Bima za afya ni hatari sana kwenye vituo binafsi vya afya

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Yalishawahi kunikuta. Yaani hizi hospitali binafsi wakishagundua tu wewe au mtoto wako ana bima ya afya ya kueleweka, basi wanaanza kumbambikia magonjwa makubwa makubwa ya ajabu ajabu.

Kuna kipindi walimsingizia mwanangu ugonjwa wa kifafa pindi alipopelekwa na mama yake kwenye hospitali moja kubwa binafsi, alipokuja kuniambia moyo ukanilipuka. Nikaingia google na kuanza kusearch zile dalili, haraka sana google ikaniambia ni ‘Febrile seizure’, kucheki google translator ikabiambia maana yake ni ‘dege dege’.

Nilichanganyikiwa, maana walimpa prescription ya dawa za kifafa za kutumia mwaka mzima, bahata nzuri ndio alikuwa ametumia wiki tu.

Nilipowafuata wakajidai kuwa hawamtambui kama aliwahi kuja kutibiwa hapo, nilipowaonyesha risiti za makato ya bima ndio ikabidi waniunganishe na dokta mwingine kunipa ufafanuzi, maana yule alieandika hiyo midawa alikimbia.., eti wananiambia ni makosa ya kibinadamu.., kwamba mama yake hakutoa malezo ya dalili vizuri..

Haya kucheki bima ya mtoto nakuta wamelamba milioni moja na zaidi kwa dawa na vipimo…, yaani nilisikia hasira, ilikuwa niwashtaki kabisa.., sema ndio vile tu.., mitaasisi mikubwa binafsi kama ile huwezi kuwashinda mahakamani, maana watafuta evidence zote za mgonjwa kwenye system zao na kukana kumjua baadae..

Kuna movie nimeiangalia usiku huu Mnet Movies 4 ikanikimbusha hii incident..

Kama unajiweza, usidiriki kutumia bima kwenye mahospitali makubwa binafsi ya kibiashara, labda za serikali.., utasingiziwa magonjwa ya gharama gharama ili wafikisi mifuko ya bima, na hapa mlengwa mkubwa ni NHIF..
 
Ulichoandika kuna uongo mwingi ina maana havikuchukuliwa vipimo maabara? Daktari kabla kutibu huchukua vipimo toka maabara sio tu kusikiliza maelezo ya mgonjwa

Hospitali gani kubwa hutibu kwa kumuangalia tu mtu usoni?
 
Ubepari ni unyama.

Watu kama hao baadae ukiwakuta kwenye bar au nyumba za ibada ni watoaji sana illi waonekane machoni mwa watu kuwa ni wema.
 
Ulichoandika kuna uongo mwingi ina maana havikuchukuliwa vipimo maabara? Daktari kabla kutibu huchukua vipimo toka maabara s

Hospitali gani kubwa hutibu kwa kumuangalia tu mtu usoni?
 
Ulichoandika kuna uongo mwingi ina maana havikuchukuliwa vipimo maabara? Daktari kabla kutibu huchukua vipimo toka maabara sio tu kusikiliza maelezo ya mgonjwa

Hospitali gani kubwa hutibu kwa kumuangalia tu mtu usoni?
Yule Dokta baada ya kumbana alijiyeyea kwamba vipimo vya Scan walivyopima vilionyesha ‘Hertz’ ngapi sijui, maana yake ana ‘Absent seizure’, kwamba tafsiri yake ni Kifafa! Sasa nikamuuliza mbona dalili za huyu mtoto nimesearch google inaonyesha ni dege dege?!

Akasema kwamba huwa wanasoma vipimo vya Scan pamoja na maelezo ya mgonjwa, kwamba hata ukipima watu 100 randonmly kwa hiyo scan machine yao, 10% wataonekana wana kifafa hata kama hawana, hivyo wanaangalia na dalili pia, sasa wanasema eti mama yake hakuwapa dalili vizuri, inaingia akilini hiyo?!
 
