Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo kipindi hiki cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu

Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo kipindi hiki cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu

Swali moja tu la msingi na muhimu sana kupatiwa jawabu sahihi!
Aloyewawekea utaratibu huo wa kufunga ni nani?!
Ni andiko gani linalowaambia kuwa mfungue saa kumi na mbili?
Ni andiko gani linalowakataza mkishafungua msile Tena hadi kesho?!
Kwamfano upande wetu Allaah katuruhusu kula usiku mzima hadi ikifika alfajiri ndio tuache kula na kuanza kufunga.!
Allaah anasema katika suuratul Baqara Aya ya 187 ya kwamba :
"{ ...................وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ ٱلۡخَيۡطُ ٱلۡأَبۡيَضُ مِنَ ٱلۡخَيۡطِ ٱلۡأَسۡوَدِ مِنَ ٱلۡفَجۡرِۖ ثُمَّ أَتِمُّواْ ٱلصِّيَامَ إِلَى ٱلَّيۡلِۚ.................. }
...................Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku........... "
Na usiku kisheria unaanza baada ya kuzama jua na sio saa kumi na mbili.
Saa kumi na mbili kwa mikoa ya Kagera, Kigoma na Rukwa bado ni mchana kabisa.
Na kuhusu daku tumeamrishwa na mtume Muhammad
صلى الله عليه وآله وسلم
katika hadithi aliyopokea Imamu Bukhari na Muslim toka kwa Swahaba Anas bin Maalik kwamba mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema:
" تَسَحَّرُوا ؛ فَإِنَّ فِي السُّحُورِ بَرَكَةً ".
" KULENI DAKU, KWA HAKIKA NDANI YA KULA DAKU KUNA BARAKA"
Kutokana na hadithi hii inakuwa ni Sunna muislamu kutamka mwisho wa usiku na kula angalau tende tatu, au funda la maji , na mtu anayetaka kula na kushiba anaruhusiwa kutokana na aya niliyoitaja hapo juu.
Na sisi tunapofuata maelekezo haya ya Allaah na mtume wake huwa hatujali wakristo na wapagani wanatuonaje au wanasema nini dhidi yetu kwa sababu SISI TUNA DINI YETU NA WAO WANA DINI ZAO.
(Kwanini mnataka ibada zetu zifanane wakati dini zetu ni tafauti?!
Kwa kumalizia nitaje ya kwamba Allaah alishatuambia ya kwamba hata tufanye nini wayahudi na wakristo hawatapata raha na sisi hadi yitakapoingia kwenye dini yao.
Allaah kalibainisha hili ndani ya Suuratul Baqara Aya ya 120 kwa kusema:
" { وَلَن تَرۡضَىٰ عَنكَ ٱلۡيَهُودُ وَلَا ٱلنَّصَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمۡۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۗ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم بَعۡدَ ٱلَّذِي جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ }
Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu".
Ndo maana tunasema mnabadili ratiba ya kula.Maswahaba walikuwa waoga wa njaa na walafi
 
Wewe ulishawahi kupigwa kisa umekula hadharani au unaleta hadithi za Abunuasi?!
Mimi nipo Moshi mjini na ninafunga mimi na waislamu wengine, na hapa mama ntilie na migahawa kutwa nzima watu wanakula hadharani wala sisi hatuoni shida yoyote kwasababu dini yao inawaruhusu kula mchana kama watakavyo!
Sio migahawa tu bali hata vilabu vya walevi na bucha za nguruwe zinafanya kazi mchana wa Ramadhani wala hakuna muislamu anayelalamika wala kunung'unika!.
Sasa habari za kwamba sisi tukiona mtu anakula mchana tunaumia naona kama HADITHI ZA PAUKA PAKAWA!.
Moshi wakristu ni wengi kuliko waislamu
nenda Zanzibar ule hadharani kipindi hichi ndio utaona kipigo chake
mfano hiyo video
 
Mtumishi wa Mungu Samson Ernest kuna huyu umat wa allah anauliza kama mnaweza vumilia njaa hata dakika 3? Najua FPCT hapo Singida Mjini mna mifungo mingi. Kuna ule wa kitaifa wa siku 21 kama ambao sisi TAG tunao wa kitaifa kwa siku 21 kila mwanzo wa Mwaka. Pia kuna mifungo ya kawaida ya kutaniko la mahali pamoja.

Ndugu yangu Lucha binafsi sasa nipo CBC hapa miuji Dodoma na nina funga kila wiki siku 3 kavu kuanzia Ijumaa hadi Jumapili jioni. Hata nikiwa natumia TAG kule GEITA huwa nafunga kavu 3 days lakini pia kuna mifungo ya masaa 12 na masaa 24.

