Binadamu na mitazamo yao, sisi na maisha yetu

Binadamu na mitazamo yao, sisi na maisha yetu

Amani Dimile

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
243
Reaction score
399
Jioni moja tulivu, siku ya tarehe 16 Mwezi wa 8 mwaka 1920 katika mji wa Andernach, Germany kilisikika kilio cha mtoto mdogo wa kiume ambae ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuja duniani. Mtoto huyo alikuja kuwa Mfasihi na mwandishi bora wa mashairi wa kiamerika na kujishindia tuzo mbali mbali za uandishi. Hapa simuongelei mtu mwingine yeyote yule, bali namuongelea 𝗖𝗵𝗮𝗿𝗹𝗲𝘀 𝗕𝘂𝗸𝗼𝘄𝘀𝗸𝗶 (apumzike kwa amani huko alipo).

Nilijitahid kadri ya uwezo wangu kusoma mashairi mbali mbali ya Bukowski, na moja kati ya vitu vilivyonivutia ni ile kauli yake aliyowahi kutamka akisema "kitabu kimoja kinachosomwa na watu elfu moja, kamwe hakiwezi kuwa na maana moja"

Ukiisoma haraka haraka hii kauli unaweza ukatoka kapa usielewe chochote kile, lakini Bukowski alimaanisha kwamba kila mwanadamu ana mtazamo wake tofauti juu ya kitu fulani, na mitazamo yetu ndio inayotufanya tutofautiane na hata kufarakana muda mwingine.

Ukweli ni kwamba, sisi binadamu huwa hatutazami vitu jinsi vilivyo bali huwa tunatazama vitu jinsi tulivyo, na ndio maana sote huishia kuwa na mitazamo tofauti.

Mitazamo ya wanadamu ndio inayowafanya watu waongee, wajione au waishi vile watakavyo. Mitazamo ya wanadamu ndio inayowafanya watu leo hii watutafsiri vile watakavyo wao hata kama ni kinyume na uhalisia wa maisha yetu.

Si ajabu sana kuona katika karne hii watu mbali mbali wakitusimanga, kutukosoa, kutukejeli, kutusengenya, kutuhukumu au hata kututukana sababu tu ya jinsi wanavyotutafsiri wao. Lakini kosa si letu, kosa ni mitazamo yao iwe ni ya kweli au ya uongo.

Mitazamo ya wanadamu imeathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya watu mbali mbali, wapo baadhi ya watu huishi kwa kuhofia kwamba binadamu watanionaje au watasemaje. Mitazamo ya wanadamu imewafanya watu wa karne hii wakose uhuru wa maisha yao maana huishi kwa kuogopa ni jinsi gani binadamu watawachukulia.

Hatuna budi kukubali kwamba tunaishi katika karne ambayo binadamu wengi wapo kutazama au kuyachunguza maisha yetu na wala si yao. Hiki ni kizazi ambacho kinajadili sana vitu kuliko kuvielewa jinsi vilivyo. Mara nyingi tunaishia kuonekana sisi ni wabaya, wakosefu, hatufai au hata wakaidi lakini la hasha yote ni kutokana na mitazamo ya watu wanaotuzunguka.

Ukweli ni kwamba huwezi kuendana na kila mtu (huwezi kuendana na mitazamo ya kila anaekutazama). Hapa sasa ndio uelewe ile kauli ya Bukowski kwamba wewe ni kama kitabu, na wanaokuzunguka ndio wasomaji hivyo kamwe hawawezi kuwa na maana au tafsiri moja juu yako.

Dale Carnegie, mwandishi wa kitabu cha 'How to win friends and influence people' anaeleza kwenye kitabu chake kwamba miaka 2200 kabla ya kuzaliwa Yesu palikuwa na mfalme aliyeitwa Akhtoi wa Misri, mfalme huyu alimuandikia mwanae ushauri. Ushauri ambao Carnegie anasema ulipaswa sana kusoma kwenye karne hii ..

Makala hii itaendelea ........ 36%

Ahsante kwa kunisikiliza naitwa Amani Dimile

InShot_20230313_124817510.jpg


Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom