Bima ya mtoto wa mtumishi wa umma itasaidia matibu ya Moyo Taasisi ya Jakaya Kikwete?

Bima ya mtoto wa mtumishi wa umma itasaidia matibu ya Moyo Taasisi ya Jakaya Kikwete?

Kategele

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2017
Posts
1,055
Reaction score
2,466
Habari wana JF, na poleni kwa msiba pia.

Mwanangu mwenye miezi 10 kaonekana ana shida ya moyo na madakitari wa BUGANDO wamesema suala lake lipo serious inabidi kupewa rufaa ya Taasisi ya Moyo ya JAKAYA.

Hivi Bima ya mtoto itasaidia gharama zote za matibabu na Operation?
 
Pole mkuu. Siku hizi BIMA wamezibana sana ila naamini itaweza ku-cover ebu njoo kwanza au tusubiri wengine.
 
Mkuu, NHIF huwa hawako wazi sana kwenye gharama zao, ila nafikiri katika hali ya kawaida inatakiwa ihusike pia katika eneo hilo.Cha kufanya wewe nenda Katika hio hospitali na BIMA yako wamtibu mwanao. SAVE the LIFE FIRST and worry about the money later.
 
Bima inataratibu zake, nenda ofisi za NHIF pale Buzuruga watakupa taratibu. Pole
 
Mradi una bima,we nenda hapo Jk heart Institute.mengine yatajipa yenyewe.msingi wa kuanzia unao,kunaweza kukawa na gharama zingine za matibabu ukahitajika kuongeza hela, lakin asilimia kubwa utatibiwa kwa bima

Toka nianze kumpeleka mzee wangu hapo sijawahi ongeza hela zaidi ya bima. Gharama zangu ilikuwa ni nauli tu
 
BIMA ya NHIF ina Packages zake, mara nyingi kwa JKCI nimeona NHIF huwa ipo kwa packages za NAJALI, WEKEZA, TIMIZA na NHIF ambayo ikiingia katika system huwa inasoma kama NHIF tu bila kuwa specified.

Kama NHIF yako ni aina ya NAJALI, WEKEZA, TIMIZA hapo kuna usumbufu utapata kwa baadhi ya huduma kulingana na Package yako.

Kama una NHIF ya kawaida ambayo haiko specified na packages nilizozitaja hapo juu.. Utapata huduma zote kulingana na utaratibu wa Bima ya NHIF na usumbufu kidogo unapungua.

Pia kuna zile NHIF ambazo huwa zina mkono wa taasisi na mashirika ya serikali mfano NHIF BUNGE, NHIF TRA, NHIF NMB BANK, NHIF BOT, nk. hawa huwa ni VIP Bima zao hazina longo longo wanapata kila kitu wakifika JKCI.

Ila kwa vyovyote vile ukiwa na kadi ya BIMA ya NHIF unaepuka usumbufu mkubwa sana ukienda JKCI, Unakuwa rahisi sana kuhudumiwa na kuonana na Daktari kwa kuwa mfumo wao pale una favor kuchakata taarifa za mtu aliyekuwa na BIMA kuliko mtu asiyekuwa nayo.

Muhimu mpeleke tu mtoto akapate huduma hayo mambo mengine watakusidia wahusika na isitoshe ofisi za Bima zipo karibu tu pale mule mule Muhimbili, kwahiyo changamoto yoyote ile inaweza kupatiwa ufumbuzi siku hiyo hiyo.
 
Kamaa bimaa ni ya mfanyakaz wa umma anayekatwa monthly kwenye mshahara bas ita cover mie nauguza bi mkubwa pale muhimbili anatumia dawa za cancer ni ghali mno ila anapata huduma japo kuna kibali kitatakiwa kukatwa kama garama za dawa na vipimo vitakuwa ghali sanaa

Polee sanaa mkuuu Mungu akufanyie wepesi na uzur tatzo limejulikana mapema
 
Back
Top Bottom