Bingwa mtetezi Simba SC out kombe la shirikisho!!

Nimewaangalia simba jana wakifungwa lakini sikushtuka kwa sababu matatizio wanayalea wenyewe. Kwanza wachezaji hawana morali kabisa ukiondoa kichuya, nyoni na mlipili hao waliobaki walikuwa wanacheza kama wamelazimishwa. Pili Omog huwa hana mbinu mbadala kabisa. timu ikibanwa hautokaa uone imebadilisha mbinu. Tatu simba haina washambuliaji wa mwisho wenye vipaji binafsi vya ufungaji au hata wenye kufosi goli lipatikane. Akishakosekana Okwi au akibanwa na mabeki simba kwishney.

Makosa mawili makubwa viongozi wa simba waliyofanya ni kumuondoa Mayanja na kumuacha Omog. Kosa lingine ni kupoteza muda mwingi kumsajili kwasi badala ya kushughulikia washambuliaji wapya wa kumpa boko changamoto na kuiewka timu kambini mapema kujiandaa na mechi dhidi ya green wariors.

Simba ukiiangalia vizuri dakika zake ni 60 tu wanaanza poteana hamna pumzi wala stamina hili Omog limemshinda kabisa. wakikutana na timu zinazocheza mpira wa nguvu na zenye pumzi hasa timu za jeshi simba hawanaga ujanja. Pia hawachezi kitimu kabisa kila mtu anacheza anavyojua yeye.

Kama kweli wanataka ubingwa mwaka huu wamtimue Omog wamrudishe mtaalamu mayanja. Vile vile wamtimue yule msemaji wao sijui naitwa nani nimesahau jina lake. Ila kwa kukosa washambuliaji mahiri wa kati ubingwa naona kama utarudi yanga tena au kwenda azam.
 
Msemaji sio mwalimu
 
Man United katolewa na Bristol City tena ndani ya dak 90,kikosi cha man u ni mara kumi ya kikosi cha bristol city,mpira unadunda inategemea utadundia upande upi kati,kulia,au kushoto
Kama mpira unadunda nenda kaudunde baharini.
 
Mlisha ambiwe siku nyingu tu kuwa Simba na Yanga ni majina tu, si lolote si chochote. We umeona wapi timu inaongozwa na Mze mmoja au wanaharakati fulani ili ipate ushindi? Time has come hizi timu zife tu.
Inatolewa Simba unahusisha Yanga.
Haikubaliki.
 
Jana sikuamini macho yangu niliposhuhudia Timu ya darajala pili na hata haina jina kuifunga Simba (Mnyama). Pamoja na usajili wa 1bn bado hamkuambulia kitu. Tafuteni kipa ndiye anayewaangusha. Naona kimo chake ndicho kinacholeta dosari. Ni mfupi sana na lile goli angeweza kulizuia.
 
man u bingwa wa uefa ama ueropa kijana??sisi tunazungumzia kutolewa FA hata Man u katolea kwenye kombe hilohilo
Basi ndiyo ufananishe maziwa na tui? Mmoja ni maziwa, ametolewa kombe la mtoano hatua ya robo fainali huku akiwa bado bingwa wa hilo kombe ulilolisema kwa usahihi. Na bado kocha wake yuko salama. Mwengine ni tui, ametolewa kwenye kombe la mtoano hatua ya kwanza, hana ubingwa wowote aliosalia nao. Na kibarua cha kocha wake kikaota nyasi. Ni kichekesho mmojawapo kufanywa kuwa ndio mfano hai wa mwengine!
 
Mlisha ambiwe siku nyingu tu kuwa Simba na Yanga ni majina tu, si lolote si chochote. We umeona wapi timu inaongozwa na Mze mmoja au wanaharakati fulani ili ipate ushindi? Time has come hizi timu zife tu.
Sema Simba, wacha kutanua goli.
 
hivi wadau kukosekana kwa Okwi,Niyonzima na Mwanjale ndo kumewanyima simba ushindi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…