Binamu Bananga: CHADEMA tunakutana kujadili mahojiano ya Rais Samia na BBC ili kujibu nini? Nasisitiza tusikurupuke

Binamu Bananga: CHADEMA tunakutana kujadili mahojiano ya Rais Samia na BBC ili kujibu nini? Nasisitiza tusikurupuke

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Ushauri aliotoa Binamu Bananga kwa CHADEMA kuhusu Mahojiano ya Rais Samia na BBC

Makamanda habari za jioni? Naamini wengi tumesikiliza mahojiano ya mama Samia na Kikeke, Nimeona Kaka yangu Lema ameandika Mahali kwamba Chama Kitakutana kumjibu, nimeshtuka kidogo, tunataka kujibu nini? Mimi naendelea kusisitiza tusikurupuke.

Najua mtasema natetea CCM kwasababau ya Ubunge wa Hawa, lakini mimi nashauri kwasababu ya mapenzi yangu kwa CHADEMA, Mama Samia kasema kuna Uhuru wa Habari, Baada ya Uchaguzi tujenge Nchi, Kesi ya Mbowe ilikuwepo lakini upelelezi haukuwa umekamilika, pengine ndio sababu ya Mwenyekiti kuwa nje.

Kati ya hayo aliyosema lipi la uongo? Kuna Vyombo vya Habari vilivyofungiwa Tanzania? Hapana. Wote humu tunajua kwamba ni kweli kesi ya Mbowe ilikuwepo, sio ya sasa, amesema uongo hapo? Hapana. Kuhusu hili la kujenga Nchi sisi CHADEMA ndio tunalichelewesha kwa migogoro isiyoisha. Sasa kama ukweli ni huu, tunataka kumjibu nini?

Imekuwa ni kawaida sana kwa Chama chetu kucheza ngoma ya CCM, Hivi kweli leo sisi CHADEMA ndio wakutaka Rais aingilie uhuru wa mahakama? Tatizo tulilolipigia kelele enzi za Mwendazake, tunataka lirudi tena, Tumehubiri Utawala wa Sheria na Uhuru wa Mahakama kwa miaka 6 halafu ndani ya miezi minne ya Samia tunataka kubadili gia angani kwa kushinikiza huyu Mama kuingilia Mahakama?

Maamuzi ya Mahakama hayapaswi kuingiliwa na Rais, Mama Samia kasema Issue ya Mwenyekiti ipo mahakamani, hawezi kuiingilia Mahakama, Kauli hiyo ina shida gani? Hatuoni kama kutaka aingilie Mahakama ni kutaka avunje Katiba? Kwanini tudai katiba Mpya kwa kuvunja Katiba ya Sasa? This is not right, I am sorry guys kama nitawakwaza lakini we really need to change our think tanks.

Sio kila kitu cha kujibu, tusijichoreshe, Chama kimestuck kama Tekno, hakuna kazi nyingine zinazoendelea, CHADEMA ni MSINGI hatujui hata Documents ziko wapi, Sera mbadala ishakuwa Zilipendwa, Mwenyekiti kuwa mahabusu siku 20 Chama kimeparalaizi kabisa, Hivi kweli Siku Mbowe akitoka CHADEMA, chama kitabaki hai?

Makamu Mwenyekiti Kaka yangu Lissu toka huko Ulipo, tunakuhitaji uwanjani, Maria Space na Clubhouse ni vijiwe vya story tu, havina maajabu, Lema anasema watu wasinywe bia, wasinywe maji ya kunywa, wasile hotelini, Yaani kweli huu ndio mkakati wa Chama kikuu cha upinzani? Kama tuko serious, Tusiwe na mipango unrealistic kama huu wa kaka yangu wa Canada.

Lema unasema hayo kutokea Canada, labda nikuulize, tukigomea maji huku Tanzania ili Serikali ikose pesa, Wewe na familia yako huko Canada mtagomea nini ili Serikali ya Tanzania ikose pesa? Au nyie mtaendelea kuishi kama kawaida wakati sisi tukiisoma namba kwa kugomea Dawasco huku? Bro kaa chini ufikirie tena wazo lako.

Narudia kushauri, tuachane na press za kila siku, Kama tunataka Mbowe atoke tukubali kwamba propaganda za Twita haziwezi kubadili kilichoandikwa kwenye Hati ya Mashtaka, tuna wanasheria wazuri, wasimame na Mwenyekiti, tuache sanaa.

Yangu ni hayo kwa leo, Samahani kwa watakaokwazika. Tusipoambiana ukweli Chama kitakufa.

