Bani Israel
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,775
- 3,593
Ngoja niwape stori, mwaka juzi tulitoka Dar kwenda Tabora kufanya biashara ya kuuziana gari ambayo ilipostiwa humu humu JF.
Tukafika Tabora tukaiona gari tukarizika nayo, tukapana, tukailipia, tukaingia sheri, tukajaza mafuta, tukatoka kuianza safari ya kurudi Dar.
Mbele kidogo akili ikanija ngoja nifungue droo za ile gari kuweka kadi, ile kufungua tu nakutana na vifurushi kama 9 hivi, kuna vyeupe, vyeusi na vyekundu nikastuka sana.
Nikamwambia jamaa paki tuwaambie jamaa kuna vitu vyao wamesahau humu. Kweli tukampigia mwenye gari tukamwambia kaka kuna vitu vyako umesahau humu kwenye droo.
Jamaa akanijibu usiogope hizo ni zako siyo zangu, hiyo gari huwa haina bima! Hizo ndiyo bima zake, ndiyo maana nilikwambia gari ina bima kubwa. Ndiyo hizo!
Asee nikamwambia nazitupa, akanambia ukitupa hizo manyoni hutoboi!
Mpaka leo ninazo napeta tu. Gari ina deni la laki 7 na ushee na polisi hawajawahi inasa kwenye kamera za barabarani, napita nanyata lakini kamera hazioni deni!
Tuheshimu tamaduni zetu jamani, ni tiba kubwa sana kwetu.