SoC02 Bima ya Afya ya Jamii

SoC02 Bima ya Afya ya Jamii

Stories of Change - 2022 Competition

think tank01

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2022
Posts
270
Reaction score
400
BIMA YA AFYA YA JAMII 🇹🇿

UTANGULIZI
;

Salamu Watanzania wote.
Ni muhimu kwa nchi hasa zinazoendelea, kuwa na dira/sera ambayo ndio muongozo wa utoaji na usimamizi wa huduma na maendeleoya nchi husika.
Ili nchi yoyote isonge mbele kiuchumi, inahitaji jamii yenye Afya Bora ili kuwezesha uzalishaji mali katika nyanja mbalimbali, mfano; Kilimo, Michezo, Afya, Viwanda, Uongozi n.k.


UFAFANUZI
;
Katika taifa lolote ni muhimu zaidi wananchi wawe na Bima ya/za Afya zitakazo wawezesha kupata huduma mbalimbali za Afya kwenye Vituo vya kutolea huduma za Afya, hasa hivi vinavyo jengwa kwa nguvu na Serikali kwa lengo la "KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA KARIBU KABISA NA JAMII".
Kufanikisha lengo hilo, "Serikali ilianzisha Mfuko wa Afya ya Jamii kwa Sheria ya mwaka 2001, ambapo kila Halmashauri ilitakiwa kuanzisha mfuko huo."

Sera hii ya Bima ya Afya ya Jamii ikasimamiwa na kusisitizwa kwa Wananchi kikamilifu na Serikali yetu kwa kuhakikisha kila kaya nchini ambayo haina mmoja wa mwanafamilia ambaye ni mwajiriwa wa Serikali (huyo atakua na Bima ya Taifa) basi hio familia wajiunge na Bima ya Afya ya Jamii kwa mujibu wa Sheria hio ya mwaka 2001.

Matokeo ya mfuko huu tangu kuanzishwa kwake yamekuwa na Mafanikio na Changamoto tofauti tofauti baina ya Halmashauri moja na nyingine kutokana na uwezo wa ufanyaji kazi wa Mfumo wa Mfuko au usimamizi hafifu wa Waratibu walioteuliwa kusimamia mfumo huo. Kufuatia changamoto zilizo jitokeza, Serikali ya awamu ya Tano (na zinazoendelea) ilidhamiria kufanya maboresho katika maeneo matatu ambayo ni;
  1. Usimamizi na Uendeshaji,
  2. Usajili wa Wananchama wa Mfuko,
  3. Kitita cha mafao na Ngazi ya Upatikanaji wa huduma za Afya.

Mwananchi (familia) yeyote ili aweze kujiunga anapaswa kufika katika Ofisi ya Kijiji/Eneo la kutolea huduma za Afya hapo atakutana na Msajili wa Bima, kikubwa awe na Orodha ya watu SITA watakao unganishwa wenye umri kuanzia miaka 5 na kuendelea, Bima hio itakua ina huishwa kila baada ya miezi 11.

Gharama za kujiunga na Bima ni Shilingi 40,000/= kwa mtu mmoja na Shilingi 150,000/= kwa watu SITA -Dar es salaam na Shilingi 30,000/= Mikoa mingine, Tanzania.

Kwa Bima hii ya Jamii iliyoboreshwa huduma zilizoamriwa utazipata katika;
  • Ngazi ya Zahanati.
  • Ngazi ya Kituo cha Afya.
  • Ngazi ya Hospitali ya Wilaya.
  • Ngazi ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa.

Baadhi ya watumiaji wa Bima hudai wanakosa Dawa au Vipimo waendapo kupata huduma, Changamoto hizi ni vyema mambo yafuatayo yafanyike;

Moja; Watoa huduma za Afya vituoni, watenge "Chumba/Kabati la Dawa" kwa ajili ya Wateja wenye Bima ya Afya ya Jamii na dawa zao zinazopatikana na ikiwezekana Ushahidi wahilo kufanyika tuuone kwa picha kupitia tovuti mbalimbali za Wizara ya Afya ikionesha Kituo A Halmashauri A kimetenga Dawa kwa Wateja wenye Bima.

Mbili; Serikali itoe ufafanuzi wa idadi na makundi ya Dawa, Vipimo na Huduma zingine ambazo mteja mwenye Bima ya Afya ya Jamii atazipata na zile atakazozikosa kutokana na gharama kubwa ya Dawa, Vipimo au huduma hizo.

