Kuzeeka sio Ugonjwa... Kuzeeka kunapelekea mwili kushindwa kuimili magonjwa... Juwa kutofautisha kuzeeka na kupata magonjwa.
Hapa duniani hakuna kiumbe hai, narudia tena kiumbe hai kinachoweza kuishi milele.
Viumbe vyote hai vimekuwa programmed kufa. Seli zetu zote mwilini zimekuwa programmed kuishi kwa muda fulani baada ya hapo kwa sababu zinakuwa zimepunguza uwezo wa kutenda kazi kwa ufanisi. Na njia moja wapo ta kugundua seli za mwili wako zimeanza kufa, ni kuanza kuona mvi. Mvi ni taarifa ya kwamba seli ambazo zinatakiwa kuipa nywele rangi zimeanza kushindwa kufanya kazi au zimeanza kufa.
Sasa seli za mwili uwa zinaanza kufa kwa sababu ziko programmed kuishi kwa kipindi fulani tu, sasa umri unavyozidi kwenda ndipo seli zako nyingi uanza kufikia ukomo wa kujitengeneza kwa sababu zimekuwa programmed kuwa hivyo. Sasa zile ambazo zimetengenezwa zikaanza kufa zinakosa seli mbadala kwa sababu kiwanda cha kutengenezea seli nacho wafanyakazi wake nao wameanza kuzeeka na kufa. Hapo ndipo magonjwa yanaanza kukunyemelea uzeeni kwa sababu mwili umeanza kukosa wanajeshi wa kutosha kupambana na magonjwa... Ndio maana wazee wengi inakuwa rahisi kuumwa. Au muda mwingine viungo kama moyo, figo na viungo vingine ukosa nguvu kwa sababu seli hazina uwezo tena wa kuchapa kazi kutokana na zimeanza kubaki chache.
Kwa sasa bado hakuna teknolojia ya kufanya seli zisizeeke, sijasemq kufa, nimesema kuzeeka, kwa sababu kufa kuko palepale... Sana sana sayansi itazifanya seli ziweze kuishi muda mrefu tu na kumpeleka binadamu kuchelewa kuzeeka, lakini bado zitazeeka tu na kufa. Lakini Teknolojia ya robots inaweza kufanya mageuzi na akili za binaadam na ufahamu ukaamishiwa kwenye robots. Yani tukawa Cyborg.