- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimesikia sehemu kuwa binadamu anaweza kupata usugu wa vimelea kutokana na kutumia mazao yatokanayo na wanyama mbalimbali, mfano wa mazao hayo ni nyama nk.
Hofu yangu ni kuwa wafugaji wengi siku hizi wamekuwa si waaminifu kabisa, wamekuwa wakitumia madawa hatari kwa ajili ya kukuzia haraka wanyama ili waingize sokoni, au wakati mwingine wamekuwa wakitumia madawa kwa ajili ya kuhifadhi mazao hayo ili yakae muda mrefu bila kuharibika.
Kumekuwepo cases nyingi za nguruwe na kuku kuchanganyiwa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI.
JamiiCheck.com naomba mniondoe wasiwasi huu maana tunakoelekea huko mbeleni ni hatari.
Hofu yangu ni kuwa wafugaji wengi siku hizi wamekuwa si waaminifu kabisa, wamekuwa wakitumia madawa hatari kwa ajili ya kukuzia haraka wanyama ili waingize sokoni, au wakati mwingine wamekuwa wakitumia madawa kwa ajili ya kuhifadhi mazao hayo ili yakae muda mrefu bila kuharibika.
Kumekuwepo cases nyingi za nguruwe na kuku kuchanganyiwa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI.
JamiiCheck.com naomba mniondoe wasiwasi huu maana tunakoelekea huko mbeleni ni hatari.
- Tunachokijua
- Tovuti ya umoja wa mataifa UN inaelezea hali ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa za kuua viini (AMR) kuwa hutokea wakati viini, virusi, kuvu na vimelea kuwa vimebadilika baada ya muda na haviwezi tena kutibika kwa dawa, hivyo kufanya maambukizi kuwa vigumu kutibika. Hii inaongeza hatari ya kuenea kwa ugonjwa, ugonjwa kuzidi kuwa mbaya na hata kifo.
Dawa za kuua viini vya magonjwa ni pamoja na antibayotiki, dawa za kupambana na virusi, dawa za kupambana na kuvu na dawa za kupambana na vimelea ni dawa zinazotumika kuzuia na kutibu maambukizi kwa binadamu, wanyama na mimea.
Kumekuwepo na madai kuwa matumizi ya mazao ya wanyama, ikiwemo nyama huweza kusababisha usugu wa vimelea kwa binadamu.
Uhalisia wa jambo hili ni upi?
JamiiCheck imepitia tafiti mbalimbali na kubaini kuwa ni kweli matumizi ya mazao ya wanyama huweza kusababisha usugu wa dawa dhidi ya vimelea kwa binadamu.
Kwa mujibu wa maktaba ya Taifa ya tiba ya nchini Marekani inaeleza kuwa Kutokana na matumizi ya dawa za binadamu, mfano Antibiotics kwa mifugo kwa lengo la kuongeza virutubisho kwa wanyama ili kusaidia wanyama hao kukua na kunenepa haraka, Ulaji wa mazao ya wanyama mfano nyama kunaweza kusababisha usugu wa vimelea kwa dawa kwani kupitia mazao ya wanyama hao ambapo vimelea sugu huweza kusafirishwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kutoka kwenye mazao hayo lakini pia hata taka za wanyama hubeba vimelea hivyo. Vimelea hivyo huweza kupelekea maambukizi yasiyotibika kwa muda mrefu na hata kusababisha kifo wakati mwingine.
Aidha tovuti ya Oxford Academy inaeleza kuwa chakula kitokanacho na wanyama waliotumia dawa za binadamu huweza kubeba vimelea hao sugu na kwenda kwa binadamu hatimaye kusababisha madhara kwa afya ya mtu, ambapo inapendekezwa kupikwa vizuri kwa chakula kitokanacho na wanyama ili kuua vimelea hao.
Kwa mujibu wa tovuti ya manispaa ya Lindi ambapo Afisa Habari wa Manispaa hiyo Pendo Mustapha akishirikiana na Afisa Afya Seif Abdallah humo waliandika baada ya kupata mafunzo yaliyotolewa na na serikali, FAO na USAID juu ya usugu wa vimelea vya magonjwa ya mifugo na binadamu kwa dawa kuwa usugu wa vimelea dhidi ya dawa kwa binadamu unaweza kusababishwa na Kula mazao ya mnyama yaliyotolewa bila kuzingatia muda wa kwisha dawa mwilini(Withdraw Period), ambapo pia matumizi ya dawa za binadamu kutibu wanyama, Matumizi ya dawa hususani antibayotiki kwenye chakula cha mifugo kwa ajili ya kunenepesha au kuharakisha ukuaji huweza kusababisha usugu wa vimelea.
Aidha shirika la afya duniani WHO linatoa tahadhari na kukataza matumizi ya antibiotics kwa wanyama kinyume na maelekezo ya wataalamu, ili kuzuia usugu wa vimelea kwa binadamu mara baada ya kutumia mazao ya wanyama wanaolishwa dawa hizo.
Aidha shirika hilo limerejea The Lancet Planetary Health ambao baada ya mapitio yao walibaini juhudi za kupambana na kuzuia matumizi ya dawa hizo kwa wanyama yalisaidia kwa asilimia 39% kupunguza vimelea sugu kwa wanyama.