SoC04 Bima ya Afya Vikoba

SoC04 Bima ya Afya Vikoba

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2014
Posts
984
Reaction score
1,179
umbrella.png

Kupitia mfumo wa kiditali bima ya AFYA VIKOBA itawezesha makundi tegemezi kama mwanafunzi, ombaomba nk kumudu gharama za matibabu kwa kuchangia Tshs 150 kwa siku, 1000 kwa wiki na 45,000 kwa mwaka. Na watoto umri wa siku 1 hadi miaka 4 wa mwanakikundi kupata tiba bure na hasa kwa magonjwa yanayofahamika magonjwa dume ambayo kimsingi hakuna wananchi wa kawaida anaweza kumudu matibabu yake. Mfano kansa, moyo, kisukari, mifupa

View: https://x.com/TheChanzo/status/1803824587886539068?t=Zfd784NPI_K42FgjwR7z6A&s=08

Source : The chanzo

1. UTANGULIZI

Wazo hili la kuanzisha bima ya afya VIKOBA lilijitokeza baada ya tukio la kusikitisha lililohusisha mgonjwa aliyelazwa katika moja ya hospitali ya rufaa ya Umma.

Wazo hili la kuanzishwa kwa bima ya afya VIKOBA kama suluhisho la kutatua changamoto za huduma za afya zinazoikumba jamii ya watu masikini nchini Tanzania lilitokana na utafiti binafsi nilioufanya hususan kwa mama mtu mzima mwenye umri niliokadiria wa zaidi ya miaka 70.

Mbali ya mama huyu, katika ufuatiliaji wangu niligundua kuwa wagonjwa wengi hukosa huduma za matibabu za kutosha ingawa hupokelewa na kulazwa hospitalini hapo .

Watu hawa walikosa kupatiwa huduma za vipimo na matibabu kutokana na uwezo wao mdogo wa kifedha.

Wale ambao waliopata sehemu ya matibabu mara nyingi walizuiliwa hospitalini hapo na hawakuweza kutoka wodini hadi madeni yao ya matibabu yatakapo malizika kulipwa ingawa kiuhalisia hawakuwa na uwezo huo wa kulipa.

Mfano mmoja muhimu ni huyo bibi mwenye umri wa zaidi ya miaka 70.

Bibi huyu baada ya kugundulika kuwa ana saratani ya utumbo mpana, alifanyiwa upasuaji wa njia mbadala ya kutoa haja kubwa ili kupunguza maumivu aliyokuwa akiyapata. Hata hivyo hakuweza kuendelea na matibabu zaidi kutokana na deni lake la matibabu na upasuaji wa shilingi za Kitanzania laki 7.

20240608_101411.jpg

Source: Remix AI

Zaidi ya hayo, nikiwa muumini wa kiislam ninaeingia misikitini tofauti tofauti kila muda wa swala unapofika, niligundua kuna gap kati ya waumini na wagonjwa waliolazwa hospitali hiyo. Kwani upo utaratibu wa kuwaombea /kuwasomea dua maalum kwa ajili ya wagonjwa na hasa aliyolazwa bibi yule. Maombi haya wakati mwengine hutoka kwa wauguzi katika hospitali hiyo kuu.

Hali hiyo iliniletea swali iwapo dua hizo pekee yake zawezaje kumsaidia mgonjwa mfano wa bibi yule bila juhudi ya kupatikana suluhisho la kijamii kwa wagonjwa wanaoletwa mahospitalini bila ya kupata matibabu wala huduma kutokana na uwezo wao mdogo wa kulipa gharama za matibabu.

Hali hii inaonyesha umuhimu wa mpango wa bima ya afya wa kina utakaokuwa na mahitaji yatokananayo na changamoto za jamii masikini, hivyo kuchochea kuundwa kwa Mradi wa Bima ya AFYA VIKOBA utaokuwa chini ya Taasisi na Jumuiya za Imani (msikiti, Kanisa, Temple) na kuratibiwa na taasisi huru itaokuwa na mfumo rasmi (portal) wa bima ya afya kidigitali.

