Mohamed Abubakar
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 984
- 1,179
Kupitia mfumo wa kiditali bima ya AFYA VIKOBA itawezesha makundi tegemezi kama mwanafunzi, ombaomba nk kumudu gharama za matibabu kwa kuchangia Tshs 150 kwa siku, 1000 kwa wiki na 45,000 kwa mwaka. Na watoto umri wa siku 1 hadi miaka 4 wa mwanakikundi kupata tiba bure na hasa kwa magonjwa yanayofahamika magonjwa dume ambayo kimsingi hakuna wananchi wa kawaida anaweza kumudu matibabu yake. Mfano kansa, moyo, kisukari, mifupa
View: https://x.com/TheChanzo/status/1803824587886539068?t=Zfd784NPI_K42FgjwR7z6A&s=08
Source : The chanzo
1. UTANGULIZI
Wazo hili la kuanzisha bima ya afya VIKOBA lilijitokeza baada ya tukio la kusikitisha lililohusisha mgonjwa aliyelazwa katika moja ya hospitali ya rufaa ya Umma.
Wazo hili la kuanzishwa kwa bima ya afya VIKOBA kama suluhisho la kutatua changamoto za huduma za afya zinazoikumba jamii ya watu masikini nchini Tanzania lilitokana na utafiti binafsi nilioufanya hususan kwa mama mtu mzima mwenye umri niliokadiria wa zaidi ya miaka 70.
Mbali ya mama huyu, katika ufuatiliaji wangu niligundua kuwa wagonjwa wengi hukosa huduma za matibabu za kutosha ingawa hupokelewa na kulazwa hospitalini hapo .
Watu hawa walikosa kupatiwa huduma za vipimo na matibabu kutokana na uwezo wao mdogo wa kifedha.
Wale ambao waliopata sehemu ya matibabu mara nyingi walizuiliwa hospitalini hapo na hawakuweza kutoka wodini hadi madeni yao ya matibabu yatakapo malizika kulipwa ingawa kiuhalisia hawakuwa na uwezo huo wa kulipa.
Mfano mmoja muhimu ni huyo bibi mwenye umri wa zaidi ya miaka 70.
Bibi huyu baada ya kugundulika kuwa ana saratani ya utumbo mpana, alifanyiwa upasuaji wa njia mbadala ya kutoa haja kubwa ili kupunguza maumivu aliyokuwa akiyapata. Hata hivyo hakuweza kuendelea na matibabu zaidi kutokana na deni lake la matibabu na upasuaji wa shilingi za Kitanzania laki 7.
Source: Remix AI
Zaidi ya hayo, nikiwa muumini wa kiislam ninaeingia misikitini tofauti tofauti kila muda wa swala unapofika, niligundua kuna gap kati ya waumini na wagonjwa waliolazwa hospitali hiyo. Kwani upo utaratibu wa kuwaombea /kuwasomea dua maalum kwa ajili ya wagonjwa na hasa aliyolazwa bibi yule. Maombi haya wakati mwengine hutoka kwa wauguzi katika hospitali hiyo kuu.
Hali hiyo iliniletea swali iwapo dua hizo pekee yake zawezaje kumsaidia mgonjwa mfano wa bibi yule bila juhudi ya kupatikana suluhisho la kijamii kwa wagonjwa wanaoletwa mahospitalini bila ya kupata matibabu wala huduma kutokana na uwezo wao mdogo wa kulipa gharama za matibabu.
Hali hii inaonyesha umuhimu wa mpango wa bima ya afya wa kina utakaokuwa na mahitaji yatokananayo na changamoto za jamii masikini, hivyo kuchochea kuundwa kwa Mradi wa Bima ya AFYA VIKOBA utaokuwa chini ya Taasisi na Jumuiya za Imani (msikiti, Kanisa, Temple) na kuratibiwa na taasisi huru itaokuwa na mfumo rasmi (portal) wa bima ya afya kidigitali.
Kupitia Bima ya afya VIKOBA itahusisha taasisi za kiimani (kanisa/misikiti) kama sehemu na wajibu wa imani tofauti zinazohimiza kutoa kwa ajili ya wenye uhitaji. Wakati huo huo mtoaji nae kufaidika.
2. HUDUMA ZILIZOPO KWASASA
Pamoja na kuwa na mifuko tofauti ya Bima inayotumika ukiwemo mfuko wa serikali yaani NHIF hata hivyo imeshindwa kukidhi mahitaji na matarajio ya watanzania. Moja ya sababu kubwa ni la kiitikadi ambapo serikali imeamua kujitenga kuhusisha shughuli zake kuchanganya na dini.