Tatu; Watumishi wa umma kwenye Vituo vya kutolea huduma za Afya wabandike Orodha ya Dawa, Vipimo na Vifaa Tiba vinavyo patikana kwa kila mwezi ili mteja akikosa Dawa au Kipimo ajue haipo ila kaandikiwa sababu vinahusiana na ugonjwa wake unao msumbua.

Nne; Jamii zetu nchini bado zina dhana ya "Mwanamke Mjamzito, huduma za Afya ni Bure". Wakati wa ujauzito hasa miezi ya mwanzo ya ujauzito kuna maudhi madogo madogo au homa za mara kwa mara ambazo Mjamzito hukumbana nazo, na inamhitaji kutumia dawa ili awe sawa. Hivyo kwa kua Jamii bado ina amini huduma za Afya kwao ni bure, ni wakati wa Serikali kutoa elimu kua huduma za bure kwa Mjamzito ni kwa ule ugonjwa unaotokana "Mimba" au Wakati wa Kujifungua tu na sio kila akiumwa au mfano kajikata na jembe shambani au na kisu jikoni halafu afike hospitalini atibiwe "Bure" sababu ana mimba.

Tano; Kwa wazee walio na miaka kuanzia 60 na kuendelea wanaotibiwa kwa "Msamaha" wapitiwe upya wathibitishwe kua hawawezi kulipia huduma za Afya ndipo wapewe fomu maalumu ya kupewa huduma Bure/Msamaha kwani kuna baadhi ya familia ambazo watoto wao wako vizuri kiuchumi ila kwa kuwa mzazi/wazazi wao wana miaka kuanzia 60 na kuendelea wamewaombea "Fomu ya msamaha" kwa ajili ya kupata Matibabu.

Sita; Katika kusimamia Mapato na Matumizi yatokanayo na Bima ya Afya ya Jamii, Serikali ingefundisha (Raia wa kawaida asie Mtumishi) na kuajiri ili majukumu yake katika Kituo husika cha kutolewa huduma za Afya yawe;
  • Kusajili Wananchama.
  • Kuhuisha Bima.
  • Kuhakiki Bima mteja anapofika kupata huduma.
  • Kutuma na kufatilia Madai ndani ya muda.
  • Kusimamia Mapato na Matumizi yatokanayo na Bima ya Afya ya Jamii.
Sambamba na hayo pia anaweza kufanya kazi za;
Kupokea, kutoa risiti na kutunza Fedha za Papo kwa Papo kabla hazijapelekwa benki na Mganga Mfawidhi wa Kituo husika. (Uanzishwaji wa dirisha la malipo na Bima)
Kuwaombea msamaha wa matibabu kwa wazee ngazi husika ( Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya) kwa kuthibitisha kua wanafamilia hio hawawezi kuchangia huduma au kukata Bima ya Afya ya Jamii

HITIMISHO
:
Serikali kupitia kwa Waratibu wa Bima ya Afya ya Jamii wa Wilaya na Mkoa, wawe wanatoa takwimu kila mwezi au baada ya miezi mitatu kwenye Vituo vya Redio na Gazeti la Serikali ili wananchi wajue idadi ya waliokwisha kujisajili na Mfuko huu, lengo ni kuweka ulinganisho kwa maana ya wenye Bima na wasio kua na Bima ambapo wasio kua na Bima ni matumaini yangu kua watahamasika zaidi kujiunga.

"Wananchi wenye Afya Bora ndio Mtaji wa Maendeleo ya Nchi".

Asanteni!
 
Upvote 3
Ndugu Watanzania wote, nawakaribisha kusoma andiko langu lenye lengo la kuelimisha na kuhamasisha wananchi tujiunge na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (CHF) kwa ajili ya kupata Matibabu.
Pia waweza kulipigia kura na kuchangia mawazo andiko hili ukiwiwa.
Asanteni.
 
Hongera mkuu nishawahi kuwa na Bima zote hizo yaani CHF na NHIF ila nawashauri mamlaka zinzojihusisha na Bima za Afya waongeze uweledi na wanaosimamia Bima za Afya wapunguze upigaji Ili kuweza kuleta matokea yenye tija.
 
Hongera mkuu nishawahi kuwa na Bima zote hizo yaani CHF na NHIF ila nawashauri mamlaka zinzojihusisha na Bima za Afya waongeze uweledi na wanaosimamia Bima za Afya wapunguze upigaji Ili kuweza kuleta matokea yenye tija.
Kabisa mkuu
 
Bima ya Afya ni muhimu sana. Usipokuwa na Bima ya Afya waweza kujikuta unalipa zaidi ya elfu hamsini Kwa siku Moja wakati Bima ya Afya ungeweza tumia 50000/= kutibiwa mwaka mzima.
 
Back
Top Bottom