Ni sababu zipi hizo na umejuaje zina-apply kwa kila mmoja wetu?
Ni kitu gani kimetuleta? Umejuaje?
Unajuaje wewe hutumiki kukamilisha mipango ya wengine?
Hehehe, introvert unanifurahisha. By the way na mi ni intovert wa ISFJ.
Haya turudi kwenye mada,
1. Sababu hizo unatakiwa uzijue wewe mwenyewe na sio mimi. Hata nikikwambia kuwa wewe inabidi
uachane na A na uanze kushughulika na B(ndiko mahala pako) bado jukumu la kuridhia litabaki kwako
wewe mwenyewe. Kuna watu wametajirika kwa vipaji vyao na kuna ambao wametajirika katika maeneo
ambayo hawana vipaji. Furaha ya watu hawa wawili ni tofauti kabisa, hata ufanisi wao haufanani kabisa.
Ukifanya kazi iliyo kuleta duniani kwanza utakuwa na furaha sana halafu vitu kama pesa, n.k havita kuwa
sababu ya msingi itayokufanya ubadili kazi hiyo. Hujawahi kuona mzazi anauza duka, watoto wake wanamfungulia
biashara kubwa lakini yeye anang'ang'ania kuuza duka ? Ni wa sababu anona pale ndio mahala pale.
2. Isingewezekana kila mtu awe ni bosi au mtawala hapa duniani. Nani angekuwa mtumwa? Hivyo basi hata kama mimi
nasaidia kutimiza malengo ya mtu mwingine, huwezi jua sababu hata ROCKET SCIENCE sio teknolojia ya mtu mmoja.
Kwa hiyo wengine wamekuja kukamilisha mambo ya watu wengine na ndiyo kazi iliyo waleta. Usiseme najicontradict!
Hapa simaanishi NASA wanakutumia sababu tu wanajua kichwani uko vizuri~ hapana. Bali ni ridhio lako wewe mwenyewe na ni moja ya ndoto zako kufanya kazi na NASA. Kwa lugha nyingine unafurahia na unakipaji kikubwa katika jukumu hilo.