Kupitia Bima ya afya VIKOBA itahusisha taasisi za kiimani (kanisa/misikiti) kama sehemu na wajibu wa imani tofauti zinazohimiza kutoa kwa ajili ya wenye uhitaji. Wakati huo huo mtoaji nae kufaidika.

2. HUDUMA ZILIZOPO KWASASA

Pamoja na kuwa na mifuko tofauti ya Bima inayotumika ukiwemo mfuko wa serikali yaani NHIF hata hivyo imeshindwa kukidhi mahitaji na matarajio ya watanzania. Moja ya sababu kubwa ni la kiitikadi ambapo serikali imeamua kujitenga kuhusisha shughuli zake kuchanganya na dini.

Ambapo kimsingi, dini na viongozi wa dini wanafanya kazi moja na Serikali, nayo ni kuhudumia jamii. Ambapo fursa waliyonayo, kauli zao zinaaminiwa zaidi na waumini kuliko kauli za viongozi wengine. Kwenye Taifa ambalo zaidi ya 85% ni waumini wa dini mbali mbali.

Huku Serikali yenyewe ikikiri kuwa Sera ya afya bure kwa watoto chini ya miaka mitano, wajawazito na wazee kushindwa kutekelezeka.

View: https://twitter.com/TheChanzo/status/1763213693276266962?t=R3-VEKJ6_DYpmDSiq7mcjg&s=19

Source: The chanzo

3. SIFA ZA ANAYESTAHILI KUJIUNGA NA MPANGO HUU WA BIMA AFYA VIKOBA

  • UMRI : miaka 5 hadi 100
  • UKUBWA WA KIKUNDi : Wanachama 200 waumini wa dini.
  • Bima hii ni ya Mwanachama mchangiaji, na watoto wao walio na umri wa siku 1 - hadi miaka 4 na siku 364 hawatohitaji kuwa sehemu ya wachangiaji.
  • Mwanachama ataruhusiwa kupata huduma kupitia hospitali ziliyoorodheshwa.

4. MAPENDEKEZO YA MKAKATI

Bima ya Afya VIKOBA inakusudiwa kuwa mpango wa hifadhi wa kijamii ambapo wanachama watakaochangia mfuko huu wataweza kupata huduma za matibabu yote pamoja na huduma za kulazwa. kwa kuanzia tutaanza na hospitali ya taifa Muhimbili pamoja na taasisi za afya za magonjwa maalum kama vituo vya matibabu ya mifupa Moi, hospitali za moyo JAKAYA, taasisi za kansa Ocean Rd.

Wanachama/waumini wanapaswa kujiunga na programu hii kupitia misikiti, makanisa, sinakogi, temple nk, kwa kujiegemeza kwayo. Taasisi hizo watakuwa wadhamini wao na na michango yao itapitia kwa taasisi hizo za dini kwa mwanachama kuchangia katika mfuko kupitia michango ya kila siku au kila wiki (Ijumaa, Jumamosi, Jumapili).

5. NJIA (APPROACH)

Bima ya afya VIKOBA umejielekeza katika taasisi za dini kwa maana makanisa, misikiti nk ambako wazazi na watoto wanakutanisha na kiongozi wanaemsikiliza, wanaemuamini na ambae akitoa maelekezo waumini hufata bila hata ya kuhoji.

Kupitia bima ya afya VIKOBA pesa wanayotoa muumini itawanufaisha wao wenyewe na au kuwanufaisha wenye uhitaji sawa na mafundisho ya kiimani yanavyotufundisha.

Taasisi ya dini ambayo ni kawaida kukutanisha waumini 200 kwa uchache itawasajili wanachama wa mfuko huu kupitia (portal) daftari la waumini Kidigitali na kupitia mfumo huo wa kidigitali mfumo utamkata kila mwanachama wastani wa shilingi za Kitanzania 150 kwa siku au Tsh 1000 kila wiki na kikundi hicho kitastahiki kunufaika na mpango huu.

Baada ya wiki mbili za michango endelevu, mshiriki mmoja (1) atakayehitaji vipimo, matibabu, kulazwa na upasuaji ataanza kupata huduma hii.

