Binadamu mnashindwaje hata na jogoo?

Joannah

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2020
Posts
20,921
Reaction score
49,014
Jamani ndiyo tunamalizia wikiendi natumai mko poa.

Basi wikiendi ilivyoanza nikaona ni busara kwenda mtembelea bibi huko kijijini kwake Mwanzo Mgumu, nikapokelewa kwa kishindo. Basi bwana, bibi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji, nilipokuwa napumzika chini ya mwembe nikagundua jambo la kipekee kuhusu jogoo.

Jogoo akiona chakula kiwe kikubwa au kidogo hali hicho chakula, bali anamwita tetea kwa madaha aje ale halafu yeye anasindikizia sindikizia kishkaji. Sasa nyie binadamu mnakwama wapi kuiga mfano? Mmekuwa walalamishi, kila siku humu nyuzi mpya za kulalamika, hamtaki kulisha matetea wenu, mara muwaite ombaomba, mara sijui nini.

Wajameni igeni mfano bora wa jogoo jamani, halafu hana hata kisasi pamoja na tetea kula mwamba ye kidogo tu👍, binadamu sasa!

Jioni njema jamani.
 
Ndio ukaona uandike kama tetea kisa umemtamani Jogoo?

vp lakini ulifuata dawa za.mvuto kwa bibi au ulienda kumfunga mumeo akupende zaidi?
😁😁😁Kumfanya mtoto wa mama mkwe aweze kucheka na wewe zaidi ya miaka kumi sio kazi ndogo,ku update penzi kwa Bibi muhimu Sana kwa ustawi wa familia
 
Njoo nikulishe tetea wangu, achana na stories za jogoo sio real
 
Huyo jogoo anaweza kuwadunga wanne wakiwa wanaona na hawana wivu. Vipi we bibie unakubali ustaarabu wa mitetea ili ugawane na wanawake wenzio?
Mbona ndo tupo Kwenye Dunia ya namna hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…