Ambapo kimsingi, dini na viongozi wa dini wanafanya kazi moja na Serikali, nayo ni kuhudumia jamii. Ambapo fursa waliyonayo, kauli zao zinaaminiwa zaidi na waumini kuliko kauli za viongozi wengine. Kwenye Taifa ambalo zaidi ya 85% ni waumini wa dini mbali mbali.
Huku Serikali yenyewe ikikiri kuwa Sera ya afya bure kwa watoto chini ya miaka mitano, wajawazito na wazee kushindwa kutekelezeka.
View: https://twitter.com/TheChanzo/status/1763213693276266962?t=R3-VEKJ6_DYpmDSiq7mcjg&s=19
Source: The chanzo
3. SIFA ZA ANAYESTAHILI KUJIUNGA NA MPANGO HUU WA BIMA AFYA VIKOBA
- UMRI : miaka 5 hadi 100
- UKUBWA WA KIKUNDi : Wanachama 200 waumini wa dini.
- Bima hii ni ya Mwanachama mchangiaji, na watoto wao walio na umri wa siku 1 - hadi miaka 4 na siku 364 hawatohitaji kuwa sehemu ya wachangiaji.
- Mwanachama ataruhusiwa kupata huduma kupitia hospitali ziliyoorodheshwa.
4. MAPENDEKEZO YA MKAKATI
Bima ya Afya VIKOBA inakusudiwa kuwa mpango wa hifadhi wa kijamii ambapo wanachama watakaochangia mfuko huu wataweza kupata huduma za matibabu yote pamoja na huduma za kulazwa. kwa kuanzia tutaanza na hospitali ya taifa Muhimbili pamoja na taasisi za afya za magonjwa maalum kama vituo vya matibabu ya mifupa Moi, hospitali za moyo JAKAYA, taasisi za kansa Ocean Rd.
Wanachama/waumini wanapaswa kujiunga na programu hii kupitia misikiti, makanisa, sinakogi, temple nk, kwa kujiegemeza kwayo. Taasisi hizo watakuwa wadhamini wao na na michango yao itapitia kwa taasisi hizo za dini kwa mwanachama kuchangia katika mfuko kupitia michango ya kila siku au kila wiki (Ijumaa, Jumamosi, Jumapili).
5. NJIA (APPROACH)
Bima ya afya VIKOBA umejielekeza katika taasisi za dini kwa maana makanisa, misikiti nk ambako wazazi na watoto wanakutanisha na kiongozi wanaemsikiliza, wanaemuamini na ambae akitoa maelekezo waumini hufata bila hata ya kuhoji.
Kupitia bima ya afya VIKOBA pesa wanayotoa muumini itawanufaisha wao wenyewe na au kuwanufaisha wenye uhitaji sawa na mafundisho ya kiimani yanavyotufundisha.
Taasisi ya dini ambayo ni kawaida kukutanisha waumini 200 kwa uchache itawasajili wanachama wa mfuko huu kupitia (portal) daftari la waumini Kidigitali na kupitia mfumo huo wa kidigitali mfumo utamkata kila mwanachama wastani wa shilingi za Kitanzania 150 kwa siku au Tsh 1000 kila wiki na kikundi hicho kitastahiki kunufaika na mpango huu.
Baada ya wiki mbili za michango endelevu, mshiriki mmoja (1) atakayehitaji vipimo, matibabu, kulazwa na upasuaji ataanza kupata huduma hii.
Zaidi ya hayo, taasisi ya dini ambayo itaweza kusajili wanachama 400 au zaidi itaweza kugharamia matibabu ya wagonjwa wawili (2) na kuendelea. Sharti kuu kila kikundi (portal) liwe na wanachama 200.
Taasisi ya dini itayokidhi vigezo hivyo itapokea simu maalum iliyounganishwa na mfumo wa kufuatilia wanachama, michango na maendeleo ya ukusanyaji michango ya mfuko.
Mradi wa Bima ya Afya VIKOBA inalenga kubadilisha taasisi za dini kuwa vituo vya hifadhi na ustawi wa jamii na kuchochea kurudisha maumini waone taasisi za dini ni kimbilio lao na ni kituo cha kijamii.
6. TAMATI
Bima ya AFYA VIKOBA ni wezeshi (viable), wa gharama nafuu na endelevu. Mbali na wachangia wa mfuko huu kufaidika, lakini pia iwapo pesa yao waliyoichanga haikutumika kwa matibabu sehemu ya pesa hiyo itarudi kwa wenyewe. Eitha kwa kupunziwa kiwango cha kuchangia kwa mwaka unaofata au kwa kupewa makundi mengine yenye uhitaji zaidi kwa hiyari yao.
Upvote
21