thinky
JF-Expert Member
- Jan 13, 2014
- 2,121
- 264
Swali zima la "tunaishi ili iweje" lina assume kwamba kuna sababu za kila kitu kuelekea. Kitu ambacho si kweli.
mandate ya kupinga si kweli unaitoa wapi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Swali zima la "tunaishi ili iweje" lina assume kwamba kuna sababu za kila kitu kuelekea. Kitu ambacho si kweli.
Kila mtu kaletwa humu duniani kwa sababu maalum sema most of us tunashindwa kujua sababu zetu za kuja duniani, kila mtu ana kipaji chache tofauti na mwenzake kukitumia kipaji chako ukiwa duniani ndo sababu yako yakuishi duniani.
Hehehe, introvert unanifurahisha. By the way na mi ni intovert wa ISFJ.
Haya turudi kwenye mada,
1. Sababu hizo unatakiwa uzijue wewe mwenyewe na sio mimi. Hata nikikwambia kuwa wewe inabidi
uachane na A na uanze kushughulika na B(ndiko mahala pako) bado jukumu la kuridhia litabaki kwako
wewe mwenyewe. Kuna watu wametajirika kwa vipaji vyao na kuna ambao wametajirika katika maeneo
ambayo hawana vipaji. Furaha ya watu hawa wawili ni tofauti kabisa, hata ufanisi wao haufanani kabisa.
Ukifanya kazi iliyo kuleta duniani kwanza utakuwa na furaha sana halafu vitu kama pesa, n.k havita kuwa
sababu ya msingi itayokufanya ubadili kazi hiyo. Hujawahi kuona mzazi anauza duka, watoto wake wanamfungulia
biashara kubwa lakini yeye anang'ang'ania kuuza duka ? Ni wa sababu anona pale ndio mahala pale.
2. Isingewezekana kila mtu awe ni bosi au mtawala hapa duniani. Nani angekuwa mtumwa? Hivyo basi hata kama mimi
nasaidia kutimiza malengo ya mtu mwingine, huwezi jua sababu hata ROCKET SCIENCE sio teknolojia ya mtu mmoja.
Kwa hiyo wengine wamekuja kukamilisha mambo ya watu wengine na ndiyo kazi iliyo waleta. Usiseme najicontradict!
Hapa simaanishi NASA wanakutumia sababu tu wanajua kichwani uko vizuri~ hapana. Bali ni ridhio lako wewe mwenyewe na ni moja ya ndoto zako kufanya kazi na NASA. Kwa lugha nyingine unafurahia na unakipaji kikubwa katika jukumu hilo.
Mimi huwa nashangaa washika dini wanavyoogopa kifo wakati ndio wanasisitiza huko mbinguni ni kuzuri kuliko duniani.
Mtu kwenye ajali utasikia Yesu niokoe, Allah niepushe, sasa ya nini yote hio wakati mnaenda kuwa karibu na muumba sehemu yenye maziwa na asali na mabikra kadhaa?
Ingetakiwa muwe mna encourage kufa kama kweli mnaamini mbinguni kupo na ni kuzuri kuliko hapa.
Kwetu pazuri, nimepakumbuka... la mkifa vilioo!!
![]()
My sentiments exacly. Kwamba hakuna universal meaning and purpose. Mtu binafsi anaweza akaamua the meaning of life and purpose for his/her being here.. Na mtu anaweza pia kusema hakuna sababu yoyote ya kuwepo hapa.
This is where I fail to understand you.
Ukisema watu wameletwa kukamilisha jambo fulani, in a way, unamaana kwamba kuna some sort of design behind all this (universe and all)? Nikimaanisha yani kuna aliyewaleta ili waweze ku-serve a certain purpose. Je, nimekuelewa sawa?
Kwa sababu kama hiyo ndiyo maana yako, then it seems kuna a universal purpose for us humans being here. Hapa ndipo tunatopofautiana.
Mimi nikiona kwamba hii idea ya kuletwa ili kuserve purpose fulani ipo constructed na jamii husika kutokana na imani, mila na desturi za hiyo jamii. Therefore, this construct does not apply to everyone.
Leonardo da Vinci ana fit kwenye fikra zako introvert. Kwa maana ya kwamba ni mtu aliyeona anakipaji cha
kufanya chochote atakacho katika ustadi wa hali ya juu. Lakini si kila mtu ni multi talented. Natumia neno
kipaji/talent kwa maana ya uasili wa neno hilo. Umepewa uwezo fulani ambao ni distinct na unique. Sasa labda
wewe huamini kwenye swala la kipaji lakini kama unaamini basi itapaswa pia uamini kuwa hicho kipaji haujapewa
bure.Kuna sababu maalum za wewe kupewa au kuwa hicho kipaji. Sasa kwa jinsi ambavyo Introvert
unaongea ni kana kwamba kila mtu anaweza akafanya chochote kile kwa ustadi wa hali ya juu! na hii si
kweli. Kuna watu wana uwezo mkubwa katika eneo / maeneo fulani na hawajui kama wana uwezo huo.
Wanahangaika kujishughulisha na sehemu ambazo wanaowezo mdogo mno. Mimi nahimiza watu wa-unleash their potential. Otherwise LET US AGREE TO DISAGREE🙂🙂🙂.
Teh teh teh. Lakini huyo mungu kwanini aliandaa hayo maisha mengine nje ya dunia?
Tu duniani kusudi tumtumikie Mungu tupate kufika naye Mbinguni
maisha ni vita ya kiroho sisi ni wanajeshi kuna waasi na wazalendo tafuta ushindi BE A GREAT THINKER Cc [MENTION=106508]juve2012[/
Mmh.. Ebu tufafanulie tukusome vizur..!!
Mimi huwa nashangaa washika dini wanavyoogopa kifo wakati ndio wanasisitiza huko mbinguni ni kuzuri kuliko duniani.
Mtu kwenye ajali utasikia Yesu niokoe, Allah niepushe, sasa ya nini yote hio wakati mnaenda kuwa karibu na muumba sehemu yenye maziwa na asali na mabikra kadhaa?
Ingetakiwa muwe mna encourage kufa kama kweli mnaamini mbinguni kupo na ni kuzuri kuliko hapa.
Kwetu pazuri, nimepakumbuka... la mkifa vilioo!!
Tofauti yetu ni kwamba wewe unaongelea kipaji na uwezo wa mtu kufanya kitu fulani. Mimi naongelea tafsiri ya mtu juu ya maisha na dhumuni la uwepo wake hapa ulimwenguni. Hapo ndipo tunatofautiana.
Nakubali kwamba si kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kila kitu na sidhani kama kuna mtu wa namna hiyo.