Kufunga kwa mkristu ni kitu cha kawaida pale anapoamua kumnyenyekea na kumtafuta Mungu wake na mara nyingi hatujitangazi kama tumefunga. Kuanzia nikiwa kazini nilikuwa nafunga na kama wenzangu wanakula kazini mi nawaacha na kujitenga wakimaliza kula tunaendelea na kazi otherwise umeandika hii comment kwa mzaha tu mkuu.
Asante, hongera kwa utaratibu uliojiwekea wa kufunga na kuomba, kubishana sana na watu wa namna hii haiwezi kuwa na matunda, hawa ni kuendelea kufundisha au kuhubiri neno kwa usahihi watakutana na Mungu huko huko.
 
Wakiristo si ndio wanafunga ukifika saa 6 mchana wanakula kidogo sasa hapo funga iko wapi
 
Kuna swali hapo Mjoli wa Bwana. Je kuna andiko gani linalowataka wakristo wafunge? Wanasubiri jibu.
Maandiko yapo mengi mno, haya ni baadhi tu;

Kutoka 8
8 Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, Mwombeni Bwana, ili awaondoe vyura hawa kwangu mimi na kwa watu wangu; nami nitawapa watu ruhusa waende zao, ili wamtolee Bwana dhabihu.

Zekaria 10
1 Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.

Mathayo 17
21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]

Mathayo 7
7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
 
Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo wa madhehebu yote yanayofunga kipindi hiki Cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu.

Sijasikia mkristo yeyote akijisifu utakatifu Kwa kufunga kwake.

Sijaona wakristo wakizuia wengine kula hadharani Wala kuonesha kuchukizwa na Hilo

Sijaona wakristo wakihangaika na vikombe vya uji Wala sahani za magimbi muda wa kufuturu.

Sijasikia wakristo wakipiga kelele alfajiri kwamba wanakula chakula Ili waweze kuvumilia njaa ya mchana kutwa Hadi muda wa kufuturu.

Sijaona vijana wa kikristo wakihangaika kwenda kula chakula kanisani kipindi hiki Cha mfungo wao.

Nimechunguza mengi Kwa wakristo na nimegundua wanafanya mambo Yao kiungwana bila kubugudhi wengine.

Nimeambiwa wakristo wanafunga siku arobaini na mwisho wa kula au kunywa ni saa 5 dakika 59 usiku baada ya hapo mkristo hatakiwi kula Wala kunywa ila wanaruhusiwa kusafisha kinywa Kwa mswaki na maji,na kuoga pia.

Hongera sana wakristo,BWANA wenu awabariki nyote katika mfungo wenu na iweni na kwaresma njema
Umeona like yangu huko?
 
Naomba kuuliza,
Hivi utaratibu wa kufunga ktk ukristo umeelekezwa ktk biblia?
Umeseme wakristo mwisho wa kula NI saa 5:59 uck, Hilo NI fundisho la kanisa au fundisho la biblia?
Jirani yangu NI dhehebu la efatha, kanisa la mwingira pale mwenge Dsm. Wao (efatha) wanafunga mwezi wa tano. Nikimuuliza, anasema kwmb hii funga ya kwalezima, NI ya katoliki.
Kanisa lengine lipo tegeta nyuki, linaitwa kanisa halisi la mungu baba. Wao wanasema hawafungi kabisa, kwasababu huyo mungu baba tayari ameshakuja, nyakati zile watu walikuwa wanafunga kwasababu mungu alikuwa yupo mbinguni, lkn kwa Sasa ameshafika, hakuna haja ya kufunga, Hilo kanisa wote wanavaa nguo nyeupe, wanawake wanavaa mashela kama ya Bibi harusi, na kofia kama ya malkia. Wanaume wanavaa suruali na shati mfano wa nusu kanzu. Kama kanzu wanazovaa waislam

FUNGA YA WAISLAM IMEELEKEZWA KTK QURAN, KTK ZILE NGUZO TANO ZA UISLAM, 1 SHAHADA, 2 SWALA, 3 FUNGA YA RAMADHANI, 4 ZAKA, 5 KUHIJI (KWA MWENYE UWEZO) QURAN IMEELEKEZWA NAMNA GANI HIYO FUNGA INAVYOTAKIWA KUWA, MUDA WA KUANZA NA MUDA WA KUFUNGUA. NI QURAN NDIYO IMEELEKEZA. SIYO MSIKITI NDIYO UMEELEKEZA.

