Kwa hali ilipofikia Tundu Lisu akae kimya asije akatusababishia machafuko kwa taifa, kama binadamu yeyote ni vigumu kuamini kama anaitafuta nafasi ya uraisi pasipo kulipiza kisasi kwa yale yalitendeka.
Vivyo hivyo kwa watawala wetu ni vigumu kuamini kwamba watakaa kimya eti demokrasia ichukue mkondo wake, ni wazi kwamba kuna hatari ya watawala kuamua liwalo na liwe endapo Tundu Lisu ataungwa mkono na hivo kupelekea mkorogano mkubwa kama tunavyo shuhudia kwenye mataifa mengine.
Mimi binafsi nautambua mchango mkubwa wa Mh. Tundu Lisu lakini kwa hali ilipofikia namuomba akae kimya aachane na harakati za kisiasa.
Kuna msemo wa kiswahili unaosema "Ukilikoroga utalinywa"
Nawasilisha.
Sent using
Jamii Forums mobile app