Binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua

Binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua

Inaogofya sana!
Mkuu hii tabia ya kuamini kila kitu tuliletewa na wazungu itatufikisha pabaya maana kwa sasa ukizungumzia chochote juu ya mungu wanapuuza na kukimbilia kusema eti hakuna mungu hiyo tu ni imagination, imagination for what
 
Mkuu hii tabia ya kuamini kila kitu tuliletewa na wazungu itatufikisha pabaya maana kwa sasa ukizungumzia chochote juu ya mungu wanapuuza na kukimbilia kusema eti hakuna mungu hiyo tu ni imagination, imagination for what
Kama kumwamini huyo Mungu ninayemwamini kuna manufaa kwangu.......wala sihitaji siasa katika hilo, awe ameletwa na mzungu, ama mhindi, ama mjapan mimi hainihusu. Imani huja kwa kusikia! So walinifanya nisikie! Nawashukuru sana!
 
Ngoja nikueleze kitu kimoja ambacho ulikuwa hukijui labda na pia itategemea na akili na uwezo wako wa kufkiri. Ni hivi.

MUNGU ; Alipowaumba ADAM NA MKEWE aliwapa watoto wawili asubuhi na wawili jioni, kwa upeo wako ulivyo mdogo unaweza kuuliza mtu atazaaje asubuhi na jioni...?. Kwa MUNGU hilo ni jambo dogo tu kumbuka pia watu wa zamani si kama tulivyo sisi walikuwa tofauti sana na staki niende sana huko acha ni-stick kwenye mada yako.

Watoto waliozaliwa asubuhi ilikuwa hawaruhusiwi kuoana, isipokuwa wale wa jioni ndio ruksa kuoana nikimaanisha kwamba ; Asubuhi walipatikana mtoto we kike na wa kiume ambao hawakutakiwa kuoana na jioni hivyohivyo wawili, sasa huyu wa kiume wa asubuhi alitakiwa kumuoa wa kike wa jioni na vice-versa, hivyo kulikuwa na KABIL NA HABIL.

HABIL alikuwa ni mwenye sura nzuri ila dadake alikuwa ni mwenye sura mbaya na KABIL alikuwa na sura mbaya ila dada'ke alikuwa ni mzuri wa sura.

HABIL akamwambia itabidi nimuoe dada'ko na wee umuoe dada'ngu HABIL anamwambia KABIL mwenye sura mbaya KABIL akakataa katakata siwezi kukupa dada'ngu ana sura nzuri kisha unipe dada'ko mwenye sura mbaya. Huyu ntamuoa mwenyewe na wee muoe dada'ko mwenye sura mbaya.

HABIL akamwambia sheria haituruhusu mutants hivyo ni HARAM tutatenda dhambi, KABIL hakutaka kuelewa hata kidogo na ugomvi ukaanzia hapo ndipo KABIL akafkia hatua ya kumuua nduguye sababu ilikuwa ni mwanamke, sasa wee hukutueleza sababu ya Luis ilikuwa ni nini labda...?.

Ahsanta.
Sasa ndio umeandika nini? Kweli ifike mahali hizi dini zipotee tu maana watu hawana akili kabisa! Sifuri kubwa imekukaa kichwani
 
Binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua aliishi Mabibo Beach.....wafia dini acheni upotoshaji
 
kwani kaini aliwekewa alama ili asiuliwe na wakina nani

Kumbuka hawa hawakuuana wakiwa watoto bali watu wazima kwa hiyo kwa kipindi wao wanakua na binadamu walikuwa wanazidi kuongezeka kupitia kwa wazazi wao yaani Adam na Hawa na hata ukisoma maandiko matakatifu yanaeleza kwamba Adam na Hawa waliendelea kuzaa watoto wengine na kadri walivyokuwa wanazaa ndivyo kizazi kilizidi kukua kwa hiyo walikuwa na watoto wengine ukiacha Kaini na Habili ila mm nilichomaanisha ni kuwa binadamu wa kwanza kuzaliwa ni Kaini na baadaye nduguye Habili akazaliwa na ni huyuhuyu Kaini aliyekuwa binadamu wa kwanza kuua baada ya kumuua nduguye Habili na kuhusu alitengwa ili asiuliwe na akina nani ni kuwa kipindi yeye na nduguye kaini wanakua pia watu walikuwa wanaongezeka kupitia adam na hawa na kipindi kaini anamuua ndugu yake tayari watu walikuwa wameshaongezeka.

Kwa Maelezo zaidi soma kitabu cha mwanzo kimeelezea kila kitu kwa undani
 
Sasa ndio umeandika nini? Kweli ifike mahali hizi dini zipotee tu maana watu hawana akili kabisa! Sifuri kubwa imekukaa kichwani

Endelea na meditation upae ndugu huwezi kuelewa kwa upeo ulionao.

Kila la heri.
 
kwani kaini aliwekewa alama ili asiuliwe na wakina nani
mbaya zaidi mungu wake alimwahidi kuwa atakaemuua KAINI ,atapewa adhabu mara saba,


lameki babake na Noah,ndiye aliemuua kaini,na adhabu mpaka leo hajapewa
 
Endelea na meditation upae ndugu huwezi kuelewa kwa upeo ulionao.

Kila la heri.
Kwahiyo mwanamke mmoja alikuwa anazaa watoto wawili wawili asubuhi na jioni?