Zaidi ya hayo, taasisi ya dini ambayo itaweza kusajili wanachama 400 au zaidi itaweza kugharamia matibabu ya wagonjwa wawili (2) na kuendelea. Sharti kuu kila kikundi (portal) liwe na wanachama 200.

Taasisi ya dini itayokidhi vigezo hivyo itapokea simu maalum iliyounganishwa na mfumo wa kufuatilia wanachama, michango na maendeleo ya ukusanyaji michango ya mfuko.

Mradi wa Bima ya Afya VIKOBA inalenga kubadilisha taasisi za dini kuwa vituo vya hifadhi na ustawi wa jamii na kuchochea kurudisha maumini waone taasisi za dini ni kimbilio lao na ni kituo cha kijamii.

6. TAMATI

Bima ya AFYA VIKOBA ni wezeshi (viable), wa gharama nafuu na endelevu. Mbali na wachangia wa mfuko huu kufaidika, lakini pia iwapo pesa yao waliyoichanga haikutumika kwa matibabu sehemu ya pesa hiyo itarudi kwa wenyewe. Eitha kwa kupunziwa kiwango cha kuchangia kwa mwaka unaofata au kwa kupewa makundi mengine yenye uhitaji zaidi kwa hiyari yao.
 
Upvote 21
Kupitia Bima ya afya VIKOBA itahusisha taasisi za kiimani (kanisa/misikiti) kama sehemu na wajibu wa imani tofauti zinazohimiza kutoa kwa ajili ya wenye uhitaji. Wakati huo huo mtoaji nae kufaidika.
Nzuri sana hii kanuni, mtu anasaidia watu na anasaidiwa pia akipata matatizo hayo. Yote yanatimizwa kikamilifu.
 
Mkuu wazo lako la Bima hii , 👆 ime Baze kwenye Dini Tu, huoni Kwamba itakuja kutugawa Kwa misingi ya kidini.
Msingi wa serikali ni kuwaunganisha watu wote pamoja.

Lakin Haya yote yanatokea Coz , serikali ya CCM kuchota fedha za nhif na kuzipeleka kwenye chaguzi, bila kuzirudisha, nakuliacha shirika likiwa mufilisi
 
Mkuu ieleweke, mfumo huu haijabase kwenye dini bali kilichopo ni taasisi za dini zitakuwa wadhamini wako. Kwa maana hata wasio na dini wanaruhusiwa kujiunga kupitia taasisi hizo. Kama ambavyo wenye dini wamejiunga ktk bima za serikali isiyo na dini. Wenye dini hawajatengwa ilimradi tu wacomply.
 
Kupitia mfumo wa kiditali bima ya AFYA VIKOBA itawezesha makundi tegemezi kama mwanafunzi, ombaomba nk kumudu gharama za matibabu kwa kuchangia Tshs 150 kwa siku, 1000 kwa wiki na 45,000 kwa mwaka. Na watoto umri wa siku 1 hadi miaka 4 wa mwanakikundi kupata tiba bure.

1. UTANGULIZI

Wazo hili la kuanzisha bima ya afya VIKOBA lilijitokeza baada ya tukio la kusikitisha lililohusisha mgonjwa aliyelazwa katika moja ya hospitali ya rufaa ya Umma.

Wazo hili la kuanzishwa kwa bima ya afya VIKOBA kama suluhisho la kutatua changamoto za huduma za afya zinazoikumba jamii ya watu masikini nchini Tanzania lilitokana na utafiti binafsi nilioufanya hususan kwa mama mtu mzima mwenye umri niliokadiria wa zaidi ya miaka 70.

Mbali ya mama huyu, katika ufuatiliaji wangu niligundua kuwa wagonjwa wengi hukosa huduma za matibabu za kutosha ingawa hupokelewa na kulazwa hospitalini hapo .

Watu hawa walikosa kupatiwa huduma za vipimo na matibabu kutokana na uwezo wao mdogo wa kifedha.

Wale ambao waliopata sehemu ya matibabu mara nyingi walizuiliwa hospitalini hapo na hawakuweza kutoka wodini hadi madeni yao ya matibabu yatakapo malizika kulipwa ingawa kiuhalisia hawakuwa na uwezo huo wa kulipa.

