Binadam bwana, hebu sikia hii

Mr Mikazo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2016
Posts
1,594
Reaction score
800
"Tatizo Simba mnamtegemea sana Mavugo, alishindwa kufunga huyo ndio basi tena, mpira haupo hivyo"

ONE MONTH LATER

"Simba pale ukimbana vizuri Tshabalala umekwisha, magoli yote anatengeneza yeye hakuna tena, ni kikosi kile kile tu cha kutegemea wachezaji wawili, bado sana"

EARLIER THIS MONTH

"Simba tatizo lao kila kitu Kichuya, siku akiumia yule na mpira ndio umekwisha maana ndio anatengeneza na kipika magoli, ndio mhimili wa timu bado mna safari ndefu sana"

YESTERDAY

"Mnaingia mnamtegemea Mzamiru, mchezaji haeleweki yule lazima mle goli, mechi za ugenini hamna ubavu wa kushinda, huyo Mzamiru atakutana na beki wenye njaa atatulizwa"

TODAY

"Mnaona sasa mnavyotegemea mchezaji mmoja? MO Ibrahim jana kawabeba sana, yaani bila yeye sijui mngetokaje.. Chezeni kama timu sio kutegemea mtu mmoja"

NEXT WEEKEND

"mmekutana na timu vibonde, hao Stand wameshajichokea Mwadui hawana kocha, wala msione kama mmefanya kitu kikubwa, subiri mzunguko wa pili ndio mtakiona cha moto na kutegemea mchezaji mmoja kitawaumiza"

HITIMISHO.

Tumesajili wachezaji ili tuwategemee, UNATAKA TUMTEGEMEE BABAAKO? Tunataka tutegemee kila mchezaji mwaka huu, ipo siku mtasema bila Angban Simba si lolote si chochote, endeleeni kuwahesabu mmoja baada ya mwingine
 
Breaking news

*Vigogo WA Yanga wazuiliwa kuingia kambini*

Na mwandishi wetu Julius Azizi

Uongozi WA timu ya mbao umewazuia watu WA tano walio taka kwenda kuonana na wachezaji WA timu hiyo. Kwamujibu WA uongozi WA mbao fc umesema kulikuwa na msafara wawatu watano waliotaka kwenda kambini kwao wakati WA mazoezi Jana jioni huku wakiwa nadhamira yakuonana nawachezaji watimu hiyo watu hao wanadaiwa kuwa ni wanachama wa yanga na kati yao ni vigogo katika club ya jangwani .
Miongoni mwawatu hao mmojawao nikiongozi mkubwa serikalini na anashiriki katika mambo mengi yakimaendeleo ndani ya timu hiyo.
Baada ya kutaka kujua majina ya Vigogo hao wanaodaiwa kuwa ni wa yanga kutaka kuonana na wachezaji wa mbao baada ya mazoezi hapo jana uongozi wa mbao fc ulisita kuweka wazi nakusema kwavile hawakuwapa ruhusa ya kuonana na wachezaji hivyo si muhimu kwao kuwataja.
C&P
[emoji115][emoji134][emoji134][emoji134]
 
Nyie chezesheni mikia, mtanyamaza tu
wanakelele hao yaan wanaanzaga kwa mikwara mwishon pumz zinakata ligi inaisha wapo nafas ya 5. Timu kubwa hawajashiriki kimataifa miaka 3 bado wanapiga kelele
 
Kuokota habar za mitaan halafu kuzileta jukwaani ni aibu kwako na kwa yule uliekopi kwake...ndo mana jukwaa hiki likaitwa great thinkers....hv sheria ya kuwabana hawa watu wanaopakaza habar bila kuwa na ushahid hazipo TFF?
 
Kuokota habar za mitaan halafu kuzileta jukwaani ni aibu kwako na kwa yule uliekopi kwake...ndo mana jukwaa hiki likaitwa great thinkers....hv sheria ya kuwabana hawa watu wanaopakaza habar bila kuwa na ushahid hazipo TFF?
TFF ni nani? Nijb hapo ndo tuanze mengne
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…