Binadamu anapojiweka shetani anayegeuka kuwa Mungu kuutawala ulimwengu

Binadamu anapojiweka shetani anayegeuka kuwa Mungu kuutawala ulimwengu

KijanaHuru

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2017
Posts
1,822
Reaction score
2,320
Umofia Kwenu!

Nilipokuwa nikipitia baadhi ya stori za wadau mbalimbali nami nikahamasika kuweza kuandika walaka huu kwa kufuata mawazo na fikra zangu binafsi kuweza kuweka mbegu mpya au mtazamo mpya juu ya ulimwengu wetu huu tulionao.
Lakini zaidi ya yote nimevutaka kuandika waraka huu kutokana na kwamba katika upande huu watu wapo wengi zaidi wanaofuatilia kuangalia mawazo mbalimbali na mitazamo ya watu.

JItahidi kusoma Yote mpaka mwisho kabla haujaweza kutoa maoni yoyote.

Sasa wacha niende katika hoja moja kwa moja kama kichwa kilivyojielezea hapo juu.

Katika mazingira yetu ya dini zilizopo hapa duniani hasa ukiangazia katika hizi dini kuu mbili Ukristo pamoja na Uislam wamekuwa niwatu ambao wakitueleza kupitia maandiko au vitabu vitakatifu yakuwa ulimwengu unapokuja kuishia basi kuna yule shetani ama mpinga kristo ama dajali ama kama ilivyozoelekea 666 atakayekuja kutawala ulimwengu,
Nadharia na matukio mbalimbali yamekuwa yakiendelea duniani yakihusishwa kabisa kuwa ndio maandalizi halisi yakuweza kuja huyu mtawala muovu wa huu ulimwengu kwa siku za mwisho kabla ya kiama.

Katika kusoma vyema na kutafakari hivi vitabu vitakatifu niliweza kugundua jambo moja kubwa na lililoweza kufichika ambalo likaweza kunithibitishia kuwa haya mambo sio kweli bali ni mwanadamu tu ndiye anayeweza kuandaa huu uongo wake kwaa jili ya manufaa yake mwenyewe binafsi ambayo tunaweza tukayajua ama tusiyajue tukabakiwa na zile nadharilia zake tu.

Jambo la kwanza linalonithibitishia kuwa haya mambo ni ya uongo wala hakuna wakati yanaweza kuja kutokea kama vitabu vyao vya dini vinavyozungumzia nipale unakutana na neno moja kubwa na muhimu sana katika vitabu hivi hili neno linaitwa UNABII hili neno ndilo limeweza kubeba siri inayosemelea na kuthibitisha kuwa BINADAMU ANAPOJIWEKA SHETANI ANAYEGEUKA KUWA MUNGU KUUTAWALA ULIMWENGU.

Sasa angalia jambo la kushangaza na kutafakarisha juu ya unabii katika vitabu hivi vitakatifu, unabii ulikuwa unawekwa ama unatolewa kwa mambo makuu mawili.

1.Kukuandaa kuweza kulivuka au kulishinda jambo
2.Kutoa taarifa yakukabiliana na jambo

Ufafanuzi wa sehemu yakwanza, Kukuandaa kuweza kukabiliana na jambo hapa nikwamba Mungu alikuwa akiwaandaa binadamu kuweza kuvushwa katika majanga fulani yaliyokuwa yakitokea katika ulimwengu huu kwa kufanywa nayeye mwenyewe ama na muovu.
Mfano
Wakati wa Nuhu Mungu aliweza kumuandaa mwanadamu kumwokoa kwa njia ya safina, unabii ubatolewa dunia itaangamizwa kwa maji kisha lakini anatoa suluhisho kuwa wataokolewa wale watakao husika kujenga safina tu.
Hapa soma kwa utulivu sana uweze kuelewa hiyo sababu ya kwanza yaani Mungu anatoa jambo lakini anakupa na majibu pia namna gani utaokoka hapo.
Mfano wa pili pia angalia unaposoma habari za jamaa mmoja aliyekuwa akiishi katika miji pacha ya sodoma na gomora waliweza kupewa unabii wakuangamizwa lakini pia walipewa suluhisho lakumfanya mwanadamu yule kipenzi chake ama mtiifu aweze kuokoka na kutoka huko.
Hivyo alitoa unabii fulani lakini anakupa na njia ya kukabiliana nao.

Ufafanuzi wa sehemu ya pili, Kutoa taarifa kukabiliana na jambo hapa Mungu alikuwa anatoa hukumu zake hasa mtu akikosea nk yeye anatoa taarifa kuwa anakuangamiza sio kukuvusha kama kule mwanzo hapa anakumaliza kabisa kabisaa,
Mfano kuna jamaa anaitwa Yona huyu alotumwa aende ninawi kuwaambia watu kuwa maovu yao wanayoyafanya Mungu amesema anawaangamiza wote, sasa walipoweza kupata hii taarifa wale watu wa ninawi waliweza kuomba sana msamaha kwa huyu Mungu hadi Mungu akaweza kuwasamehe na kubatilisha hukumu yake.
Mfano wapili ni kwa Jamaa mmoja mfalme mbabe sana aliitwa Daudi huyu jamaa alipora mke wa mtu na kuua kabisa mume wake, Mwisho wa siku Mungu anatoa taarifa kuwa huyu Daudi atakufa lakini Daudi anaomba sana msamaha mwisho wa siku anakuja kusamehewa na maisha yanendelea.