Mfano mmoja muhimu ni huyo bibi mwenye umri wa zaidi ya miaka 70.

Bibi huyu baada ya kugundulika kuwa ana saratani ya utumbo mpana, alifanyiwa upasuaji wa njia mbadala ya kutoa haja kubwa ili kupunguza maumivu aliyokuwa akiyapata. Hata hivyo hakuweza kuendelea na matibabu zaidi kutokana na deni lake la matibabu na upasuaji wa shilingi za Kitanzania laki saba.

Zaidi ya hayo, nikiwa muumini wa kiislam ninaeingia misikitini tofauti tofauti kila muda wa swala unapofika, niligundua kuna gap kati ya waumini na wagonjwa waliolazwa hospitali hiyo. Kwani upo utaratibu wa kuwaombea /kusomea dua maalum kwa ajili ya wagonjwa na hasa aliyolazwa bibi yule. Maombi haya wakati mwengine hutoka kwa wauguzi katika hospitali hiyo kuu.

Hali hiyo iliniletea swali iwapo dua hizo pekee yake zawezaje kumsaidia mgonjwa mfano wa bibi yule bila juhudi ya kupatikana suluhisho la kijamii kwa wagonjwa wanaoletwa mahospitalini bila ya kupata matibabu wala huduma kutokana na uwezo wao mdogo wa kulipa gharama za matibabu.

Hali hii inaonyesha umuhimu wa mpango wa bima ya afya wa kina utakaokuwa na mahitaji yatokananayo na changamoto za jamii masikini, hivyo kuchochea kuundwa kwa Mradi wa Bima ya AFYA VIKOBA utaokuwa chini ya Taasisi na Jumuiya za Imani (msikiti, Kanisa, Temple) na kuratibiwa na taasisi huru itaokuwa na mfumo rasmi (portal) wa bima ya afya kidigitali.

Kupitia Bima ya afya VIKOBA itahusisha taasisi za kiimani (kanisa/misikiti) kama sehemu na wajibu wa imani tofauti zinazohimiza kutoa kwa ajili ya wenye uhitaji. Wakati huo huo mtoaji nae kufaidika.

2. HUDUMA ZILIZOPO KWASASA

Pamoja na kuwa na mifuko tofauti ya Bima inayotumika ukiwemo mfuko wa serikali yaani NHIF hata hivyo imeshindwa kukidhi mahitaji na matarajio ya watanzania. Moja ya sababu kubwa ni la kiitikadi ambapo serikali imeamua kujitenga kuhusisha shughuli zake kuchanganya na dini.

Ambapo kimsingi, dini na viongozi wa dini wanafanya kazi moja na Serikali, nayo ni kuhudumia jamii. Ambapo fursa waliyonayo, kauli zao zinaaminiwa zaidi na waumini kuliko kauli za viongozi wengine. Kwenye Taifa ambalo zaidi ya 85% ni waumini wa dini mbali mbali.

Huku Serikali yenyewe ikikiri kuwa Sera ya afya bure kwa watoto chini ya miaka mitano, wajawazito na wazee kushindwa kutekelezeka.

View: https://twitter.com/TheChanzo/status/1763213693276266962?t=R3-VEKJ6_DYpmDSiq7mcjg&s=19

Source: The chanzo

3. SIFA ZA ANAYESTAHILI KUJIUNGA NA MPANGO HUU WA BIMA AFYA VIKOBA

  • UMRI : miaka 5 hadi 100
  • UKUBWA WA KIKUNDi : Wanachama 200 waumini wa dini.
  • Bima hii ni ya Mwanachama mchangiaji, na watoto wao walio na umri wa siku 1 - hadi miaka 4 na siku 364 hawatohitaji kuwa sehemu ya wachangiaji.
  • Mwanachama ataruhusiwa kupata huduma kupitia hospitali ziliyoorodheshwa.

