Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo kipindi hiki cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu

Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo kipindi hiki cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu

Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo wa madhehebu yote yanayofunga kipindi hiki Cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu.

Sijasikia mkristo yeyote akijisifu utakatifu Kwa kufunga kwake.

Sijaona wakristo wakizuia wengine kula hadharani Wala kuonesha kuchukizwa na Hilo

Sijaona wakristo wakihangaika na vikombe vya uji Wala sahani za magimbi muda wa kufuturu.

Sijasikia wakristo wakipiga kelele alfajiri kwamba wanakula chakula Ili waweze kuvumilia njaa ya mchana kutwa Hadi muda wa kufuturu.

Sijaona vijana wa kikristo wakihangaika kwenda kula chakula kanisani kipindi hiki Cha mfungo wao.

Nimechunguza mengi Kwa wakristo na nimegundua wanafanya mambo Yao kiungwana bila kubugudhi wengine.

Nimeambiwa wakristo wanafunga siku arobaini na mwisho wa kula au kunywa ni saa 5 dakika 59 usiku baada ya hapo mkristo hatakiwi kula Wala kunywa ila wanaruhusiwa kusafisha kinywa Kwa mswaki na maji,na kuoga pia.

Hongera sana wakristo,BWANA wenu awabariki nyote katika mfungo wenu na iweni na kwaresma njema
Hiyo ndiyo funga ya kweli, funga ni baina yako na Muumba wako.
 
Mimi najiuliza sasa kama unafunga usiku usiku unaamka kushindilia Ugali ya Nini?

Alafu Unashinda unajisifu Umefunga kweli?

Alafu najiuliza kwa Nini bei za vitu zinapanda kipindi cha mfungo wa ramadhani?

Utagundua wafanyabiashara waligundua kwamba bidhaa za vyakula utumika sana kipindi hicho.

Sasa kama tunafunga kwa Nini jioni misufuria machakula kibao ya Nini kama sio ulafitu. Yaani jioni ukakula na unafidia chai ya Asubui + CHAKULA cha mchana = hakuna funga hapo.

Mtume Alikua mwadilifu sana na Aliweka vizuri sana maana ya funga, unajinyima ili sehemu ya fedha uwasaidie waitaji.
Kwani wewe hao wanaofunga unajua utaratibu wa funga yao ukoje? Mbona kama unataka kuwapangia vya kufanya!

huwa unaingia kwenye nyumba zao usiku na kuona wanavyohangaika na masufuria ya ugali?

Hivi unajua kwanini wanavyofungua wanapendelea kutumia uji? Duu, we mkuu ni noma unateswa hadi na uji,hatari mwanawane!

Je,wewe huwa una funga? Kama unafunga,huwa unafunga usiku au mchana?

Hivi unajua maana ya kujisifu? Nani aliyejisifia kwako kuwa yeye kafunga?

Yaani hadi bei za vyakula unazihusisha na mfungo wa watu,kweli we kiboko! Kwahio waliopandisha bei za vyakula ni wepi,wa ramadhani au wa kwaresma? Maana wote wamefunga mwezi huu?

Vipi funga zingeangukia mwezi wa sita unafikiri bei za vyakula bado zingekua juu?

Unaonekana unateseka sana na masufuria ya kwenye nyumba za watu kuliko masufuria ya nyumbani kwako,nakosea mkuu kuwaza hivo?

Hivi kuna funga ya kufunga usiku? Maana ni kama unakereka na watu kufunga mchana na kula usiku!

Hivi huwa unalala na kuamka kula usiku? Vipi ukifanya hivyo chakula huwa kinalika(kinashuka) sawa na wakati wa mchana?

Wewe ulitaka watu wafungaje ili wawe wamefunga kwa mtazamo wako? maana waliofunga wewe huoni kama wamefunga,unaona tu masufuria na vikombe vya uji!

Kikubwa kuheshimiana tu,kubeza na kukejeli imani ya mwingine haikufanyi wewe kuwa bora,bali muda mwingine inakufunua na kukuonesha wewe ni mtu mwenye akili na roho ya namna gani.
 
Katika ukristu, funga ni SIRI
View attachment 3269499


Ila tusiwanyime waislamu maua yao. Wapo serious na mfungo kuliko wakristu ndio maana wanapoanza kufunga, impact inaonekana kwa uharaka..
kutana na mfuasi wa mudi mnamo saa sita mchana domo limepauka akihema hali inabadilika kinywa kimechacha mda wote anawaza kwenda kugonga komwe chini apate alama nyeusi dah tuna safari ndeu sana
 
Asante sana.sifa na utukufu ni Kwa Mungu.

