Katika ukristu, funga ni SIRI
View attachment 3269499
Ila tusiwanyime waislamu maua yao. Wapo serious na mfungo kuliko wakristu ndio maana wanapoanza kufunga, impact inaonekana kwa uharaka..
Allaah ametuagiza tuwaambieni hivi :
"{ قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ }
Sema: Enyi makafiri!
{ لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ }
Siabudu mnacho kiabudu;
{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ }
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
{ وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ }
Wala sitaabudu mnacho abudu.
{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ }
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
{ لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ }
NYINYI MNA DINI YENU NA MIMI NINA DINI YANGU. .
--mwisho wa kunukuu--
Kwanini mnataka tufanane?!
Nyinyi mna dini yenu na sisi tuna dini yetu!
Nyinyi mna ibada zenu na sisi tuna ibada zetu!
Nyinyi mna sala zenu na sisi tuna swala zetu!
Nyinyi mna zaka na sadaka zenu na sisi tuna zaka na swadaqa zetu!
Nyinyi mna funga zenu na sisi tuna swaumu zetu!
Nyinyi mna hija zenu na sisi tuna hija na Umra zetu!
Msilazimishe tufanane wakati dini zetu ni tafauti na hivyo swala zetu haziwezi kufanana na sala zenu!
Zaka na swadaqa zetu haziwezi fanana na zaka na sadaka zenu!
Swaumu zetu haziwezi fanana na funga zenu?
Hija zetu haziwezi fanana na hija zenu!.
Sisi tunafanya ibada kulingana na tulivyofundishwa na mtume صلى الله عليه وآله وسلم wala hatuigi dini ya mtu yeyote kwa sababu
NYINYI MNA DINI YENU NA SISI TUNA DINI YETU katu! Ibada za kiislamu haziwezi fanana na ibada za dini yoyote nyingine.
Sasa kama mnaona nyinyi ndio mnafunga sawasawa endeleeni hivyohivyo na sisi tunafunga kulingana na tulivyofundishwa na mtume wetu
صلى الله عليه وآله وسلم.
Lakini mwisho nawauliza tena swali ambalo hamtaki kulijibu.
Yesu alifunga siku arobaini usiku na mchana!
Nyinyi ni shetani gani aliwafindisha kufunga mchana na kula usiku?!
Andiko la kuruhusiwa kula usiku mumefundishwa na nani?!
Kwanini mnashindwa kumuiga bwana yesu au imani zenu ni ndogo ?!