Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo kipindi hiki cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu

Asilimia 90 ya wanaochangia huu uzi wala hawafungi..

Acheni unafki.
 
Tatizo unafananisha chaki na chizi, huenda vikafanana kimuonekano (zote zinaitwa ni funga) lakini ni vitu viwili tofauti.
Naomba kupata muongozo wa funga ya Kwaresma, kwani funga ya waislamu ni kutokula na kutokunywa na kujizuia na matamanio ya nafsi kuanzia Alfajiri mpaka kwa kuzama kwa jua.
 

Ukitaka kujua kwamba watu (dhehebu flani) wamefunga angalia matendo yao- hata kama hawajasema
kama watakuwa wamefunga kimya kimya lakini kila kitu kipo vile vile jua tu kuwa kuna kitu hakipo sawa

Waislam wakifunga kila kitu hadi wanyama wafungwao wanaona utofauti, sijaongelea Ombaomba, mayatima, wagonjwa mahospitali, ukarimu kwa wahitaji unaongezeka x 10; wakikuuzia kitu unapata ulichotaka (genuine) na hakuna kupunja kwa namna yoyote ile. Hata wakinyamaza kimya, MTAJUA TU!..... Kimsingi Funga ya kiislam inamisingi yake inayo ambatana na kutokula na kunywa.

Uamuzi ni wako.....
 
Nimezungumzia kwaresma boss na nimewapongeza wakristo Kwa Utaratibu wao mzuri na WA kuigwa,vipi Kuna shida hapo boss wangu?
 
Nimezungumzia Funga ya wakristo na kwaresma,hakuna mahala nimetaja dini nyingine tafadhali wewe ndo unafananisha boss
 


Ni maagizo ya Bwana wetu Yesu Krisyto kuwa mfungapo mfanye kwa siri baina yako na Mungu wangu. Usifunge kwa kutafuta sifa kama wafanyavyo wanafiki. Ukifunga, haifakiwi utangaze kwa yeyote, bali Mungu wako ndiye anaijua dhamira yako.

Math 6:

Matayo 6
16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao.
17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu 18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.”​

 
Mfungo ni tendo la kiimani na la kibinfasi sana
 
Sijui kwa nini nikimuona mtu anahangaisha akili juu ya hizi imani huwa namdharau.

Kwani ukisimama unapopaamini wewe na kuheshimu wengine hata kama unawaona hawapo sahihi utapungukiwa nini?

#HebuMkue.
Ni vibaya kuwapongeza wengine pale unapoona wanafanya vizuri?
 
Isaya 58:6-8 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? (7) Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako, kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao, kuwavalisha wasio na nguo, bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu. (8) Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na uponyaji wako utatokea punde; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
tunza tiketi yako derby ipo palepale hakuna kupewa point 3 za mezani lazma uzitolee jasho
 
Ahsante sana,nazidi kujifunza
 
Mfungo ni tendo la kiimani na la kibinfasi sana
Matayo 6
16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao.
17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu 18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.”
 
Nyinyi huwa mnatafuta nini kwenda kuwachungulia na kuwapeleleza waislamu wanavyofuturu?!
Si muangalie mambo ya ugalatia wenu ?!
Kwanini mfatilie futari na daku za waislamu?! Kama sio umbea na viherehere ni nini?!
c huwa wanajianika mabarazani na kando kando ya njia wakati wa kula kujionyesha walifunga
 
Kufuturu pamoja ni jambi jema naona ndugu yako analia lia hapo hata viongozi wa kikristo wanakuja kujumuika ni utaratibu mzuri ..Pia, ni sehemu muhimu ya kuwakumbuka wenye uhitaji.
Mkuu, ni wapi nimelia lia? Kwenye Uzi wangu nimezungumzia kwaresma pekee na sijagusia dini nyingine,hivyo kupongezwa upande mmoja haikumaanisha kwamba upande mwingine uko wrong ila Kwa jinsi mnavyokuja moto hii inaleta mashaka ni kama nimetupa jiwe gizani hivi
 
Sasa kama mtu anafunga
BIA,
WALI
NYAMACHOMA
ENERGY DRINKS
halafu mchana huo ANAKULA
UGALI,
MAHARAGE NA SAMAKI
atahangaikaje na futuru ya jioni?
 
Shida Iko wapi mkuu kwenye huu Uzi wangu wa kuwapongeza Wacha MUNGU?
Mcha Mungu alikuwa Yesu ndiye aliyeweza kumshinda shetani katika funga yake, alifunga siku 40 usiku na mchana bila ya kula chochote akiwa nyikani na kujaribiwa na shetani kwa vishawishi tofauti, soma (Mathayo 4:1-11, Marko 1:12-13, and Luka 4:1-13). Kama wanaojiita ni wafuasi wa Yesu kweli wangefunga funga aliyoifunga Yesu, wangekuwa ndiyo mfano pekee wa ucha Mungu, kwani imeandikwa katika Mathayo 11:29-30 Yesu anasema "Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…