Tena aliyekwambua sie mwisho kula sa tano usiku kakudanganya, hakuna mkristo anaefunga anakula usiku huo
Tukishafungua sa kumi na mbili wachache wanakula sa mbili kidogo basi mpk kesho tena
Swali moja tu la msingi na muhimu sana kupatiwa jawabu sahihi!
Aloyewawekea utaratibu huo wa kufunga ni nani?!
Ni andiko gani linalowaambia kuwa mfungue saa kumi na mbili?
Ni andiko gani linalowakataza mkishafungua msile Tena hadi kesho?!
Kwamfano upande wetu Allaah katuruhusu kula usiku mzima hadi ikifika alfajiri ndio tuache kula na kuanza kufunga.!
Allaah anasema katika suuratul Baqara Aya ya 187 ya kwamba :
"{ ...................وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ ٱلۡخَيۡطُ ٱلۡأَبۡيَضُ مِنَ ٱلۡخَيۡطِ ٱلۡأَسۡوَدِ مِنَ ٱلۡفَجۡرِۖ ثُمَّ أَتِمُّواْ ٱلصِّيَامَ إِلَى ٱلَّيۡلِۚ.................. }
...................Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku........... "
Na usiku kisheria unaanza baada ya kuzama jua na sio saa kumi na mbili.
Saa kumi na mbili kwa mikoa ya Kagera, Kigoma na Rukwa bado ni mchana kabisa.
Na kuhusu daku tumeamrishwa na mtume Muhammad
صلى الله عليه وآله وسلم
katika hadithi aliyopokea Imamu Bukhari na Muslim toka kwa Swahaba Anas bin Maalik kwamba mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema:
" تَسَحَّرُوا ؛ فَإِنَّ فِي السُّحُورِ بَرَكَةً ".
" KULENI DAKU, KWA HAKIKA NDANI YA KULA DAKU KUNA BARAKA"
Kutokana na hadithi hii inakuwa ni Sunna muislamu kutamka mwisho wa usiku na kula angalau tende tatu, au funda la maji , na mtu anayetaka kula na kushiba anaruhusiwa kutokana na aya niliyoitaja hapo juu.
Na sisi tunapofuata maelekezo haya ya Allaah na mtume wake huwa hatujali wakristo na wapagani wanatuonaje au wanasema nini dhidi yetu kwa sababu SISI TUNA DINI YETU NA WAO WANA DINI ZAO.
(Kwanini mnataka ibada zetu zifanane wakati dini zetu ni tafauti?!
Kwa kumalizia nitaje ya kwamba Allaah alishatuambia ya kwamba hata tufanye nini wayahudi na wakristo hawatapata raha na sisi hadi yitakapoingia kwenye dini yao.
Allaah kalibainisha hili ndani ya Suuratul Baqara Aya ya 120 kwa kusema:
" { وَلَن تَرۡضَىٰ عَنكَ ٱلۡيَهُودُ وَلَا ٱلنَّصَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمۡۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۗ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم بَعۡدَ ٱلَّذِي جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ }
Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu".
 
Funga ya mtu haipaswi kukera wengine.
Ile mijamaa miroho sana
Waroho kwani wamekuja kuomba chakula nyumbani kwenu?!
Chakula wamenunua wenyewe! Wamekula wenyewe!
Wewe unaumia watu wakila kisa hujaalikwa kufuturu nao!
Unadhani ungealikwa kama walivyoalikwa hawa masista wa kikatoliki hapa chini ungrkaa na kupiga kelele kuwa waislamu wanakula sana?!
Hebu cheki hapa chini wakristo wanaojua kuwa waislamu ni ndugu zao wakishiriki na waislamu kufuturu!
 

Attachments

  • images(28) (1).jpg
    images(28) (1).jpg
    64.4 KB · Views: 1
  • images(26) (2).jpg
    images(26) (2).jpg
    41.3 KB · Views: 1
Ongezea na hii.... Hakuna kufatiliana kama umefunga kwani kufunga ni kati ya mtu na Mungu na siyo kuwindana nani anakula ili kuchapana viboko na kupeana majina ya ajabu ajabu.
Kati ya misingi muhimu sana ya dini ya kiislamu ni kuamrisha mema na kukataza mabaya:
Allaah ameamrisha jambo hili kwa kusema kati Suurat Aalu Imrani Aya ya 104 ya kwamba:.

{ وَلۡتَكُن مِّنكُمۡ أُمَّةٞ يَدۡعُونَ إِلَى ٱلۡخَيۡرِ وَيَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ }
Na liwepo miongoni mwenu kundi (ambalo) linalingania katika kheri na linaamrisha mema na linakataza mabaya.
Na hao ndio walio fanikiwa.