Lakini ktk ukristo hii funga ya kwalezima, msingi wake mkubwa umeegemea ktk mafundisho ya kanisa, lkn ndani ya biblia hauwezi ukapata yanayojitosheleza kuhusu kufunga.
Naomba niwasilishe hoja
 
Asili Ya kitu Huwa hakipotei Kwa hiyo Yesu Alisimama kwa Neno la Mungu?
Mi nilijua utaandika kama hivi:

Yesu alisimama kwa Neno lake!
Wakristo hamna tofauti na Wahindi wanao Amini Ng'ombe Ni Mungu Wote Akili kisoda.
Huna Hoja......Mnamuombea mtu amani kila siku hamna uhakika alipo ??
 
Swali moja tu la msingi na muhimu sana kupatiwa jawabu sahihi!
Aloyewawekea utaratibu huo wa kufunga ni nani?!
Ni andiko gani linalowaambia kuwa mfungue saa kumi na mbili?
Ni andiko gani linalowakataza mkishafungua msile Tena hadi kesho?!
Kwamfano upande wetu Allaah katuruhusu kula usiku mzima hadi ikifika alfajiri ndio tuache kula na kuanza kufunga.!
Allaah anasema katika suuratul Baqara Aya ya 187 ya kwamba :
"{ ...................وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ ٱلۡخَيۡطُ ٱلۡأَبۡيَضُ مِنَ ٱلۡخَيۡطِ ٱلۡأَسۡوَدِ مِنَ ٱلۡفَجۡرِۖ ثُمَّ أَتِمُّواْ ٱلصِّيَامَ إِلَى ٱلَّيۡلِۚ.................. }
...................Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku........... "
Na usiku kisheria unaanza baada ya kuzama jua na sio saa kumi na mbili.
Saa kumi na mbili kwa mikoa ya Kagera, Kigoma na Rukwa bado ni mchana kabisa.
Na kuhusu daku tumeamrishwa na mtume Muhammad
صلى الله عليه وآله وسلم
katika hadithi aliyopokea Imamu Bukhari na Muslim toka kwa Swahaba Anas bin Maalik kwamba mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema:
" تَسَحَّرُوا ؛ فَإِنَّ فِي السُّحُورِ بَرَكَةً ".
" KULENI DAKU, KWA HAKIKA NDANI YA KULA DAKU KUNA BARAKA"
Kutokana na hadithi hii inakuwa ni Sunna muislamu kutamka mwisho wa usiku na kula angalau tende tatu, au funda la maji , na mtu anayetaka kula na kushiba anaruhusiwa kutokana na aya niliyoitaja hapo juu.
Na sisi tunapofuata maelekezo haya ya Allaah na mtume wake huwa hatujali wakristo na wapagani wanatuonaje au wanasema nini dhidi yetu kwa sababu SISI TUNA DINI YETU NA WAO WANA DINI ZAO.
(Kwanini mnataka ibada zetu zifanane wakati dini zetu ni tafauti?!
Kwa kumalizia nitaje ya kwamba Allaah alishatuambia ya kwamba hata tufanye nini wayahudi na wakristo hawatapata raha na sisi hadi yitakapoingia kwenye dini yao.
Allaah kalibainisha hili ndani ya Suuratul Baqara Aya ya 120 kwa kusema:
" { وَلَن تَرۡضَىٰ عَنكَ ٱلۡيَهُودُ وَلَا ٱلنَّصَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمۡۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۗ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم بَعۡدَ ٱلَّذِي جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ }
Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu".
Tunaabudu Mungu tofauti na maelekezo tofauti
Kwahiyo hayo ya kwenu Sio ya kwetu
Jua hivyo maana km ni kufunga sisi tuna ibada tofauti tofauti
Soma Daniel, Esta, pia Musa msome plus Yesu mwenyewe
SS we huwezi kuelewa!
Na Tuna funga yetu kasome isaya 58.

Na sisi hatufungi Kwaresma tu
 
Qur
Naomba kuuliza,
Hivi utaratibu wa kufunga ktk ukristo umeelekezwa ktk biblia?
Umeseme wakristo mwisho wa kula NI saa 5:59 uck, Hilo NI fundisho la kanisa au fundisho la biblia?
Jirani yangu NI dhehebu la efatha, kanisa la mwingira pale mwenge Dsm. Wao (efatha) wanafunga mwezi wa tano. Nikimuuliza, anasema kwmb hii funga ya kwalezima, NI ya katoliki.
Kanisa lengine lipo tegeta nyuki, linaitwa kanisa halisi la mungu baba. Wao wanasema hawafungi kabisa, kwasababu huyo mungu baba tayari ameshakuja, nyakati zile watu walikuwa wanafunga kwasababu mungu alikuwa yupo mbinguni, lkn kwa Sasa ameshafika, hakuna haja ya kufunga, Hilo kanisa wote wanavaa nguo nyeupe, wanawake wanavaa mashela kama ya Bibi harusi, na kofia kama ya malkia. Wanaume wanavaa suruali na shati mfano wa nusu kanzu. Kama kanzu wanazovaa waislam

