Binamu yangu na safari hadi ya kuwa mtendaji

Binamu yangu na safari hadi ya kuwa mtendaji

MIRIMA

Senior Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
126
Reaction score
357
Mawasilino na binamu

Mimi....Hongereni binamu kwa uchaguzi huko nyumbani.

Binamu....Asante ndugu yangu ,nilikuambia hatuwezi kukubali kutangaza mpizani hata kama ameshinda.

Binamu....Zengwe tulianza mapema hata kabla ya uchaguzi au huangali taarifa ya habari huko mjini.

Mimi....Nimewaona hata huku itakuwa mlipewa maelekezo kutoka juu

Binamu...Huwezi kupingana na serikali na ili ulinde kibarua chako lazima utekeleze ..

Mimi...Ok binamu ,Mzee kaniambia wanakijiji wanakuchukia unapewa uhamisho kuondoka hapo kwa ajili ya usalama wako

Binamu....Nimepewa likizo nipo Mwanza nasoma upepo kama hali ni mbaya nitaomba nihamishwe niende sehemu nyingine.

Mimi ....Sawa binamu lakini kumbuka uchaguzi 2020 kidogo wakutoe roho ukakimbia na kuhama kule , namba hazidanganyi mtu akishinda kwa idadi ya kura Kwa nini usitangaze huyo huyo alieshinda .

Mimi.. .Kuna siku wananchi watakugeuka kwa ujinga huo ukaacha familia Yako ,hao wanasiasa hawatakukumbuka wataendelea kufurahia wao na familia Yao wewe wanao watabaki tunaangaika nao huku wanateseka ,siku zote nakukumbusha take care hao Wana siasa wakishashinda wanajijali wenyewe na familia Yao

Binamu ....wewe hujui siasa na haujasomea endelea kupima damu

Mimi...sawa binamu kazi njema
 
Back
Top Bottom