Hiyo ya kwako ni special case watu mamilioni wanatibiwa na bima ya afya kila siku kwa miaka hospital za private kubwa na ndogo hawajapata hilo tatizo la kubambikwa magonjwa
 
Ulichoandika kuna uongo mwingi ina maana havikuchukuliwa vipimo maabara? Daktari kabla kutibu huchukua vipimo toka maabara sio tu kusikiliza maelezo ya mgonjwa

Hospitali gani kubwa hutibu kwa kumuangalia tu mtu usoni?
Acha kusema ni uwongo, binafsi yaliwahi kunikuta Daktari alinibandika ugonjwa wa uwongo ili apige pesa, nina hasira naye mpaka leo, watu wapumbavu ni wapumbavu tuu hata wasome vipi
 
Hiyo ya kwako ni special case watu mamilioni wanatibiwa na bima ya afya kila siku kwa miaka hospital za private kubwa na ndogo hawajapata hilo tatizo la kubambikwa magonjwa
Hii case sio mara ya kwanza kuletwa humu au watu kusikia mitaani

Hadi unampinga mtu namna hii basi kuna jinsi huu mchezo unakuhusu au una maslahi nayo.
 
Acha kusema ni uwongo, binafsi yaliwahi kunikuta Daktari alinibandika ugonjwa wa uwongo ili apige pesa, nina hasira naye mpaka leo, watu wapumbavu ni wapumbavu tuu hata wasome vipi
Daktari anapigaje pesa kwa kukubandika ugonjwa .? Daktari analipwa kwa masaa au idadi ya anaowahudumia
Hakuna daktari analipwa kwa kubandika mtu magonjwa
 
Hiyo ya kwako ni special case watu mamilioni wanatibiwa na bima ya afya kila siku kwa miaka hospital za private kubwa na ndogo hawajapata hilo tatizo la kubambikwa magonjwa
Hibi mimi nisinhekuwa mtu anaejielewa na aliyeelimika kiasi cha kuweza kufanya enquiry mtandaoni na kuanza kubishana nao ingekuwaje?

Si ningeamini tu na kumpa mtoto midawa mwaka mzima.., mbonamama yake walishamwingiza kingi kabisa! Ni vile tu mimi ni mtu ninaejielewa, i am not a push over, mwanzo daktari alibisha, eti ananiambie yeye ndie dokta hivyo nitulie tu mtoto apone, mxnge yule!!

Baada ya kuona baba mtu nimechachamaa anabadili gia angani, anasema mama hakutoa maaelzo mazuri, namwambia nioe file lake ulikochukua maelezo ya mama hataki!
 
Daktari anapigaje pesa kwa kukubandika ugonjwa .? Daktari analipwa kwa masaa au idadi ya anaowahudumia
Hakuna daktari analipwa kwa kubandika mtu magonjwa
Miki najuaje commission scheme waliyowekeana kati ya hospitali na daktari?! Kwamba ukiingizia hospitali hivi unapata hiki, how am i to know?! No wonder NHIF inafilisika, ukichunguza ni hivi vituo binafsi
 
Kwamba kisa maaadili hayaruhusi ndio guarantee kwamba wanfuata hayo maadili?! Pengine wameweka monthly quotas za kumeet? How am i to know?!
Kifupi hizo situation za kufikirika haziko kwenye fani ya udaktari duniani kote
Hospitali ni huduma sio biashara.Haina cha mambo ya target kama mtu unauza njugu
Watu kuumwa huwezi weka target kuwa mwezi huu wataumwa mia na kuja hospitali
 
Toa matokeo ya vipimo na dawa zilizotolewa (prescribed) kuna madaktari wa binadamu humu wataseme probable medications zilikuwa right or wrong
Ni kitu cha muda kidogo, ila nakumbuka kipimo kilikuwa kinaitwa ‘EGG’ sijui, halafu kikasma matokeo ni ‘Hertz 8’ kitu kama hivho, halafu conclusion ikawa ni ‘Absent Seizure’, ambayo wakadai ni kifafa. Dawa ndio hivyo vidonge vya mwaka mzima, mara sijui unamega nusu nisu, , baadae unampa kizima sijui, halaafu mwisho unaamza kufanya wanaita ‘Tappering’ , kwamba unapunguza dozi, yaani mwaka mzima, sasa hiki kipimo baadae anasema sio decisive, kwamba eti wanaangalia maelezo pia.., blaa blaa nyingi..!
 
Kifupi hizo situation za kufikirika haziko kwenye fani ya udaktari duniani kote
Hospitali ni huduma sio biashara.Haina cha mambo ya target kama mtu unauza njugu
Watu kuumwa huwezi weka target kuwa mwezi huu wataumwa mia na kuja hospitali
Sio biashara au sio? Sawa…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…