Binadamu mwenye akili timamu hawezi kujitekenya kisha akacheka

Binadamu mwenye akili timamu hawezi kujitekenya kisha akacheka

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
4,555
Reaction score
4,758
Wasalaam.

Kitendo cha Serikali ya CCM kutunga sheria ya tozo za simu na kisha bunge la CCM kupitisha na mwenyekiti wa CCM kusaini na kuwa sheria kiliibua vilio nchi nzima. Lakini leo hii tunaambiwa mh mwenyekiti yule yule aliesaini amepunguza tozo ni jambo jema.

Swali ambalo nimekosa majibu ni je, mh mwenyekiti wakati anasaini hakusoma hii sheria? Je wabunge wa CCM wakati wanapitisha hii sheria, wakiongozwa na spika wao hawakuona km ingeumiza watanzania? Tunaelekea wapi?

Mola tunusuru waja wako ibariki tanzania maana CCM wanajitekenya na kucheka wenyewe taifa linakosa mwelekeo.
 
Wabunge Wakati wanapitisha Sheria walikuwa!

20210819_191521.jpg
 
Hapo haujaongelea bei ya mafuta kupanda na halafu serikali "sikivu" ikaingilia kati!!
 
Hii ndio maana halisi ya kutengeneza tatizo wewe mwenyewe (ccm) hao. wanalitatua wao wenyewe (ccm)

Halafu eti wanajipongeza wao wenyewe.

Huu ni upunguwani kupita kiasi
 
Bunge la chama kimoja shida yake ndiyo hii. Mawaziri na wabunge hawajiandai kwa kuwa hakuna challenge kwa masuala watakayo wasilisha ama kuongea hungeni.
 
Nchi haipigi MAENDELEO bila ya kubuniwa KODI MPYA NA TOZO MBALIMBALI.

Tujiandae na TOZO za YouTube na Amazon.

#NchiKwanza
#SiempreJMT
#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom