Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Binadamu kiasili ameumbwa na hofu mbili tu,yaani hofu hizi ndio asili yake
Hofu ya kwanza ni kuanguka,hii ni hofu ya asili tangu tukiwa utotoni, ndio maana mtoto ambaye anaanza kusimama mara nyingi huwa na hofu ya kuanguka
Hofu ya pili ni ya sauti, hizi hofu mbili hatukufundishwa bali tumekuwa nazo kiasili tangu utotoni
Hofu nyingine zote tumefundishwa katika makuzi yetu,mfano mtoto ambaye hajajua hatar ya nyoka hawezi kumuogopa nyoka,na si ajabu ukamkuta anacheza na nyoka
Mtoto ambaye hajajua hatar ya moto labda mpaka umuunguze au aambiwe huo moto utaungua,ndio maana kuna msemo kama mtoto akililia wembe mpe kwani akijikata atajua kuwa wembe ni hatar
Ninachotaka kusema hapa,si kila jambo ni la kuhofia kwasababu hofu yako wewe sio hofu yangu mie,kama wewe unahofia single maza kwangu mimi ni watamu na wazuri tu
Kama wewe unahofia ndoa,basi usiniambukize hiyo hofu yako baki nayo mwenyewe mtuache sie ambao ndoa ndio msingi wa kujenga taasisi ya familia bora
Kwahiyo kwa hofu yoyote ambayo tumeaminishwa ipo na inasumbua jamii basi jitahidi usiwe sehemu ya hofu hiyo kwani hofu nyingine ni kwa watu dhaifu tu
Ni hayo tu!