Binadamu kujiita CHAWA ni Lugha ya Staha?

Binadamu kujiita CHAWA ni Lugha ya Staha?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Naona kwa sasa kila mtu " tegemezi" anajiita Chawa wa fulani

Kwa mfano nimetoka pale Chato nimewakuta Chawa wa Mbunge na ni cheo rasmi mtu anajitambulisha

Nimeshangaa Sana kwa sababu Chawa ni miongoni mwa Wadudu Wachafu kabisa

Zamani tukimuona Muhindi jambo la kwanza ni kuangalia Mayai ya Chawa kwenye nywele zake za kichwani 😂😂

Mlale Unono 😃
 
Kuna jina na hadhi.

Hiyo ya chawa ni hadhi, majina yao yanajulikana kwa kila mmoja.

Chawa pamoja na kuwa ni wadudu wasumbufu, lakini wanafaidi vinono kwa kunyonya damu ya boss wao. Na kwa kuwa Boss mwenyewe karidhia kunyonywa basi, ni burudani kwa Chawa. Ndiyo maana hawaoni soni kujitambulisha hadharani.
 
Unayajua maeneo ya binadamu ambayo CHAWA hupendelea kujivinjali kunyonya hiyo damu lakini?!!
 
images - 2023-07-26T225023.351.jpeg
 
Ni kiswahili kinakuwa ni sawa na mdada anavyojiita chura akimaanisha matako yaliyozidi ukubwa!
 
Aloooooooooo.
ingependeza kama uchawa ungewekewa kozi ukasomewe ikibidi hata degree yake iwepo maana naona ni jambo linaloshika hatamu kwa sasa.
 
Sijui kwa nini rais wetu ameruhusu na kukubali kuwepo na kikundi kinachojiita chawa wa mama?

Mbona walikua wanaweza kuwa na jina nzuri lisilo na ukakasi.

Wangejiita wazalendo wa mama isingependeza kwani.
 
Siasa zetu zinawafaidisha wanaojitoa ufahamu.

Hii ni parasitic symbiosis ambayo kwayo victim ni mwananchi wa kawaida. Huyo mwenye chawa anawategemea wananchi na hivyo hao chawa wananyonya damu yake ambayo inapata compensation from walalahoi.

Kwa hiyo, Hawa chawa wananyonya walalahoi indirectly. Hii ni tafsiri yangu kwa kutumia akili ya kawaida.
 
Back
Top Bottom