4. MAPENDEKEZO YA MKAKATI

Bima ya Afya VIKOBA inakusudiwa kuwa mpango wa hifadhi wa kijamii ambapo wanachama watakaochangia mfuko huu wataweza kupata huduma za matibabu yote pamoja na huduma za kulazwa. kwa kuanzia tutaanza na hospitali ya taifa Muhimbili pamoja na taasisi za afya za magonjwa maalum kama vituo vya matibabu ya mifupa Moi, hospitali za moyo JAKAYA, taasisi za kansa Ocean Rd nk.

Wanachama/waumini wanapaswa kujiunga na programu hii kupitia misikiti, makanisa, sinakogi, temple nk, kwa kujiegemeza kwayo. Taasisi hizo watakuwa wadhamini wao na na michango yao itapitia kwa taasisi hizo za dini kwa mwanachama kuchangia katika mfuko kupitia michango ya kila siku au kila wiki (Ijumaa, Jumamosi, Jumapili).

5. NJIA (APPROACH)

Bima ya afya VIKOBA umejielekeza katika taasisi za dini kwa maana makanisa, misikiti nk ambako wazazi na watoto wanakutanisha na kiongozi wanaemsikiliza, wanaemuamini na ambae akitoa maelekezo waumini hufata bila hata ya kuhoji.

Kupitia bima ya afya VIKOBA pesa wanayotoa muumini itawanufaisha wao wenyewe na au kuwanufaisha wenye uhitaji sawa na mafundisho ya kiimani yanavyotufundisha.

Taasisi ya dini ambayo ni kawaida kukutanisha waumini 200 kwa uchache itawasajili wanachama wa mfuko huu kupitia (portal) daftari la waumini Kidigitali na kupitia mfumo huo wa kidigitali mfumo utamkata kila mwanachama wastani wa shilingi za Kitanzania 150 kwa siku au Tsh 1000 kila wiki na kikundi hicho kitastahiki kunufaika na mpango huu.

Baada ya wiki mbili za michango endelevu, mshiriki mmoja (1) atakayehitaji vipimo, matibabu, kulazwa na upasuaji ataanza kupata huduma hii.

Zaidi ya hayo, taasisi ya dini ambayo itaweza kusajili wanachama 400 au zaidi itaweza kugharamia matibabu ya wagonjwa wawili (2) na kuendelea. Sharti kuu kila kikundi (portal) liwe na wanachama 200.

Taasisi ya dini itayokidhi vigezo hivyo itapokea simu maalum iliyounganishwa na mfumo wa kufuatilia wanachama, michango na maendeleo ya ukusanyaji michango ya mfuko.

Mradi wa Bima ya Afya VIKOBA inalenga kubadilisha taasisi za dini kuwa vituo vya hifadhi na ustawi wa jamii na kuchochea kurudisha maumini waone taasisi za dini ni kimbilio lao na ni kituo cha kijamii.

6. TAMATI

Bima ya AFYA VIKOBA ni wezeshi (feasable), wa gharama nafuu na endelevu. Mbali na wachangia wa mfuko huu kufaidika, lakini pia iwapo pesa yao waliyoichanga haikutumika kwa matibabu sehemu ya pesa hiyo itarudi kwa wenyewe. Eitha kwa kupunziwa kiwango cha kuchangia kwa mwaka unaofata au kwa kupewa makundi mengine yenye uhitaji zaidi kwa hiyari yao.
Mkuu, hoja yako ilipaswa iaksi dira ya maendeleo ya taia na dira haina ubaguzi. Wewe hili unalionaje?
 
Mkuu ieleweke, mfumo huu haijabase kwenye dini bali kilichopo ni taasisi za dini zitakuwa wadhamini wako. Kwa maana hata wasio na dini wanaruhusiwa kujiunga kupitia taasisi hizo. Kama ambavyo wenye dini wamejiunga ktk bima za serikali isiyo na dini. Wenye dini hawajatengwa ilimradi tu wacomply.
Kwa hiyo serikali imeshindwa mpaka tutumie dini kuwa msimamizi, mbona unaongeza urasimu,
Kumbuka hizo Dini hazitambui Bima kwenye mafundisho Yao.
 
Kwa kauli ya serikali yenyewe mifuko yao imeshondwa kuwasaidia walengwa.