Screenshot_20210810-112158.png
 
Kweli Kaka naona umeamua kusimama na Mke wako, endelea kupambana kiongozi kwani poso za ubunge ni sana hata katika kipindi hiki ambacho wanaume wengi kama wewe tunategemea ada za shule za watoto wetu, nyumba na mafuta ya gari zigharamiwe na wake zetu.
Kweli Kaka naona umeamua kusimama na Mke wako, endelea kupambana kiongozi kwani posho za ubunge ni muhimu sana hata katika kipindi hiki ambacho wanaume wengi kama wewe tunategemea ada za shule za watoto wetu, nyumba na mafuta ya gari zigharamiwe na wake zetu.
 
Plz tungemjua na huyo covid wake ingependeza. Japo huyo jamaa nikimwangalia tu usoni akili yake haipo sawa.
 
Ushauri mzuri sana ila viongozi wa chadema watukutu sana!! bado wana chembe chembe za kigaidi sijui kama wata uelewa ushauri huu, ila kwa sasa kwa hali inayo mkabili Mbowe hawana budi kubadilika.
 
Ushauri aliotoa Binamu Bananga kwa CHADEMA kuhusu Mahojiano ya Rais Samia na BBC

Makamanda habari za jioni? Naamini wengi tumesikiliza mahojiano ya mama Samia na Kikeke, Nimeona Kaka yangu Lema ameandika Mahali kwamba Chama Kitakutana kumjibu, nimeshtuka kidogo, tunataka kujibu nini? Mimi naendelea kusisitiza tusikurupuke.
Ukweli upi hapo umetuambia? Chama kife kivipi kwa mawazo yako chama kitakufa? Swali kwako ebu ni tuelezi watu ambao tayari wamehukumiwa kwa hiyo kesi ya ugaidi maana Samia kasema tayari wengine wamehukumiwa wataje waliohukumiwa kwanza, tuanzie hapo
 
Angalau huyu anatumia akili, siyo kama BAVICHA wengine akili mfukoni. Wanafuata upepo unaopulizwa na Mbowe kupitia vijana wake.
Wewe mwenyewe huna Akili timamu unawezaje kujua asiye na Akili? Kipimo cha wewe kuwa na Akili ni kutukuza uonevu unyanyasaji uovu kwa wapinzani kisha utake wakae kimya?kuendekeza kuwabambikia kesi wapinzani ndiyo kuwa na Akili? Kukandamiza demokrasia ndiyo kuwa na Akili? Wapo wapi makaburu wapo wapi akina Bokasa chiluba Abacha Gadafi Sadam Hussein Elbashiri Iddy Amin dada magufuli? Kuna mabaya yasiyo na mwisho?
 
Ushauri mzuri sana ila viongozi wa chadema watukutu sana!! bado wana chembe chembe za kigaidi sijui kama wata uelewa ushauri huu, ila kwa sasa kwa hali inayo mkabili Mbowe hawana budi kubadilika.
Ushauri upi? Kwa kosa lipi? Ushauri kwa makosa bandia ya kubambikiwa ni ushauri wa kijinga jinga huo, ugaidi ni Polisiccm kwenda kuwapekua wapinzani saa nane usiku pasipo wapinzani kuwa na ndugu zao mashahidi wa kushuhudia upekuzi haramu ukifanyika
 
Chadema wanaendelea kumchekea huyu kiumbe sijui kwa nini?kama ni kweli kayasema haya nashauri afukuzwe haraka chamani.Kwanza mkewe ni msaliti tuanzie hapa ni wapialipata barua ya utambulisho wake?inamaana mikakati yote ya usaliti Bananga anaifahamu lakini kama alivyosema alichagua upande wa mke wake ilimradi mkono uende kinywani.Chadema muondoeni huyu MTU.
 
Dah, tuna bahati mbaya kiumbe kama huyu kuwa associated na Chadema. Anatumia nafasi hiyo vibaya! Hopeless kabisa! Yaani analazimika kuwafurahisha CCM ili mke wake asinyanganywe tonge!
Wasaka uteuzi Huko CCM wapo tayari kujitoa fahamu ili mradi mwenyekiti wa CCM awaone awazawadie uteuzi
 
Chadema wanaendelea kumchekea huyu kiumbe sijui kwa nini?kama ni kweli kayasema haya nashauri afukuzwe haraka chamani.Kwanza mkewe ni msaliti tuanzie hapa ni wapialipata barua ya utambulisho wake?inamaana mikakati yote ya usaliti Bananga anaifahamu lakini kama alivyosema alichagua upande wa mke wake ilimradi mkono uende kinywani.Chadema muondoeni huyu MTU.
Dawa yake ataipata humu humu JF akisoma maoni ya wapenda demokrasia lazima atajutia ushauri wake wa kijinga
 
Back
Top Bottom