FUNGA YA WAISLAM IMEELEKEZWA KTK QURAN, KTK ZILE NGUZO TANO ZA UISLAM, 1 SHAHADA, 2 SWALA, 3 FUNGA YA RAMADHANI, 4 ZAKA, 5 KUHIJI (KWA MWENYE UWEZO) QURAN IMEELEKEZWA NAMNA GANI HIYO FUNGA INAVYOTAKIWA KUWA, MUDA WA KUANZA NA MUDA WA KUFUNGUA. NI QURAN NDIYO IMEELEKEZA. SIYO MSIKITI NDIYO UMEELEKEZA.

Lakini ktk ukristo hii funga ya kwalezima, msingi wake mkubwa umeegemea ktk mafundisho ya kanisa, lkn ndani ya biblia hauwezi ukapata yanayojitosheleza kuhusu kufunga.
Naomba niwasilishe hoja
an ni maneno ya Waraqah bin NaufAlikopi kila kitu kwenye biblia na kumpa Mudy awadanganye
 
Ndo maana tunasema mnabadili ratiba ya kula.Maswahaba walikuwa waoga wa njaa na walafi
Wewe huwa una funga?
Kama huwa unafunga,huwa unafunga mchana au usiku?

Je,ili wasiwe wamebadili ratiba ya kula ina bidi wafungaje kwa mujibu wako?

Hivi watu wakila usiku kikwenu wanakua ni walafi?

Je,Wewe unaujua vizuri utaratibu wa funga yao kuliko wao? Unataka wa funge kwa utaratibu wao au kwa utaratibu wako?

Kashfa na kejeli juu ya imani isiyokuwa yako haikufanyi wewe kuwa bora na mtakatifu.zaidi inaweza kukufunua na kuonesha una akili na roho ya namna gani juu ya wengine.

Wewe una kwaresma yako,funga kwa utaratibu wako,wao wana ramadhani yao acha wafunge kwa utaratibu wao.

Usipangie watu katika imani yao!
 
Ndo maana tunasema mnabadili ratiba ya kula.Maswahaba walikuwa waoga wa njaa na walafi
Nyie ambao sio waoga wa njaa na walafi tuambie
A. Yatakiwa mfunge kuanzia muda gani hadi muda gani na uweke andiko linaloonyesha maelekezo hayo toka kwa Mingi au hata kutoka kwa Yesu.
B. Kuna mgalatia mwenzenu kasema yatakiwa mfunge hadi saa kumi na mbili halafu hamna kula Tena hadi kesho saa 12.
Ni andiko gani linasema tufungue saa 12 ?!
C. Ni wapi Yesu kakataza mtu akifungua hiyo saa 12 asile tena hadi siku ya pili?!
 
Makafiri ni wepi hao?
Twende kwenye kamusi ya kiswahili sanifu utilize kwa mujibu wa lugha ya kiswahili kafiri ni nani?
Hapa chini nakuwekea picha ya kamusi ya kiswahili sanifu toleo la 3 iliyoyotolewa na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili TATAKI ambayo zamani ilikuwa ukijulikana kama Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili TUKI.
ya chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 
Attachments

  • IMG_20250314_223456_376.jpg
    IMG_20250314_223456_376.jpg
    430.6 KB · Views: 1
  • IMG_20250314_223605_621.jpg
    IMG_20250314_223605_621.jpg
    428.2 KB · Views: 1
  • IMG_20250314_223702_408.jpg
    IMG_20250314_223702_408.jpg
    429.4 KB · Views: 1
Twende kwenye kamusi ya kiswahili sanifu utilize kwa mujibu wa lugha ya kiswahili kafiri ni nani?
Hapa chini nakuwekea picha ya kamusi ya kiswahili sanifu toleo la 3 iliyoyotolewa na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili TATAKI ambayo zamani ilikuwa ukijulikana kama Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili TUKI.
ya chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Hapo kwenye kamusi wameweka maana tatu za neno kafiri sasa hiyo maana ya tatu ndiyo ambayo waislamu tunamaanisha tunaposema neno kafiri kwa mujibu wa dini yetu na kwa mujibu wa lugha ya kiswahili.
 
Back
Top Bottom