Na naamini hii ni njia MBADALA ya kuwafikia walengwa. Ambapo hali ilivyo kwasasa wakitoa sadaka zao zinakwenda kwa Mungu na haziwanufaishi tena.

Dini zinatambua mfumo huu wa bima ambapo wachangiaji wasipoumwa pesa waliochangia inarudi tena kwao baada ya kukatwa kiasi kidogo cha pesa za uendeshaji. Kwa mfano ktk imani ya Uislam inaitwa TAQAFUL INSURANCE.

Mfuko huu wa bima ya afya unatoa kama sadaka inavyokwenda kumnufaisha mgonjwa ambay si kwamba alikosa daftari wa kujua tiba ya ugonjwa wake, so kwamba kukosekana madawa na vifaa tiba. Serikali imewekeza sana hilo. Bali alikosa pesa za kumtibia. Lkn si huyo tu, kila binadamu ni mgonjwa mtarajiwa kwa wewe unatoa mchango au sadaka hiyo ukija kuumwa itakuja kukusaidia.

"Sera ya afya bure kwa watoto chini ya miaka mitano, wajawazito na wazee haitekelezeki"

Serikali

View: https://twitter.com/TheChanzo/status/1763213693276266962?t=R3-VEKJ6_DYpmDSiq7mcjg&s=19
 
Mkuu, hoja yako ilipaswa iaksi dira ya maendeleo ya taia na dira haina ubaguzi. Wewe hili unalionaje?

Mkuu kama nilivyotangulia kumjibu mchanguaji aliyepita, mfumo huu haijabase kwa watu wa dini pekee bali approach ya kukusanya michango ndio unapitia kwa watu (viongozi) wenye ushawishi mkubwa kwa jamii. Badala ya kupitia kwenye taasisi na viongozi wa serikali, mfano mtendaji kata au walimu wakuu wa shule kama ilivyo kwa bima toto. Approach iliyoshindwa mapema.

Mfumo huu utapitia kwa taasisi za dini.

Kwa maana ingine hata wasio na dini wanaruhusiwa kujiunga kupitia taasisi hizo. Twaweza pia kuongeza wigo nao walipitia katika taasisi zao wanazoziamini. Sharti isiwe kujiunga direct. Lazima kupitia kwa taasisi. Na lengo kuu ni kuachana na mfumo wa sasa wa kichoyo ambapo mtu na familia yake (wategemezi wake).

Mfumo huu unalenga kusaidia wenye uhitaji zaidi huku anaedaidia nae ni mnufaika.

kwa maana ingine hakuna misingi ya kibaguzi bali tunaondoa misingi ya KICHOYO.
Kama ambavyo wenye dini wamejiunga ktk bima za serikali isiyo na dini. Kwanini bima ya serikali isiyo na dini ionekane haina ubaguzi wakati misingi ya dhana hii inatokana na Wakana Mungu.

Hivyo mfuko huu ni MBADALA, unatokana na dhana ya "Wenye Kuamini Uwepo wa Mungu"

Na kwamba mwisho wa siku kutakuwa na ushindani wenye faida.

Kuwa ni sera na itikadi gani yenye manufaa kwa taifa.

Ile ya wakana Mungu iliopo Au Sera ya Waamini Uwepo wa Mungu.

kwa ufupi mfuko huu unaleta dira MBADALA ya Taifa. Kutoka Taifa la kisekyula (lisilo na dini) kuwa na taifa la Kidaivasi (Diversity State) Kwa maana ya Taifa la dini Zote, falsafa yangu.

Hii haina maana tutaendesha taifa kwa misingi ya kidini. Laa. Bali tutahusisha taasisi za dini katika mambo muhimu kuwa ni sehemu ya serikali kuunganisha, kufamasisha na kichocheo cha maendeleo.

Lakini pia serikali hiyo mpya inaweza kuwadhibiti viongozi wa dini wanaotumia dini kunyongwa waumini.

Dhana ya toa kwa ajili ya Mungu, kumbe ni kwa ajili yake mwenyewe.

Pesa za sadaka ilitumika sawa na matakwa ya Mungu manake tunapaswa zirudi kusaidia jamii.
 
Back
Top Bottom