Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 23,234
- 28,473
Anaamka mtu na pombe zake kichwani na kutamka eti, tuna Rais katili sana, nacheeka sana, wanasahau ya kwamba, hata mikutano yao ilizuiliwa, wengine walipasuliwa mifupa, wengine walikimbia nchi mazima, wengine waliwekwa kwenye viroba, kweli shukurani ya punda ni mateke, eti wanasahau kabisa, ya miaka minne tu iliyopita, nacheka sana, kibaya baadhi yao wanasema eti, bora yule wa viroba baharini kuliko huyu aliyewapa, uhuru, ukweli, Furaha na amani, narudia kweli binadamu habebeki hata ukimpa nini milele hataridhika haa.....
Wakati ule, habari zilikuwa ni kama hizi, -
MAITI ZAOKOTWA MTO RUVU.
~~~~
Maiti sita ambazo hazijatambulika zimekutwa zikielea katika Mto Ruvu eneo la Bagamoyo, Mkoa wa Pwani zikiwa zimehifadhiwa kwenye mifuko ya Sandarusi maarufu viroba vya uzito wa Kilogramu 200, huku zikiwa zimeharibika vibaya. Diwani wa Kata ya Makurunge, Paul Kabile alisema maiti hizo ambazo ni za jinsia ya kiume ziligunduliwa na wavuvi Kabile alisema maiti tano ziligunduliwa.
Desemba 6 majira ya alfajiri kwenye Kitongoji cha Kitopeni wilayani Bagamoyo, ambako wavuvi hao waligundua miili hiyo wakati wakiendelea na shughuli zao kwenye Mto huo "Maiti hizo kila moja
ilikuwa imehifadhiwa kwenye kiroba huku zikiwa zimewekewa mawe
na mifuko hiyo ikiwa imeshonwa juu kama vile yamehifadhiwa mahindi
au mchele" alieleza.
Kabile alisema kuwa wavuvi hao baada ya kuziona maiti hizo walizizika kutokana na kuharibika sana na kushindwa kuzipeleka hospitali kuzihifadhi. "Wavuvi hao walizizika maiti hizo huku kukiwa hakuna taarifa yoyote juu ya kuwa zimetoka wapi na ni watu gani waliofanya tukio hilo",
alisema Kabile na kubainisha kuwa maiti nyingine moja iligunduliwa jana.
Mwandishi wa habari wa jeshi la polisi Mkoa wa Pwani, Hassan Mtengevu, alithibitisha kutokea tukio hilo, na kueleza kuwa wanafanya
uchunguzi kwa kushirikiana na daktari ili kufahamu watu hao walikufa kwenye mazingira gani.