Binadamu tunakula chakula kingi kuliko mahitaji ya mwili

Binadamu tunakula chakula kingi kuliko mahitaji ya mwili

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Hapo zamani za kale tuliishi kwa matunda an mizizi. Tulitembea umbali mrefu kutafuta mizizi an matunda haya. Mungu aliuwezesha mwili kuhifadhi chakula kwa njia ya mafuta. Hivyo ukikosa chakula kwa siku mbili au tatu mwili uliweza kutumia akiba kulisha ubongo na kuendeleza uhai.

Maendeleo ya zama za mawe an zama za vyuma yalituwezesha kuwinda na kulima nafaka pamoja an ile mizizi iliyokuwa inatafutwa porini kama mihogo, viazi, majimbi, nk.

Siku hizi vyakula vimekuwa vingi na tunavipata bila kutoka jasho. Ukweli ni kuwa ndizi moja mbivu inatosha kuwa kifungua kinywa. Mchana mayai mawili ya kuchemsha pamoja na nyanya an tango vinatosha kwa mlo wa mchana. Jioni vijiko vinne vya chakula na nusu mug ya maharage inatosha kwa mlo wa kulalia.

Huu no mlo wa wale wasiotumia nguvu nyingi kupata mkate wa kila siku.

Unaamka asubuhi unafungua fridge kuna mkate , mayai, sausage, unamaliza kula unaangalia tamthilia makes kesho kama kawa. Ni kukaribisha obesity
 
[emoji232] " tamu sana hii chakula ..nakula sana usiku ..ina protein.carbohydrate na lipid .. "[emoji124]
 
Umeelezea vyema dada ake ila shida ni kwamba tulio wengi tunaishi kwa kula kwa mazowea pasi kufuata utaratibu wa ulaji umekaa vipi.

Elimu inahitajika sana dada ili ile ya asubuhi supu na chapati, mchana ugali na samaki na usiku ubwabwa na maharage ipate kuisha.
 
Ubaya wa tumbo halisemagi basiiii unavyolizoesha na lenyewe linazoea!kuna jamaa mmoja mchimba mitaro yeye asubuhi anakula chapati 8 jagi la maarage na vikombe mama vi3 vya chai ukiona utajua hali tena mchana.ikifika mchana huwa hali hoteli anaenda nyumbani anajibonda ugali ndoo ndogo ile imejaa!siku unga wa ugali umebaki kilo4 anamwambia mkewe aupikie uji tu maana hawezi kushiba ukirushwa kwenye ugali.hapo dessert zake ni mihogo na karanga mbichi hizo ni mda wote anatafuna.appetize yaani kabla ya lunch ndo anakula wali sahani 3.
 
Kesho utakuja kulalamika hapa mumeo kaishiwa nguvu za kiume.
Sasa kwa menu hiyo walaah, hizo nguvu anatoa wapi? Akiweza kusimamisha tu, acha hata kupiga game moja, atakuwa na energy aisee
 
Ubaya wa tumbo halisemagi basiiii unavyolizoesha na lenyewe linazoea!kuna jamaa mmoja mchimba mitaro yeye asubuhi anakula chapati 8 jagi la maarage na vikombe mama vi3 vya chai ukiona utajua hali tena mchana.ikifika mchana huwa hali hoteli anaenda nyumbani anajibonda ugali ndoo ndogo ile imejaa!siku unga wa ugali umebaki kilo4 anamwambia mkewe aupikie uji tu maana hawezi kushiba ukirushwa kwenye ugali.hapo dessert zake ni mihogo na karanga mbichi hizo ni mda wote anatafuna.appetize yaani kabla ya lunch ndo anakula wali sahani 3.
Kazi ya kuchimba mitaro si utani muache afaidi
 
Umeelezea vyema dada ake ila shida ni kwamba tulio wengi tunaishi kwa kula kwa mazowea pasi kufuata utaratibu wa ulaji umekaa vipi.

Elimu inahitajika sana dada ili ile ya asubuhi supu na chapati, mchana ugali na samaki na usiku ubwabwa na maharage ipate kuisha.
Rafiki kile kitambi chako una mpango gani nacho?
 
Back
Top Bottom