Huko madrassa ndio mnafunzwa haya au ni makanisani? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Duh ! Kwa majibu yaliyotolewa hapa, inaonyesha dhahiri watu wanaomwamini Mwenyezi Mungu idadi inazidi kuporomoka kwa kasi. Hatari kubwa hii.

Waamini wa Mungu wengi tuko Africa huku ila uko kwa wenzetu idadi inazidi kuporomoka
 
3f0a8d625e7eb4cf29100f87e9066697.jpg

Ukiachana na wanasayansi wanaotudanganya kila kukicha juu ya chimbuko la binadamu neno la Mungu linatueleza kwa kinagaubaga chimbuko la binadamu pamoja na viumbe hai wengine namna walivyoumbwa na mwenyezi Mungu kwa hiyo viumbe hai vyote na visivyo hai vimeumbwa na mwenyezi Mungu.

Hebu leo basi tuangalie juu ya binadamu wa kwanza kabisa kuzaliwa na kuua. kadiri ya kitabu cha mwanzo (Bibilia) katika agano la kale baada ya Adam na mkewe Hawa kula tunda la kati walilokatazwa na Mungu, Mungu aliwatoa katika bustani ya Eden na kuwaamuru wakazae ili waijaze dunia.

Katika kitabu cha mwanzo kinaeleza baada ya Adam na Hawa kufukuzwa kwenye bustani ya Eden, Adam akamjua mkewe na wakapata mtoto wa kwanza KAINI na baadaye wakazaa mtoto mwingine kwa jina HABILI ambao hawa ndo wana wa kwanza wa Adam na Hawa na hawa Kaini na Habili walitunza imani yao kwa Mungu wakamtolea sadaka.

Habili alitoa sadaka yake kwa Mungu katika wanyama bora wa kundi lake akiwa na hali ya unyenyekevu na imani naye Mungu akampokea. Tabia ya Kaini ilikuwa ya kiburi bila ya kumcha Mungu, kwa hiyo Mungu alimkataa (mwanzo 4:1-5, soma ebr 11:4, 1yoh 3:12). Tabia na maisha ya watoaji wa sadaka ina maana kuliko vitu wanavyovitoa, kwa hiyo Mungu alimwambia Kaini kuwa akitaka Mungu ampokee angepaswa kushinda dhambi iliyokuwa ikitaka kumwangamiza. Dhambi hiyo ilikuwa kama mnyama wa mwitu ajikunjaye na kuotea mlangoni ili aweze kumshambulia mtu akitoka nje (mwanzo 4:6-7). Kaini hakushinda dhambi yake na katika hasira na wivu alimuua nduguye Habili.

Tendo lake la kutwaa uzima na ndugu yake ilidai kisasi kwa Mungu aliyetoa uhai ule, kwa hiyo Mungu alimfukuza Kaini aende mbali na mahali walipoishi watu wengine. Ingawa Kaini alidumu katika hali ya kutotubu Mungu katika huruma yake kubwa alimlinda asiuwawe kwa kisasi (mwanzo 4:8-16). Kwa hiyo katika maandiko matakatifu KAINI ndiye binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua baada ya kumuua nduguye HABILI.

God bless you
Ndugu Yangu, haya yote nakubaliana na we we. Kwani na Mimi ni mfuasi Wa Yesu Wa Nazareth.
Nipo ktk safari ya kuelekea mbinguni.

Lakini Nina swali hapa, la kimaandiko.
Kaini ndie alie muua Abel, sawa.

Sasa basi kaini alipata watoto, alizaa na nani? Na wakati huo dunia ina watu watatu?
 
Kwahiyo mwanamke mmoja alikuwa anazaa watoto wawili wawili asubuhi na jioni?

Huko madrassa ndio mnafunzwa haya au ni makanisani? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Ndio maana nakwambia kwa upeo ulionao huwezi kuelewa coz upeo wako ni mdogo sana hata nikueleweshe vipi.

Kazana na meditation kwanza uweze kupaa ukishaweza hilo kidooogo ntakuona ume-advance lakini kwa sasa bado mchanga sana hujakomaa.
 
Ndugu Yangu, haya yote nakubaliana na we we. Kwani na Mimi ni mfuasi Wa Yesu Wa Nazareth.
Nipo ktk safari ya kuelekea mbinguni.

Lakini Nina swali hapa, la kimaandiko.
Kaini ndie alie muua Abel, sawa.

Sasa basi kaini alipata watoto, alizaa na nani? Na wakati huo dunia ina watu watatu?
Hili swali tayari nimeshalijibu kwa hiyo tafuta moja kati ya comment zangu utaliona hilo jibu
 
Hivi ni nani angemuua kwa kisasi ? Maana walikuwa wawili tu Kaini na kaka yake Habil ,waliobaki ni wazazi wao ,
 
Hapana, anaandika kile anacho kiamini.
Wabongo tumekuwa watu wa ajabu kwa kuamini kila kitu tumeletewa na wazungu na ninaamini hata leo akitokea mzungu halafu aseme wao ndo walileta waafrika kuna waafrika wengi watakaomsapoti yaani tupo pabaya mno kwa kuendelea kujazwa ujinga na hawa wazungu na kuwaamini inashangaza eti mtu kusema kuwa hakuna mungu eti ni imagination tu yaani daah poleni sana waafrika
 
Back
Top Bottom