adha kubwa Wananchi wako

MH Rais mwakani 2025 kuna Uchaguzi Mkuu hivyo chonde chonde usiingie kwenye mtego huo wa baadhi ya watendaji wenye nio ovu kutaka kukugombanisha na wapiga Kura

Nikuombe MH Rais haraka iwezekanavyo mchakato uanze haraka na Wananchi waweze kupata huduma muhimu kwa ustawi wa Afya zao

Alex Fredrick
+255655308494
 
Back
Top Bottom