Na katika sura hiyohiyo aya ya 110 Allaah akasema:

{ كُنتُمۡ خَيۡرَ أُمَّةٍ أُخۡرِجَتۡ لِلنَّاسِ تَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَتَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَتُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِۗ
Nyinyi mmekuwa umma bora walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu".

Na mtume Muhammad
صلى الله عليه وآله وسلم
anasema katika hadithi aliyoipokea Imamu Muslim kutoka kwa swahaba Abuu Sai'yd Al khudry
رضي الله عنه.
Mtume amesema:

" مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ ".
Atakayeona miongoni mwenu jambo ovu na alizuie kwa mkono wake, kama hawezi basi ( alikataze ) kwa ulimi wake , na kama hawezi basi ( alichukie ) kwa moyo wake na huyo ni mdhaifu mno wa imani"

Sasa Allaah ameamrisha waislamu wote ambao hawana dharura za kisheria wafunge mwezi wa Ramadhani pale aliposema katika Suuratul Baqara Aya ya 183 ya kwamba :

{ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ }
"Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, ( mumefaradhishiwa kufunga )
kama waliyo andikiwa (walivyofaradhishiwa ) walio kuwa kabla yenu ili mpate kumchamungu."

Na katika Aya ya 185 Allaah akasema:

" { شَهۡرُ رَمَضَانَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ فِيهِ ٱلۡقُرۡءَانُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَٰتٖ مِّنَ ٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡفُرۡقَانِۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ ٱلشَّهۡرَ فَلۡيَصُمۡهُۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٖ فَعِدَّةٞ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَۗ يُرِيدُ ٱللَّهُ بِكُمُ ٱلۡيُسۡرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ ٱلۡعُسۡرَ وَلِتُكۡمِلُواْ ٱلۡعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ }

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo (ndani yake ) Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru."

Kwakuwa Allaah kaamrisha waislamu wasiokuwa na dharura za kisheria kufunga, basi ni dhambi na maasi kwa mwislamu asiyekuwa na dharura kula mchana wa Ramadhani na anapoonekana akifanya hivyo katika jamii ya waislamu wengi lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.!
Ama wakristo na wapagani hakuna mahala wamekatazwa kula kwakuwa tukifanya hivyo hata mbwa, nguruwe,paka ,mbuzi na ng'ombe tutawalazimisha kufunga wakati wao Allaah hajawawekea sheria ya kufunga.
 
Allaah ametuagiza tuwaambieni hivi :
"{ قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ }

Sema: Enyi makafiri!

{ لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ }
Siabudu mnacho kiabudu;

{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ }
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.

{ وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ }

Wala sitaabudu mnacho abudu.

{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ }
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.

{ لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ }

NYINYI MNA DINI YENU NA MIMI NINA DINI YANGU. .

--mwisho wa kunukuu--

Kwanini mnataka tufanane?!
Nyinyi mna dini yenu na sisi tuna dini yetu!
Nyinyi mna ibada zenu na sisi tuna ibada zetu!
Nyinyi mna sala zenu na sisi tuna swala zetu!
Nyinyi mna zaka na sadaka zenu na sisi tuna zaka na swadaqa zetu!
Nyinyi mna funga zenu na sisi tuna swaumu zetu!
Nyinyi mna hija zenu na sisi tuna hija na Umra zetu!
Msilazimishe tufanane wakati dini zetu ni tafauti na hivyo swala zetu haziwezi kufanana na sala zenu!
Zaka na swadaqa zetu haziwezi fanana na zaka na sadaka zenu!
Swaumu zetu haziwezi fanana na funga zenu?
Hija zetu haziwezi fanana na hija zenu!.
Sisi tunafanya ibada kulingana na tulivyofundishwa na mtume صلى الله عليه وآله وسلم wala hatuigi dini ya mtu yeyote kwa sababu
NYINYI MNA DINI YENU NA SISI TUNA DINI YETU katu! Ibada za kiislamu haziwezi fanana na ibada za dini yoyote nyingine.
Sasa kama mnaona nyinyi ndio mnafunga sawasawa endeleeni hivyohivyo na sisi tunafunga kulingana na tulivyofundishwa na mtume wetu
صلى الله عليه وآله وسلم.
Lakini mwisho nawauliza tena swali ambalo hamtaki kulijibu.
Yesu alifunga siku arobaini usiku na mchana!
Nyinyi ni shetani gani aliwafindisha kufunga mchana na kula usiku?!
Andiko la kuruhusiwa kula usiku mumefundishwa na nani?!
Kwanini mnashindwa kumuiga bwana yesu au imani zenu ni ndogo ?!
Makafiri ni wepi hao?
 
Back
Top Bottom