Ukisoma visa vingi sana katika hivyo vitabu vitakatifu unakuja kuona kuwa Mungu alazima akupe njia ya kutokea ama anaweza kubatilisha maamuzi yake endapo mkifanya toba.

Sasa najiuliza kuwa kwanini kwa wakati huu wanalazimisha kutuaminisha kuwa nilazima huu unabii uweze kutimia? maana kumbuka bila kuwa na chapa inayosemwa hata ungekuwa mcha Mungu namna gani au unaupako kama wote ama umesoma nakuushika msahafu mzima bado utaishi kwa mateso sababu upo ulimwengu ambao hauendi sawa na Mungu wako na shetani ndiye mwenye Nguvu.

Kwa lugha rahisi nikwamba hakuna kuchomoka hata kama ukimwomba Mungu usiku na mchana,
Sasa kupitia haya nikaona kabisa hizi ni njama za watu kwasababu wanataka tukae domant tu tusiweze kujitetea bali tujiandae kukabiliana na kile wao wamekwisha kukiandaa kiweze kutudhuru sisi.

Kama Mungu muweza wa yote kwanini hatuwezi kuomba ili huyu 666 asiweze kuja?
sasa angalia ukimuweka Mungu pembeni ambavyo 666 haiwezi kuwa na nguvu hata kidogo.

Wanadamu tukiamua kusimama wote kwa umoja na kuzungumza wazo moja na kuwa na nia moja hakuna mfumo wowote unaoweza kutuangusha sababu hata hiyo mifumo inatutegemea sisi,
sasa kama kibinadamu tunaweza kuangusha utawala wowote pasipo Mungu kwanini sasa tunaaminishwa kuwa shetani ndiye anaharibu ulimwengu na wakati maovu yote yanafanywa na hawa hawa binadamu?
Hawa watu wa dini wanaweza kukwepa vipi kuwa wao sio waanzilishi wa hivi vitabu vyao ambavyo vinatulisha hizo propaganda kutuandaa kutawaliwa?

na sign out huo ndio mtazamo wangu kwa leo

pic1.jpg
 
Unvyoisi nikwanini Mungu alimuumba shetani.
ni nature jema lipo ili baya liwepo japo kwa wale wafia dini wao wanaamini shetani aliumbwa kama kiumbe mzuri baadaye akaja kuasi,
na maisha ya kiroho tunaamini kuwa Mungu na Shetani ni namna tu yakutofautisha nguvu zinazouendesha mfumo mzima wa ulimwengu pamoja na vitu vilivyomo ndani yake
 
Maelezo ni mengi lakini hayana maana..
Nikweli mkuu labda ingekuwa vema kuuliza pale ambapo hapajaeleweka na ukasaidiwa kueleweshwa,
maana hata usichoweza kukielewa siku zote hakina maana
 
Mkuu nakubali sana hoja na maarifa yako. Nakuomba uandike chichote kitu kwenye kukwaa la intelijesia. Ninapata shida sana sina maarifa kama yako. Nakuomba japo usome mada yangu ya 666 yaweza kuongezea maarifa yako. Usikae kimya sana. Na pia wajinga wamekuwa wengi sana ila tupo wachache wenye kukuelewa.
 
Unvyoisi nikwanini Mungu alimuumba shetani.

Kapipi shetani ni negative energy hajaumbwa alikuwepo tuu. Kila kitu kilikiwepo hakuna muumbaji.wala hakuna muumbaji bali tulikuwepo na kila mtu ana safari yake. Kuna nguvu moja inaitwa most high ndio mkuu. Kama
Kulikiwa na uumbaji watu wasinge zaliwa au shetani ukute nae alisha kufa miaka mingi wanadamu wanamlaumu shetani ila kila kitu kina muta wa ku expire huenda shetani alishakufa.
 
Kapipi shetani ni negative energy hajaumbwa alikuwepo tuu. Kila kitu kilikiwepo hakuna muumbaji.wala hakuna muumbaji bali tulikuwepo na kila mtu ana safari yake. Kuna nguvu moja inaitwa most high ndio mkuu. Kama
Kulikiwa na uumbaji watu wasinge zaliwa au shetani ukute nae alisha kufa miaka mingi wanadamu wanamlaumu shetani ila kila kitu kina muta wa ku expire huenda shetani alishakufa.
Most high ndio mkuu, umemaanisha Nini??
Mnachekesha nyie.[emoji23][emoji23]
 
Most high ndio mkuu, umemaanisha Nini??
Mnachekesha nyie.[emoji23][emoji23]

Unacheka unadhani mazuri embu jipatie reference kutoka kwa ndugu yako shetani pale aliposema ... I will ascend above the heights of the clouds, I will be like the Most High”' (Isaiah 14:12-14)
 
Back
Top Bottom