Haendi kwenye majukumu yake?Hata ukiletewa usafiri wa kwenda na kurudi
Hujanielewa..Majukumu gani kwenda kusikiliza nini kipya
Nilimjibu aliyesema wakikufata na V8. Nikamuuliza ukienda huko kuwasikiliza nani atafanya majukumu yako ya kutafuta mkate wa siku..Majukumu gani kwenda kusikiliza nini kipya
Unaenda kusikiliza jambo gani jipya?Tupo pamoja.
Kuna mahali leo nilipita kulikuwa na mkutano wa kampeni za mgombea ubunge wa mboga mboga, yaani watu hata 100 hawafiki. Nikajisemea "no wonder bi tozo wanamsombea watu"πββοΈπββοΈπββοΈ
Sawa sio lazima kuhudhuria kampeni ila ni muhimu siku ya kupiga kura, nenda ukatiki, ili kuhalalisha mshahara unaomlipa. Hata isipomchagua, atachaguliwa na wengine, lakini wewe ni lazima umlipe mshahara wake!.Mimi binafsi siwezi kutoka kwenda kusikiliza Mgombea yoyote yule. Naona hakuna jipya wanaloweza kunieleza nikawaelewa. Miaka yote ya uhuru matatizo ni yale yale ambayo yameshidwa kutatulika.
Kama tu nchi yenye watu milion 65 tumeshidwa kuendesha mradi tu mdogo wa mwendo kasi. Hapo naweza kutoka kwenda kusikiliza nini kwa mfano.
Hata wakija kunifuata na V8 zao na pesa juu nitawambia nashukuru ila siwezi kutoka siwezi kwenda kusikiliza watu ambao kabisa naona nawashinda akili kiufupi.